Kiwanda Cha Vifaa Vya Michezo nchini kinahitajika sana

Kiwanda Cha Vifaa Vya Michezo nchini kinahitajika sana

astranaut

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
1,276
Reaction score
1,024
Serikali ione umuhimu wa kushawishi wawekezaji katika sekta ya viwanda kuja kuwekeza kwenye viwanda vya kuchakata vifaa vya michezo.Nilikua naangalia Azam Sports HD 2 saa 2 ambayo imerusha Kaitaba Football Club Academy,watoto na wakufunzi kwa ujumla wanalia na uhaba wa vifaa vya michezo ikiwa ni pamoja na mipira michache ambapo ata hiyo michache iliyopo imeisha,wenzetu nchi zlizoendelea unakuta uwanja wa mazoezi(football training ground) una kila kitu mipira ya kutosha,vifaa mbali mbali vya mazoezi, jezi za kutosha na hayo yote hayachangiwi tu na kwamba wao ni matajili wanapesa nyingi bali upatikanaji wa vifaa vyenyewe ni wa bei ya chini kutokana viwanda vipo.Mimi sio mtalaam sana wa kupangilia mawazo lakini naimani lengo lanulitaeleweka na kuwafikia wadau.
 
Back
Top Bottom