Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,850
Kuwa mwanasiasa Uganda lazima uwe na wito toka kwa mungu.Kizza toka amedumbukiza kura yake kwenye box amekuwa mtu wa korokoroni tu.
Leo tena Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha (FDC) Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa polisi nchini Uganda.Huku Rais Museveni akijitapa ushindi wake ulishangiliwa na waganda wote wakiwa ndani.
Nimejiuliza huko ndani aliwaona wakishangilia ushindi huo?
Kama kweli alishinda kihalali na anayo sapoti ya wananchi,Mbona anaogopa kivuli cha Kizza?
Africa na demokrasia za maigizo!