Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,670
- 218,173
Wanaosimamia Kanisa la KKKT kwenye Jimbo la Mashariki na Pwani wameingia matatani kwa kuhamisha hovyo watumishi wao wakiwemo Wachungaji na Wainjilisti .
Taarifa za Uhakika kutoka kwa waumini wa kanisa hilo zinadai kwamba hata familia za watumishi kwa maana ya watoto wanaosoma shule mbali mbali hawana uhakika wa shule watakazomalizia masomo yao , kwa vile wazazi wao ambao ni watumishi wa Mungu waweza kuhamishwa hata mara nne kwa mwaka , sasa hoja ni hii , wawezaje kuhamisha watoto shule mara zote hizo kwa mwaka mmoja tu ? Taarifa zingine zinadai kwamba kuhamishwa hamishwa kwa wachungaji hao kunahusiana sana na Mahusiano yao na viongozi wa juu , wanaoenda nao sawa hawasumbuliwi lakini wale wanaoonekana kwenda kinyume na mambo binafsi ya viongozi huhamishiwa kusiko na Network .
Yawezekana ni kweli kwamba utumishi wa Mungu ni wito na kwamba Wachungaji na Wainjilisti hawachagui pa kutoa huduma , lakini kuhamisha watu hawa kila baada ya muda mfupi hakulijengi kanisa hilo bali kunaleta manung'uniko , kuna haja ya VIONGOZI WA MASHARIKI NA PWANI KUJITAFAKARI KAMA MAAMUZI YAO YANASUKUMWA NA KAZI YA KITUME YA MWENYEZI MUNGU AU NI MATAKWA YAO BINAFSI .
NOTE : Niko Tayari kusahihishwa .