Habari wana jamvi, kwa muda nimekuwa nikisikia kuna uwanja wa kimataifa uitwao Chato International Airport. Binafsi siujui, lakini sijawahi kuona uzinduzi wake, vilevile sijaona hata kwa vyombo vya habari kuhusu ndege zinazotua kwenye huo uwanja.
Mwenye takwimu anijuze huu uwanja ukoje na kwa siku unapokea wastani wa ndege ngapi. Lakini nilitaka kujua kama tayari Bombadier za ATCL zinatua kwenye uwanja huo