Kiwanja au Biashara


Nunua Kiwanja, ila usijegenge; Kama Bado utakuwa na passion ya biashara, unaweza kiuza baadae kwa faida ukafikiq malengo
 
Hela iliyopo inaweza tosha kiwanja.
Ningependa kupokea ushauri kwa mtu aliyewahi pitia hii hali au kwa yeyote mwenye mawazo ya kujenga anisaidie kunipa uelekeo utakaofaa. Ahsanteni na karibuni
Kama kipato chako ni cha uhakika, hiyo hela uliyo nayo ifanye mtaji wa kuanzia. Anza biashara mdogo mdogo. Ukiona mwenendo wa biashara unaridhisha, tafuta Microfinance nenda ukope kiasi cha kujazilizia huo mtaji wako. Endelea na biashara huku unalipa mkopo na ukipata hela za ziada pia zitumie kulipa mkopo ili umalize mapema. Ukimaliza kulipa unakopa tena unapanua biashara
 
Nakupa mfano mmoja:-
Benki iliamua kuwapa mkopo bwana A, na bwana B; kila mmoja kiasi cha milioni 5, na kila mmoja alitakiwa kuzirejesha pesa hizo baada ya miaka 2.​
  • Bwana A aliamua kuwekeza pesa zile kwenye biashara yake ya uuzaji wa bia na soda; kwa sababu bidhaa alizokuwa auza si za kuharibika, aliweza kuziuza na kupata faida.​
  • Bwana B aliamua kuchukua pesa ile na kununua kiwanja, bila kufanya uzalishaji wowote.​
Muda wa marejesho ulipofika, bwana A aliweza kurudisha na kubaki na faida, ila bwana B hakuwa na pesa ya kurudisha zaidi ya kile kiwanja; kutokana na kutakiwa kurudisha lile deni kwa haraka, ilibidi bwana B auze kile kiwanja kwa bei ya hasara ili aweze kurejesha mkopo.

Swali; Je, Bwana A na Bwana B ni nani aliyetumia akili zaidi?​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ