Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,060
Vitabu vyote vya dini vinatamka wazi kabisa kuwa anayetakiwa kuabudiwa, kutukuzwa na kusifiwa ni Mungu pekee yake. Biblia inaongeza kwa kusema, amelainiwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, na kumfanya mwanadamu kuwa kinga yake.
Nimerejea maandiko ya vitabu vya dini kwa sababu ndiko huko mifumo ya tawala zote ilirithiwa.
Kwa sasa bila shaka, nchi yetu imelaanika maana viongozi wote hakuna wanalolijua zaidi ya kumsifu na kumtukuza Rais, tena kwa kiwango kinachokaribia kumwabudu.
Anayewezesha yote kufanyika, kwa watu wanaomwamini Mungu, ni Mungu pekee yake. Sisi wanadamu, bila ya kujali vyeo vyetu, utajiri wetu, maarifa yetu, akili zetu na nguvu zetu, bado tumejawa na mapungufu mengi.
Leo tuna watu wanaonena na kutaka kuwaaminisha watu wote kuwa kila linalofanyika nchini mwetu limewezeshwa na Rais. Wameifuta nafasi ya Mungu, na kumkweza Rais. Na yeye, kwa kutolikemea hili, maana yake amekubali, na kama amekubali kuwa yeye ndiye mwezeshaji wa kila kitu, basi ina maana anajifananisha na Mungu. Na kama ndivyo, basi shauri yake.
Mimi siwezi kusema nini kitatokea au ni nini adhabu ya mtu kujifananisha na Mungu, kwa sababu mimi sina nafasi hata ile ndogo kabisa ya kumsemea Mungu. Mimi napaza sauti tu kwa wanadamu wenzangu ili waijue kufuru wanayoifanya, na adhabu wanayojitengenezea kwa nafsi zao na kwa yule waliyeamua kumtukuza.
Leo hii, ikijengwa barabara, ni Rais kajenga.
Maji yakitoka bombani, Rais kaleta maji.
Simba au Yanga ikishinda, Rais katuletea ushindi.
Kukiwa na umeme, Rais katuletea umeme.
Kukiwa na chakula cha kutosha, Rais katuletea chakula.
Leo hii kwa Tanzania, hakuna kinachowezeshwa na Mungu, bali ni Rais tu.
Wale walioamua kumpa rushwa ya utukufu na suia Rais, wanawaaminishwa watu wote kuwa Leo hii kwa Tanzania hakuna kinachofanywa na wananchi zaidi ya milioni 63, isipokuwa Rais pekee yake ndiye anafanya kila kitu. Rais ndiye anayejenga miradi yote. Rais ndiye mwenye akili kuliko Watanzania wote. Rais ndiye mwenye upendo kuzidi Watanzania wote. Na Rais ndiye anayependwa zaidi kuliko Mtanzania yeyote.
Rushwa ya sifa na utukufu ni rushwa sawa na rushwa nyingine, yenye malengo yale yale. Rushwa ya sifa na utukufu humpofusha mtawala sawa na rushwa ya pesa inavyompofusha mtumishi wa Serikali asiye na pesa.
Watanzania mliobakiwa na hekima, jitengene na laana za kuwatukuza wanadamu.
Mwalimu Nyerere hekima ilimwongoza hata aliweza kuishinda rushwa ya sifa:
1) Watu waliamua kumwita Musa, Mwalimu Nyerere aligomba na kukemea kabisa.
2) Alipotaka kung'atuka, watu walienda kwake na sifa kedekede, na kumwambia Mwalimu, 'nchi hii itaendaje bila wewe'. Mwalimu akang'aka na kuuliza, kama yeye ataishi milele; na kama siku akifa na nchi itakufa. Baadaye mwalimu alisema kuwa baada ya kufanya utafiti wake aligundua kuwa "nchi" wanayoiongelea ni familia zao. Hawakuwa na uhakika akitoka yeye, akaja Rais mwingine, kama wangeendelea kuwa kwenye nafasi alizokuwa amewaweka.
Kusema kuwa kila kitu kinafanywa na Rais, ni kuwadharau, kuwatusi na kuwakatisha tamaa Watanzania wanaoteseka usiku na mchana kuleta ustawi katika Taifa lao. Ni sawa na kuwaambia Watanzania wote kuwa hayo wanayoyafanya hayana maana yoyote wala hayana mchango wowote kwenye ustawi wa Taifa lao, maana mtu pekee anayefanya kazi katika nchi hii na kuistawisha ni Rais pekee yake.
Yatafakarini haya kwa hekima badala ya sifa, ubishi na ushindani.