Kizungumkuti cha Dowans na TANESCO kinaendelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizungumkuti cha Dowans na TANESCO kinaendelea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 26, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Tanesco, Dowans waendelea kuvutana mahakamani [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] S[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 25 January 2012 20:37 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  James Magai
  Mwananchi

  MVUTANO mkali baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya Dowans, kuhusu hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoamuru Tanesco iilipe Dowans zaidi ya Sh 94 bilioni, bado unaendelea.

  Mvutano huo unafautia hatua ya Tanesco kutafuta njia za kisheria baada ya kuomba kibali cha kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga hukumu na kuepukana na malipo hayo, lakini Dowans nayo ikaendelea kuibana kwa kuiwekea pingamizi ili inyimwe kibali hicho.

  Septemba 28 mwaka jana, Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, aliamua tuzo ya Dowans iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), isajiliwe ili kuwa hukumu halali ya mahakama hiyo.

  Kwa uamuzi huo, Tanesco sasa inatakiwa iilipe Dowans Sh 111 bilioni badala ya Sh 94 bilioni za awali.

  Tanesco inapaswa kulipa fidia hiyo pamoja na riba ya asilimia 7.5.

  Hata hivyo shirika hilo la umeme limeeleea kutokuridhishwa na hukumu hiyo na hivyo kutoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

  Maombi ya kutaka kibali cha kukata rufaa hiyo, yalitarajiwa kuanza kusikilizwa jana na Jaji Dk. Fauz Twaib lakini mahakama ilishindwa kuyasikiliza baada ya Dowans kuweka pingamizi, ikiomba mahakama isiipe Tanesco kibali.

  Dowans iliiwekea Tanesco pingamizi hilo mwezi huu ikidai kuwa kwa mujibu wa mkataba baina ya pande hizo, hukumu ya ICC haiwezi kukatiwa rufaa.

  Ni hoja kama hizo ilizozitoa Dowansa wakati wa pingamizi la Tanesco kutaka Mahakama Kuu isiisajili tuzo yake na baadaye Jaji Mushi alikubaliana na hoja za Dowans na kuamuru tuzo hiyo isajiliwe.

  Jana Jaji Dk Twaib aliziambia pande hizo mbili kuwa mahakama haitaweza kusikiliza maombi ya Tanesco kuhusu kibali cha kukata rufaa hadi hapo pingamizi la Dowans litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

  Jaji huyo, alizitaka pande hizo, kuwasilisha hoja zao kwa njia ya maandishi na kwamba pingamizi hilo litaamuliwa Februari 16 mwaka huu, baada ya kupitia hoja zote.

  Ikiwa mahakama itatupilia mbali pingamizi la Dowans, basi Tanesco itapewa kibali cha kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

  Lakini kama mahakama itakubaliana na pingamizi la Dowans basi harakati za Tanesco kujinusuru katika malipo hayo kwa njia za kisheria zitakuwa mashakani.

  Hukumu ya Jaji Mushi ilionekana dhahiri kwenda sambamba na kile alichowahi kukisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema kuwa hakuna uwezekano wowote wa kisheria kuepuka malipo hayo.

  Wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama alisema hadi wakati hukumu hiyo inatoka, Tanesco ilipaswa kuilipa Dowans kiasi cha Sh 111bilioni badala ya Sh94 bilioni.

  “Fidia ya awali katika uamuzi wa ICC ilikuwa ni Dola za Marekani 65milioni, lakini kwa sasa ukiweka na riba ya asilimia 7.5 fidia hiyo imeongezeka hadi takribani Dola za Marekani 72milioni ambazo ni kama Sh111bilioni,” alisema Fungamtama.

  Katika hukumu yake Jaji Mushi alisema baada ya kupitia mwenendo na hoja za pande zote nimebaini kwamba si sawa kwa mahakama hiyo kuingilia uamuzi wa ICC.

  “Hivyo ninaagiza kuwa tuzo hiyo isajiliwe na iwe huku halali ya mahakama hii,” alisema Jaji Emiliani Mushi ambaye kabla ya kusoma hukumu hiyo alisema kuwa anatambua kuwa suala hilo limekuwa na msukumo mkubwa wa kisiasa lakini akabainisha kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa sheria.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wapi tunakwenda na nini tunahitaji?
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Hapa delay tactic lazma itumike hadi tumsafishe Lowassa atakate kabisa, akiwa kwenye kiti cha enzi anaweza akajitolea kuzilipa kimyakimya ili asukumize mikataba mingine!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  ...Halipwi mtu mpaka kieleweke. Bilioni hizi 94 zilitakiwa kulipwa December 2010 hivyo ni zaidi ya mwaka sasa na zilithibitishwa kwamba zinastahili kulipwa na Ngeleja, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu Pinda, lakini kelele za walipa kodi katika kila kona ya nchi zimesababisha pesa hizo kutolipwa haraka kama ambavyo mafisadi wa ndani ya Serikali walitaka iwe ili kupata mgao wao wa mabilioni. Tusubiri tuone kizungumkuti hiki kitamalizika vipi.
   
 5. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,108
  Likes Received: 7,366
  Trophy Points: 280
  Hii inaweza kua mojawapo ya Movie zenye Series nyingi Na ndefu zaidi duniani.
  Kwa kukadiria tu inaweza kushindana Na Isidingo au Egoli
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Atatumia njia zote ila kukifikia icho kiti cha enzi ndo kutakuwa kuna kazi na tukiangalia mwamko wa waTz kwa sasa hasa vijana kazi mbona atakuwa nayo
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Iwe ndefu lakini mwisho wake kieleweka na kuwaumbua hao mafisadi
   
 8. fikrapevu sungura

  fikrapevu sungura Senior Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Source: Mwananchi

  MVUTANO mkali baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya Dowans, kuhusu hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoamuru Tanesco iilipe Dowans zaidi ya Sh 94 bilioni, bado unaendelea.

  Mvutano huo unafautia hatua ya Tanesco kutafuta njia za kisheria baada ya kuomba kibali cha kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga hukumu na kuepukana na malipo hayo, lakini Dowans nayo ikaendelea kuibana kwa kuiwekea pingamizi ili inyimwe kibali hicho.

  Septemba 28 mwaka jana, Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, aliamua tuzo ya Dowans iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), isajiliwe ili kuwa hukumu halali ya mahakama hiyo.

  Kwa uamuzi huo, Tanesco sasa inatakiwa iilipe Dowans Sh 111 bilioni badala ya Sh 94 bilioni za awali.

  Tanesco inapaswa kulipa fidia hiyo pamoja na riba ya asilimia 7.5.

  Hata hivyo shirika hilo la umeme limeeleea kutokuridhishwa na hukumu hiyo na hivyo kutoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

  Maombi ya kutaka kibali cha kukata rufaa hiyo, yalitarajiwa kuanza kusikilizwa jana na Jaji Dk. Fauz Twaib lakini mahakama ilishindwa kuyasikiliza baada ya Dowans kuweka pingamizi, ikiomba mahakama isiipe Tanesco kibali.

  Dowans iliiwekea Tanesco pingamizi hilo mwezi huu ikidai kuwa kwa mujibu wa mkataba baina ya pande hizo, hukumu ya ICC haiwezi kukatiwa rufaa.

  Ni hoja kama hizo ilizozitoa Dowansa wakati wa pingamizi la Tanesco kutaka Mahakama Kuu isiisajili tuzo yake na baadaye Jaji Mushi alikubaliana na hoja za Dowans na kuamuru tuzo hiyo isajiliwe.

  Jana Jaji Dk Twaib aliziambia pande hizo mbili kuwa mahakama haitaweza kusikiliza maombi ya Tanesco kuhusu kibali cha kukata rufaa hadi hapo pingamizi la Dowans litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

  Jaji huyo, alizitaka pande hizo, kuwasilisha hoja zao kwa njia ya maandishi na kwamba pingamizi hilo litaamuliwa Februari 16 mwaka huu, baada ya kupitia hoja zote.

  Ikiwa mahakama itatupilia mbali pingamizi la Dowans, basi Tanesco itapewa kibali cha kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

  Lakini kama mahakama itakubaliana na pingamizi la Dowans basi harakati za Tanesco kujinusuru katika malipo hayo kwa njia za kisheria zitakuwa mashakani.

  Hukumu ya Jaji Mushi ilionekana dhahiri kwenda sambamba na kile alichowahi kukisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema kuwa hakuna uwezekano wowote wa kisheria kuepuka malipo hayo.

  Wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama alisema hadi wakati hukumu hiyo inatoka, Tanesco ilipaswa kuilipa Dowans kiasi cha Sh 111bilioni badala ya Sh94 bilioni.

  "Fidia ya awali katika uamuzi wa ICC ilikuwa ni Dola za Marekani 65milioni, lakini kwa sasa ukiweka na riba ya asilimia 7.5 fidia hiyo imeongezeka hadi takribani Dola za Marekani 72milioni ambazo ni kama Sh111bilioni," alisema Fungamtama.

  Katika hukumu yake Jaji Mushi alisema baada ya kupitia mwenendo na hoja za pande zote nimebaini kwamba si sawa kwa mahakama hiyo kuingilia uamuzi wa ICC.

  "Hivyo ninaagiza kuwa tuzo hiyo isajiliwe na iwe huku halali ya mahakama hii," alisema Jaji Emiliani Mushi ambaye kabla ya kusoma hukumu hiyo alisema kuwa anatambua kuwa suala hilo limekuwa na msukumo mkubwa wa kisiasa lakini akabainisha kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa sheria.
   
 9. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Richmond=dowans=symbion!
   
 10. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,108
  Likes Received: 7,366
  Trophy Points: 280
  =RosAz
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  ..Sijui kama anasafishika huyu amechafuka kupita kiasi....kuzilipa labda azitoe mfukoni mwake maana TANESCO kwa sasa hawana ubavu wa kuzilipa.
   
 12. l

  luckman JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160

  ngeleja, pinda na mwanasheria wanalipa kwa pesa za nani? hapa tunajua pesa za nani na anataka kufanya nini! mungu yu pamoja nasi!wala msiwe na shida, tulieni muone jasho la walalahoi linavyochafua hali ya hewa hapa mjini!
   
 13. koo

  koo JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Siwezi kuamini kama 2015 lowasa atakosa urais natamani mungu amjalie afya njema anilinde namimi nishuhudie kama kweri atakosa manake sijaona uwezekano wa mtu aliyejiandaa kugombea kwa miaka 20 yaani tangu 1995 mpaka 2015 tena maandalizi ya umakini na kina eti ashindwe? mhhh ngoja nivute subira
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kesi ya TANESCO, DOWANS imeamuliwaje leo?
   
Loading...