Kizimbani kwa kughushi benki na kuiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizimbani kwa kughushi benki na kuiba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 26, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,451
  Likes Received: 22,383
  Trophy Points: 280
  MKAZI wa Sinza Abdul Adam (25), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kughushi cheki ya benki na kuiba.

  Mshitakiwa amesomewa mashitaka yake na Mwendesha mashitaka Wakili wa Serikali Credo Lugaju.

  Mbele ya Hakimu Pamela Kalala imedaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo, Januari 16, mwaka huu, katika kituo cha mafuta cha Euro Petrol Lubs ltd.

  Imedai kuwa mshitakiwa alighushi cheki namba 00132 ya benki ya Standard Charter ya sh mil 10 na kuiwakilisha kwa mfanyakazi wa kituo hicho Bupendra Motichand.

  Wakili Credo aliendelea kudai kuwa mara baada ya kuiwakilisha cheki hiyo, mshitakiwa alijipatia madumu 10 ya mafuta kilamoja likiwa na lita 20 mengine 20 kila moja likiwa na lita 10 mali ya euro petrol lub ltd.

  Mshitakiwa amekana mashitaka dhidi yake na amerudishwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana hadi kesi itakapotajwa tena Februali 3 mwaka huu.

  Katikia kesi nyingine mkazi wa Keko Dickson Anael (42), amefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kufoji kitambulisho cha kazi.

  Mbele ya Hakimu Agnes Mchome imedaiwa Mwendesha mashitaka Asma Shemweta kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 8 mwaka huu katika maeneo ya mahakama ya Wilaya ya Ilala.

  Inspekta Shemweta aliendelea kudai kuwa mshitakiwa alifoji kitambulisho namba 15 na barua yenye namba KMC/VOL/ 1/8/10 ya tarehe 13 Januari mwaka huu ambayo ilionyesha kuwa imetolewa na Meneja wa soko la kariakoo na kuwasilisha kwa Mwendesha mashitaka Musa Gumbo.

  Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na kesi itatajwa tena Februari 3, mwaka huu.

  SORCE; DAR LEO
   
Loading...