Kizaizai nilivyoiokoa timu ya kijiji!

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,223
56,877
Asalaam aleikyum waungwana..?
Natumai mu wazima na Buheri wa afya zenu mnazozitumia kumtukuza muumba na wengine mnazitumia kutenda maovu!.. yote kwa yote kikubwa tunaishi.

Turudi kwenye kizaizai chetu,kisa hichi ni kabla sijawa kijana wa hovyo ambae nakunywa mpaka natumbukia kwenye kisima cha nzengo!..
Miaka kadhaa hapo nyuma vijiji kadhaa viliandaa ligi ya mpira wa miguu vikishindania ng'ombe na fedha taslimu isiyopungua laki tano.. kijiji chetu nacho kiliamua kushiriki,tukateuliwa vijana wenye hali,nguvu na uchu wa kulisakata kabumbu na moja ya kitu ambacho tulibahatika tulipata mfadhiri hivyo vitu kama jezi na viatu havikutupa tabu!.

Timu iliandaliwa vyema chini ya kocha wetu sitomtaja jina!,kwa ufupi ligi ilikuwa imekamiwa na timu zote za kila kijiji!..
Timu yetu ilifuzu mpaka fainali japo kwa mbinde huku mimi mwenyewe nikiwa kiungo mkabaji na mshambuliaji wa kushitukiza!.

Kwenye hii fainali ndipo vizaizai vyenyewe vilipoanzia!.. picha linaanza siku moja kabla ya fainali yenyewe wachezaji tunachukuliwa usiku wa saa sita tunapelekwa kijiji chengine kwenda kukutana na mtaalum wa maswala ya uchawi,mtu alietapikwa na nyongo ya uganga,mizimu na majini yote yamelala kwake!.. hii yote ni katika kuhakikisha tunapata ushindi!.

Ilikuwa usiku tulivu,usiku ambao mbalamwezi ilitandaza nuru hafifu katika kijimsitu cha kijiji hichi,kwa takribani lisaa limoja tulifika kwa mganga husika tukiongozwa na mmoja wa wazee toka kijiji chetu. Tulipokelewa vyema na kukaribishwa kwenye kichumba cha majani ambacho hakitutosha watu wote wengine ilibidi wakae nje ila binafsi nilipata bahati ya kuingia kwenye chumba kile ambapo kwa idadi tulikuwa kama watu Saba ukitoa mganga na msaidizi wake.

Mzee wetu akaeleza shida iliyotupeleka pale,baada ya kueleza tukaombwa tutoe fedha shilingi elfu hamsini tukaweka kwenye kiungo kidogo ambacho kilikuwa mbele ya mganga mkabala na kibatari kilichokuwa kikiwaka na kutupatia mwanga.
mganga akaanza machachali yake ya kuiita mizimu yake,lakini kabla hajafanya hivyo tulipewa tahadhari kuwa anamoja ya zimwi ambalo ni korofi hivyo ikitokea likapanda chochote chaweza kutokea!.. taarifa hiyo ilimuweka kila mtu mguu ndani mguu nje!..

Mganga akaanza kushika tungule zake mara aimbe mara aache,macho yangu yaliamua ku focus na vitu vitatu mganga,fedha iliyokuwa kwenye ungo na msaidizi wa mganga.. punde munkali wa mganga ukawa unapanda kila mmoja kitete mule ndani kikampanda lkn tukawa tunajikaza kisabuni si tunataka ushindi bhana!..
Sasa munkali wa mganga mi ukaanza kunitia kiwewe maana alikuwa anapumua kwa spidi kiasi kwamba kile kibatari kilikuwa kinazima muda wowote! Nilipofikiria taarifa tuliyopewa halafu litokee lakutokea na kibatari kiwe kimezima si tutauana humu!. Uvumilivu uliponishinda nikaamua nikisogeze kibatari pembeni kisije kuzima watu tukashindwa kuona hata mlango wa kutokea!.. wakati nashika kile kibatari watu wote walinitumbulia macho lkn kwa nilivyowaona wengi wao walishukuru maana hata wao walitamani wafanye hivyo lkn tulitofautiana ujasiri!..

Mganga akazidi kucharuka alipokuwa amekaa akaanza kurukaruka ile namcheki msaidizi wake kama vile uoga ulizidi kumtanda akawa hana amani!,akawa hatulii punde si punde msaidizi wa mganga kwa spidi ya ajabu akarukia mlangoni!,sasa tukaona lile dhoruba tulilokuwa tumelirejea ndo limefika! Mganga hakamatiki anapiga ukelele kana kwamba anataka kutoka na roho ya mtu!.. ile tiba tuliyokuwa tumeifata ili kushinda ikageuka kuwa mwiba kwetu!,chumba kile tulichoingia kwa utulivu sasa tuligombania kutoka kwa spidi kila mtu akitaka kuinusuru nafsi yake dhidi ya mganga alietubadirikia!

Tafrani za kila mtu kuwania mlango zilikuwa sio za kifani! Katika hatua yangu ya kwanza tu niliangushwa kwa pushi nami nikaanguka karibu na mganga ambae alikuwa kachafukwa haswa!,ule mzimu wake korofi ulikuwa umemfika pasipofikika!.. hapo ndipo nilipoona kiama hichi hapa! Kwa nusu sekunde kabla ya kunyanyuka nilipoanguka nilijikuta najilaumu mara elfu hamsini na kenda kwa mimi kuingia kwenye chumba kile!,haikutosha nilikuta najiuliza hivi huu ndio mpira..??!
Sasa wakati nanyanyuka nikapata kuona zile fedha zetu zilizokuwa kwenye kale kaungo!,kitu nachoshangaa sijui nilitoa wapi akili ya ujasiri ya kubeba zile fedha!.
Mara hii niliponyanyuka nilinyanyuka na ujasiri wote sikuwa na subira kitu nilichokuwa nimesahau ni kuwa nilijiona nimewahi kumbe nilikuwa nimechelewa!.
Ile nanyanyua hatua kuuwania mlango nashangaa mguu mmoja hauendi! Nikaongeza nguvu lakini wapi! Kumbe mganga alikuwa ameshaniwahi mguu wangu! Nikaona usinitanie wewe nilimpiga teke mkono wake uliokuwa umenishika!,naona mzimu ulipata pigo ukaamua uniachie!.. hiyo ndio fursa ambayo niliitumia vilivyo maana ktk namna nilivyopenyeza kwenye ule mlango nafikiri hata mzimu wa mganga ulishangazwa.

Chakushangaza ile natoka nje kwa spidi kali sikukuta mtu! Maana yake ni kwamba mimi ndio nilikuwa wa mwisho!,nikaona hapa nikicheza napotezwa kwenye uso wa dunia maana ukitarajia huko ndani nimeshafanya makosa mawili kwanza nimechukua fedha ya mzimu pili nimempiga teke mzimu!!!..
mzimu nae hakukubali yaishe hivihivi! Hakupenda kupokwa fedha na pia alitaka kulipiza teke alilopigwa!..
Akiwa amechafukwa zaidi huku akipiga makelele mganga aliniundia mkia kwa spidi ambayo vishindo vyake vilisikika kwa kutisha!..
Kenzy wa watu nilitamani kupiga kelele lkn koo liligoma nafsi,moyo na roho yangu nikaielekeza kwenye mbio tu ndio dhana niliyokuwa nimebakiza!,kucheki nyuma Kaniki nyeusi ya mganga aliyokuwa amevaa kiunoni ilikuwa ikipepea mithiri ya parachuti la komandoo John! Chakuogofya zaidi ni zile kelele zake za kuunguruma alizozitoa bila tuo la kupumzika mpaka nilihisi huyu kiumbe anamapafu ya mbwa mwitu!.

niliwaza au nitupe hizi hela huyu mzimu aniachie! Lkn wazo hili nililipinga ghafla nilipoona naanza kumzidi mbio! Kumbe nisichokijua alikuwa akinivutia spidi punde mganga akaacha kupiga kelele naona sasa Aliamua hili jambo alimalize kimyakimya!,sasa hapo ndipo nilishuhudia spidi halisi ya mganga yule kwani kila nikiongeza spidi vishindo vyake ndio vilizidi kunisogelea!. Dakika mbili mbele akawa nyuma yangu akiwa kabakiza tambo mbili tu anidabe!. Nilitamani ardhi ipasuke nitumbukie maana aliniweka kwenye hatihati sikujua kama bado nakimbizwa na mzimu au mganga mwenye utimamu wake!.

Nikiwa katika hatari hiyo ghafla hatari nyengine ikajitokeza mbele yetu!.. kwa spidi ya hatari mbele yetu niliona fisi wawili wakikatiza wakiwa kama wanafukuzana!,hata mkimbizi mwenzangu aliliona hilo tukio nilichosikia nilimsikia akiguna tu nakupiga breki kali inaitwa breki ya Kenge! Nami vivyohivyo bila hiana na bila hisani ktk namna hiyohiyo nilitandika breki inaitwa propera!.. kilichofuata ilikuwa ni kukanyaga anapokanyaga mganga tuliona tuache utani sasa tuokoe nafsi zetu!..
Nilipoona nakaribia kwa mganga na wale fisi hawatufati niliuma kona yangu asijue nimekwenda kona ipi!.

Kesho yake wanatimu tukakutana kijijini kwetu nakuwasimulia mambo yalivyokwenda,siku ya fainali ilipowadia wale wapinzani wetu walikuwa wamejidhatiti ktk mbinu zote kipindi cha kwanza tu tukachezeshwa mbili!,kipindi cha pili tukarudisha zote dakika za mwishoni mshambuliaji wa kushitukiza nikafunga bao la ushindi! Hivyo tulibeba ng'ombe na pesa pasipo dhana yoyote ya kishirikina!.
 
Mambo ya chandimu hayo,usiombe muende kwa mganga mmoja patachimbika
 
Dah...nimecheka...paragrafu za mwisho ungetupia video 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
😂 ukianza kusoma nyuzi ulizoandika unaweza ukajihisi sio wewe!
 
Back
Top Bottom