[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Kuna siku nlikwama na gari porini ilikuwa mida ya saa9 usiku
***** nikaanza kusikia sauti ya roli aina ya scania linakuja
Nikiangalia nyuma ama mbele taa za hilo gari sizioni lkn mlio unazidi kusikika tu
Nliingia ndani ya gari langu nikapiga loki milango
Siku hio ndio nlipata jibu ya Kwanini chips hainaga ukoko[emoji1321]
Baadhi ya mawazo/picha za gizani huwa fursa. Hili ni somo refu imagination, Idealism and realismUlishawahi kutembea kizani kwenye giza totoro? Ulishawahi kulala chumba chenye giza mwanzo mwisho? Ulishawahi kuona yale maumbo ya watu na viumbe vya ajabu?
Unatembea kwenye barabara yenye miti vichaka na majani unaona mbele yako au pembeni kuna vitu kama watu au wanyama tena vinatikisika au kutembea au kuongea kwa sauti ya chini
Au unahisi kabisa nyuma yako kuna mtu anakuja anakufuata unatamani ugeuke uangalie au utimue mbio[emoji23] [emoji23] [emoji23] nywele zinasimama kabisa moyo unaenda mbio mambo yanakuwa magumu kweli
Kuna story za vibwengo na vinyamkera vingi hujitokeza kwenye maeneo kama haya lakini si mara zote kila kitu ni hivyo viumbe
Waganga makanjanja wajanja sana hutumia giza na makaburini na sehemu zenye miti na misitu au vichaka kukupiga anakuandalia mazingira kabisa ya wewe kuwaona hao viumbe
Kinachofanyika na ubongo wako mwenyewe kupitia macho yako....unawaza kuhisi na kuhusu vitu vya ajabu kizani kisha unatengeneza picha zake automatically majani yakicheza tu kidogo ile sura na umbo ulivyoviumba akilini vitakujia live...hapa ndio ishu ya vinyamkera na vibwengo hujitokeza, akili yako ndio inakuchezea michezo kulingana na mawazo yako
Fanya jaribio hili usiku wa leo zima taa zote mpaka ile ya nje inayoingiza mwanga kupitia dirishani kisha anza kuwaza kuhusu vibwengo mashetani majini vinyamkera na mizimu nk ...wallah nakuambia utaviona live....
Makaburini kuna story nyingi sana za namna huyo lakini nyingi hazina ukweli na hata hao marehemu tunawasingizia tu
Maisha ni safari ndefu hujui ni lini na wapi unaweza kukutana na hili usibabaike wala kubabaishwa...matukio mengi ya namna hii ni own mind creations...
Ahsante sana mkuu Mshana JR umenifumbua kwa kiaisi fulani japo mada ni ya muda mrefu!
Mzee baba,una mambo mengi
Benny tafuta siku nikuchukue ziara tukatembee pahala usiku ni nje ya mji lakini
[emoji3] [emoji3] [emoji3]Hahahaha! Mkuu umenikumbusha mbali sana. Iliwahi kutokea nikiwa nasoma Advance. Kuna Jamaa alisimamishwa shule kwa makosa ya kinidhamu. Sasa watu wakawa wanatania kuwa kuna mzimu wake kila siku unazurura hapo shuleni. Sasa siku moja tumetokea darasani usiku kupiga msuli,tumekaa mahali tunajipumzisha huku tunasikiliza redio. Bahati mbaya nikapitiwa na usingizi.
Niliokuwa nimekaa nao wakaenda kutafuta shuka leupe pee,wakaja kunifunika kisha wakawajulisha watu kuwa Leo waje wakamshuhudie mzimu wa Jamaa. Sasa wamejikusanya wakaja wengi,wakaanza kujiuliza eti siyo mzimu. Ile wamesema twendeni tukamfumue,mm nikakurupuka kwa wenge la ajabu .......hahahaha! Watu wote walikimbia mpaka wale waliokuwa wamecheza mchezo. Na mm nilipoona wanakimbia,nikawafata mbio nikijua kuna noma. Bado shuka limenishikilia tu. Shule nzima walitoka mbio wanakimbia. Majamaa na wenyewe hawakuwa na uwezo tena wa kujitutumua. Watu tulicheka Sana siku hyo.