KKKT kwachafuka: Kikosi maalum chaundwa kuchunguza tuhuma za wachungaji kujihusisha na USHOGA.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,374
2,000
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, limeunda kikosi kazi kuchunguza tuhuma za baadhi ya Wachungaji na Wainjilisiti wa kanisa hilo, wanaotuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kikosi hicho kimeundwa wiki iliyopita na Askofu wa Kanisa hilo, Dk. Frederick Shoo, ambaye pia ni Mkuu wa Kanisa la KKKT, kutokana na taarifa za kuwapo kwa baadhi ya watumishi hao wa kwenda kinyume na mafundisho ya Mungu.

Taarifa za uhakika toka ndani ya Kanisa hilo na zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa Dayosisi hiyo, zinadai kuwapo kwa Mwinjilisti mmoja (jina linahifadhiwa) anayehudumu katika moja ya sharika za dayosisi hiyo, anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Inadaiwa kuwa Mwinjilisti huyo amekuwa akiwatumia vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kama boda boda kufanya nao mapenzi kisha huwalipa ujira wa kati ya Sh 15,000 hadi Sh. 20,000 kwa tendo moja na kwamba amewahi kukiri kujihusisha na ushoga.

Akizungumza taarifa hizi, Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Ather Shoo, amesema kuwa kutokana na madai hayo kuwa mazito, ni vigumu kwa mkuu wao kuzungumzia tukio hilo kabla ya kuwa na taarifa sahihi.

Amesema kwamba anaomba kupewa muda wa wiki moja ili kikosi alichokiunda kuchunguza tuhuma kiweze kumaliza kazi yake na kuwa katika nafasi nzuri ya kutoa kauli kuhusiana na kashfa hiyo.

“Msimamo wa kanisa siyo wa dayosisi tu, ni KKKT kwa ujumla kwamba tabia hiyo haikubaliki na inakemewa, hivyo tunaomba mtupe wiki moja maana hatuwezi kujua kwa sasa kama vitendo hivyo vipo au havipo, ndiyo maana tumetuma watu wetu wakachunguze na baada ya hapo Baba Askofu atalitolea maelezo,” anasema Shoo.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa miaka michache iliyopita, Mwinjilisti huyo aliwahi kukumbwa na kashfa hiyo baada ya kubanwa na mkuu wake wa kazi, ambaye ni Mchungaji Kiongozi katika usharika anaohudumu, aliweza kukiri kujihusisha na vitendo hivyo lakini aliomba msamaha na kuahidi kutorudia.

Baadhi ya Wachungaji (majina yanahifadhiwa) wamedokeza, kuwapo na taarifa za baadhi ya wachungaji na wainjilisti wenzao kujihusisha na vitendo hivyo na kulitaka kanisa kutowaonea haya, kuwafichua ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi.

“Ushoga upo na wanaofanya hivyo vitendo wanafahamika lakini huwezi ukalizungumzia kwa uwazi kwa sababu kufanya hivyo ni kulivua nguo kanisa na waumini wake ambao wamekuwa wakiwaamini viongozi wao,” anasema mchungaji.

Source: Jamhuri.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
34,502
2,000
Mchungaji avuliwa nguo na Polisi
Story ya siku nyingi sana na wale polisi walishafukuzwa kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom