klabu ya michezo yenye thamani zaidi duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

klabu ya michezo yenye thamani zaidi duniani

Discussion in 'Sports' started by Dj Khalid, Jul 15, 2011.

 1. Dj Khalid

  Dj Khalid Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Mabingwa wa ligi kuu ya England Manchester United wametajwa na jarida la FORBES kuwa ndio klabu ya michezo yenye thamani kubwa zaidi duniani.

  The Red Devils wanatajwa kuwa na thamani paundi billion 1.165 ikiwazidi vilabu tajiri kama Dallas Cowboys na New York Yankees.

  Thamani ya United inahusisha timu, uwanja, mapato na mikataba ya udhamini.
  Taarifa hizi ni nzuri kwa familia ya Glazer ambayo ilinunua klabu hii kwa £790m in 2005, ingawa bado wana deni la linalokaribia £500.
  Mapato ya matangazo ya United yamechangia sana kwa timu hii ku-top the chart, wakiwa wanapata £80m kwa mkataba wa miaka 4 kwa udhamini wa jezi waliosaini na kampuni ya bima ya Aon pamoja na mkataba mwingine Nike wa miaka 13 wenye thamani ya £300m.

  Real Madrid walishika nafasi ya pili kwa vilabu vya soka wakiwa na thamni ya £900m.
  Huku Arsenal wakiwa nafasi ya saba wakiwa na thamani ya £740m.


  Chelsea walishika nafasi ya 46, na timu nyingine za soka zilizoingia katika top 50 ni Bayern Munich(19), AC Milan(34) na Juventus wakashika nafasi ya 49.
  Na timu inayoaminika kuwa ni bora ulimwenguni kwa sasa (Barcelona) wameshika nafasi 26 wakiwa na thamani ya £606million.  VILABU 10 VYA MICHEZO VYENYE THAMANI KUBWA
  1. Manchester United £1.165billion
  2. Dallas Cowboys £1.13bn
  3. New York Yankees £1.06bn
  4. Washington Redskins £960million
  5. Real Madrid £900m
  6. New England Patriots £850m
  7. Arsenal £740m
  8. New York Giants £734m
  9. Houstan Texans £727m
  10. New York Jets £708m
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hapo ukitoa deni la manchester la p.mil 500 anabaki kama na p.mil 665 pungufu ya arsenalp.mil750
   
 3. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,518
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135

  Safi sana hiyo ndiyo hesabu....unapotafuta Finacial position ya team ama kitu chochote.. Take off Short & Long term liabilities then give us financial position of an entity. so kwa hapo Man U hakuna kitu.
   
 4. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  msikurupuke...
  Hiyo orodha ni ya vilabu vya mpira wa miguu ''soccer au vilabu vya michezo including Basketball, Hockey, American Football, Baseball na mingine?
   
 5. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  then mkimaliza hapo mkapekue ni klabu gani ya Soka yenye mafanikio ya kimataifa zaidi?
   
Loading...