Wakati tunaisubiri hiyo historia, mi najua Dr Kiiza Besigye alikuwa Kanali wa Jeshi na alikuwa daktari wa Rais Yoweri Museveni.
Kumbuka Museveni ame spend maidha yake ya ujana Tanzania, amesoma University of Dar es Salaam. Mipango yote ya kuvamia Uganda imefanyika Tanzania akiwa na vijana wenzake kina Besigye, Paul Kagame na marehemu John Garang wa Sudan Kusini ambaye pia alisoma Tanzania tangu sekondari hadi UDSM.
Kiswahili kilipata nguvu katika jeshi la Uganda baada ya majeshi ya Tanzania kuvamia Uganda na kumng'oa Rais Idd Amin madarakani mwaka 1979.
Baada ya hapo, majeshi ya Tanzania yalikaa Uganda kwa miaka kadhaa, hata Rais Milton Obote aliporudi.
Hata hivyo kiswahili kilipata pigo Uganda kwa kuwa watu waliona ni lugha ya kikatili iliyotumika jeshini. Wengi hawakupenda kujifunza.
Mpaka leo kiswahili ni lugha rasmi jeshini, lakini wananchi wa kawaida hawaipendi.