Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,639
- 729,585
Lakini iko hivi wewe ni muunganiko wa roho mbili tofauti kupitia manii ya baba na yai lililopevuka la mama vilivyokutana na kuunda/kuumba roho moja (wewe) kwahiyo wewe ni muunganiko wa roho mbili +moja
Hii ina maana gani? Ni kwamba kwenye ulimwengu wa roho una connection ya moja kwa moja na hao watu wawili waitwao wazazi na kadiri unavyoendelea kukua hufyonza nguvu yao na kujenga nguvu yako....hata kama wawe ni wafu tayari huo mchakato huendelea kwakuwa hili ni jambo la kiroho na si la kimwili
Kwa sisi tunaoamini katika Mungu mmoja mzazi huitwa Mungu wa pili, hivyo mzazi ana nguvu kubwa sana na madhara ya moja kwa moja(direct effect) kwako kwa lolote lile liwe baya au zuri
Mwaka jana mwanzoni tulikuwa na mada inayohusu laana na kama je kuna connection gani kati ya mzazi anayetoa laana na mtoto anayelaaniwa
Usiku huu na kesho pia ukiwa na bundle la kutosha kuingia JF nk huku ukiwa umeshiba wewe na familia yako....!Je umemkumbuka mzazi pale kijijini je kashiba kama ulivyoshiba wewe? Kumbuka yeye ni sehemu ya wewe na bila yeye wewe usingekuwepo hapa! Wewe unayejiita mimi...!
Ulalapo muda huu na utakapoamka kesho usisahau kusahau kuhusu hili