KKKT yawasihi madaktari kurejea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KKKT yawasihi madaktari kurejea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by R.B, Jun 28, 2012.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,166
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  Daniel Mjema, Moshi
  ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini ya Dk Martin Shao amewasihi madaktari waliogoma katika hospitali mbalimbali nchini ikiwamo KCMC kurejea kazini.

  Hospitali ya Rufaa ya KCMC inayoendeshwa na Shirika la Kidini la Msamaria Mwema (GSF) la KKKT ni miongoni mwa hospitali zilizokumbwa na mgomo ulioanza Jumatatu wiki hii.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Askofu Shao alisema kuwa hata ikiwa madaktari hao wana hoja za msingi kiasi gani, zinaweza kupoteza ushawishi iwapo watatumia njia zisizo halali kushinikiza madai yao.
  “Walitakiwa kuwa waungwana, walipaswa kujua wito wao kwa maana ya maisha ya wagonjwa kwanza maslahi baadaye. Njia bora ya kutatua migogoro ni mazungumzo, ”alisema Askofu Shao.

  Askofu Shao alisema anazo taarifa za madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya KCMC kuingia katika mgomo lakini, akasema suala lao linashughulikiwa na Serikali.

  “Hili la madaktari walio mafunzoni tunashukuru linaendelea kutufanyiwa kazi na Serikali, hata mahakama imetoa amri yake, nawashukuru madaktari bingwa na wanaosomea ubingwa wako kazini,”alisema.

  Hali ya utoaji huduma katika hospitali hiyo imezidi kuzorota baada ya madaktari wanaofikia 80 kugoma kurejea kazini huku taarifa zikieleza kuwa hadi jana walikuwa hawajarejea kazini.
  Baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamepewa rufaa kutoka hospitali mbalimbali kwenda KCMC, walijikuta wakirudishwa walikotoka kutokana na mgomo huo unaoendelea.

  Mbali na kutopokelewa kwa wagonjwa wapya wanaohitaji kulazwa, kliniki zote za wagonjwa wa kisukari, Ukimwi na waliofanyiwa operesheni zimefungwa rasmi kutoa huduma kwa wagonjwa.

  Mgomo wa madaktari ulianza mwanzoni mwa wiki hii wakidai kutotekelezwa kwa madai yao ya maslahi bora kama walivyoahidiwa na Serikali kupitia vikao vya upatatishi, hata hivyo Serikali imepeleka suala hilo mahakama ya kazi kutafuta ufumbuzi ambapo leo itatoa tamko bungeni.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Huyu Askofu Martin Shayo naye asiwafundishe watu uoga hata punje!

  Yeye anaona alichofanyiwa Dr. Steven Ulimboka ni haki ya kibinadamu?

  Yaelekea huyu Askofu ana usingizi!
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Siku hizi hakuna kazi ya wito, hata hao maaskofu, wachungaji, mitume wate wako kimaslai zaidi.
  Sembusse madaktari, ambao wametumia miaka saaba kusomea hiyo taaruma.

  yaani unaaenda shule na mtu, ukirudi mwenzako ameshakuwa mbunge maarufu, wakati wewe bado unakula kwa baba. Watu katika kada hiyo na walimu wanatakiwa kulipwa vizuri.
   
 4. j

  jigoku JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Askofu nawewe!tena wa kanisa kubwa hivyo,sikuungi mkono bali naunga mkono mgomo wa madaktari,tena nawashauri hata madaktari bingwa hapo KCMC wajiunge katika mgomo unaoweza kutuletea mabadiliko na mapinduzi yenye tija katika sector ya afya hapa TZ.afya haiitaji propaganda wakuu,afya inahitaji facts,mkipanga sera zitekelezeke,mkiahidi mtekeleze,afya sio habari ya kuambia tutawajengea barabara za angani,kigoma nitaifanya kuwa kama dubai,umeme utakuwa historia.NO,hapana,hatuwezi kuendelea katika misingi hii kila siku bila ukomo.
  Natoa rai kwa watanzania wote ifike mahali tukatae kupuuzwa,tukatae kudharauliwa na watu tunaowaweka madarakani ili watupangie safu ya uongozi kwa maslahi ya umma,mwisho wa siku wanatupangia safu ya viongozi mafisadi wanaotupumbaza kwa kutuambia kazi ya madaktari ni wito hivyo wanapashwa kufanya kazi kwa malipo kiduchu na wala mazingira yao ya kazi hayahitaji kuboreshwa tu kwa sababu kazi yao ni ya wito.Hivi niulize,Ubunge na u-daktari ni ipi hasa kazi ya wito?maana Ubunge hauhitaji usomee,sasa hapo si ni wito tu uliojaliwa na mwenyezi Mungu wa kuweza kuongea sana mbele ya majukwaa ya kisiasa?hivi ukiwa muongeaji sana tena mwenye kuweza kutukana kama Lusinde L wa jimbo la Mtera nako kunahitaji ukasome miaka 6 -hadi 7?na je kati ya kina lusinde wa bungeni na madaktari wetu ni wepi wana mazingira mazuri?hivi jengo la Bunge lina gharama kiasi gani?hivi ubora wa jengo la bunge linalingana na hospitali gani TZ?hivi daktari gani anapewa diplomatic passport kama wabunge?hivi ni madaktari wangapi wamepewa mikopo ya mashangingi kama waliyonayo kina lusinde,maji marefu,Wasira na wengine wote?hivi ni madaktari wangapi wamefanya kazi kwa muda wa miaka michche kama aliyofanya waziri aliyetemwa-Maige na kisha akanunua nyumba ya billioni moja?leo wakidai mazingira ya kazi yaboreshwe,wakidai vitendea kazi vinunuliwe kwenye mahospitali,vifaa tiba vijae mahospitalini,na maslahi yao binafsi yaongezwe tuna piga kelele,hivini haki kweli tunawatendea madaktari wetu na hata wagonjwa wanaokufa kwa kukosa huduma?hivi huu wito tunaousema ni wito upi?na maana halisi ya wito ni nini wakuu mnisaidie?hapana hapa kuna kasoro ambayo lazima irekebishwe na wananchi wote tusio sehemu ya mafisadi.
  Nawasilisha wakuu
   
 5. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Njoo ufanyiwe maombi.
   
 6. T

  Talklicious Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tena asiongee mana ni fisadi kuliko jina lenyewe halafu aache kudanganya umma kuna rafiki yangu ni resident hapo hata kazini kabisa hakanyagi halafu anajifanya kusema anashukuru resident doctors hawajagoma! Yaani siku hizi hawa viongozi wawe wa siasa au dini hamna hata wenye unafuu sijui nani kailoga Tanzania?!
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Siyo kufundisha watu uoga mkuu! Huu Mgogoro wa madaktari unaathiri pia KKKT, ukizingatia hata madaktari KCMC nao wamegoma!
   
 8. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,166
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  mdhalau mwiba................................................ :israel:
   
 9. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,927
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  madaktari wana hoja lakini wananchi ndio wanaumia wakuu.
   
 10. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Daini haki zenu kwa wanasiasa, ndo mliwapigia kura wawaakikishie huduma za afya vinginevyo tuendelee kujiju tu.
   
 11. Electron

  Electron Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Warudi wakati sirikali imewafukuza....... mbona kachelewa kama ana akili na anauvuvio si aishauri serikali iwarejeshee kwanza usajili, ndipo awombe hao madaktari warudi...
   
Loading...