Kiwanda cha Twiga Cement chafungwa kwa muda usiojulikana

Kiwanda cha Twiga Cement chafungwa kwa muda usiojulikana

lukindo

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2010
Posts
8,467
Reaction score
9,053
Kiwanda cha saruji cha Twiga Cement cha jijini Dar es Salaam, kimepigwa marufuku kuzalisha sementi kutokana na kusambaza vumbi la linalohatarisha afya za watu na kuchafua mazingira.


Amri ya kukifungia kiwanda hicho kwa muda usiojulikana ilitolewa jana na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kukiagiza kulipa faini ya Shilingi milioni 50 kwa kuvunja sheria.

‘Twiga Cement’ kwa mujibu wa NEMC inachafua mazingira na imeshindwa kudhibiti vumbi linalotokana na uzalishaji wa sementi linalopitia kwenye bomba lililoelekezwa angani.

Kiwanda hicho cha Twiga Cement ambacho kipo eneo la Wazo Hill nje kidogo ya Dar es Salaam kinahusishwa na kutodhibiti vumbi linalosaabisha watu kupata maradhi.
Kiwanda hicho kiliamriwa kulipa mara moja faini ya Shilingi milioni 50 kwa kuvunja kifungu namba 191 cha sheria ya mazingira ya mwaka 2004.

Kifungu hicho kinasema yeyote ambaye atachafua mazingira kwa namna yoyote atachukuliwa hatua ikiwemo kufungiwa kiwanda pamoja na kulipa faini.

Akizungumza na wanahabari wakati akikifungia kiwanda hicho, Mwanasheria wa NEMC, Heche Suguta alisema wamepokea malalamiko mengi kutoka kwa wakazi ambao wanakizunguka kiwanda hicho pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo wakilalamikia vumbi hilo kuathiri afya.

Alisema baraza lilijulishwa kuwa uchafuzi unaofanywa na kiwanda hicho umesababisha watoto kupata mafua yasiyoisha, kukohoa, kuumwa vichwa na Kifua Kikuu (TB).

Walilalamikia wakati mwingine kushindwa kulala.

Heche alisema vumbi hilo ambalo ni la saruji limesababisha matatizo mengi kwa wananchi na kwamba hawapo tayari kuona watu wakiendelea kupata shida.
“Tumeamua kukifungia kiwanda hiki kikubwa cha Cement cha Tanzania ili iwe fundisho kwa viwanda vingine ambavyo vina tabia ya kukaidi maagizo ya serikali,” alisema Aliwaambia wanahabari kuwa endapo kiwanda hicho kitakiuka agizo hilo polisi na NEMC watamkamata Mkurugenzi wake na utaratibu mwingine wa kisheria utaendelea.

Alieleza kuwa kabla ya kukifungia kiwanda hicho jana walituma wataalamu kwenda kuchunguza suala hilo ili kubaini hali ya wanaathirika.
Wataalamu hao walithibitisha kuwa kiwanda hicho kinatoa vumbi lenye athari kiafya na hatua ya kukifungia ilichukuliwa.

Awali Mkurugenzi wa Twiga Cement , Alfonso Rodriguez, alisema bomba ya kupitishia vumbi la saruji la kiwanda kipya limeharibika, hatua iliyowalazimisha kutumia la kiwanda cha zamani ambalo limeelekezwa angani.



Alisema kiwanda hicho kinafanya marekebisho ya kasoro hiyo.


Nipashe

My take:
Hivi kiwanda hiki ndicho 'kimevamia' makazi ya watu au watu wamevamia eneo la kiwanda!?
Najaribu kuangalia hiki kiwanda kilijengwa mbali kabisa na mji lakini kutokana na ukuaji wa miji usiofuata mipangilio wananchi kwa kutumia udhaifu wa mamlaka za utawala tumevamia eneo jirani na kiwanda.

Nawasilisha.

 
Your take: Unahisi vumbi linalotoka pale linaishia maeneo jirani na kiwanda peke yake? Unadhani kiwanda kinashindwa kudhibiti hilo vumbi lisitoke?

Jamaa wana kiburi sana, wafungiwe tu.
 
Tuna tatizo kubwa hapa nchini katika masuala ya mipango miji, kama hali itaendelea hivi kuna hatari ya viwanda vingi kukumbwa na mkono wa sheria. Kiwanda kilipojengwa kikiwa cha uma kilikuwa mbali kabisa na makazi ya watu, vumbi litokanalo na uzalishaji lilikuwa halifiki kabisa katika makazi ya watu. Leo hii tumepeana viwanja mpaka tumegusa mipaka ya kiwanda halafu tunalalamikia vumbi. Tatizo kama hilo lipo pia kiwanda cha tumbaku Morogoro TTPL. Kiwanda kinafanya kazi tangu miaka ya 1968 na kilikuwa nje kabisa ya mji wa Morogoro, leo hii watu tumegawana viwanja na kujenga makazi mpaka kwenye fence ya kiwanda halafu tunalalamikia harufu ya ugoro na vumbi la tumbaku. Huu ni ujinga wa mipango miji. Sehemu nyingi makazi yamefuata viwanda. Tufike mahali tujiulize kwa nini makazi yanafuata viwanda tena kwa baraka za halmashauri husika na kisha tunalalamika? Vinginevyo halmashauri husika zibebe mzigo wake.
 
Your take: Unahisi vumbi linalotoka pale linaishia maeneo jirani na kiwanda peke yake? Unadhani kiwanda kinashindwa kudhibiti hilo vumbi lisitoke?

Jamaa wana kiburi sana, wafungiwe tu.
Nimetafakari sana juu ya hilo pia lakini kama unafuatilia tangia zamani kulikuwa hakuna mfumo wa kuzuia vumbi, lote pamoja na moshi vilikuwa vikienda angani.
Kwa maana hiyo athari zilikuwa zaidi kwenye global warming na sio kwa wakazi wa jirani kwa maana hakukuwa na majirani wa kiwanda. Sasa nawaza athari za kukifunga kiwanda hiki kwenye bei ya cement au ikiwezekana basi 'kihamishwe' ili kuwapa amani wakazi wa eneo hilo.
Swali la msingi ni kama viwanda vingine navyo vinatimiza masharti ya kimazingira kama wote tunavyojua.
 
Halafu hiyo ni porojo tuu,wamefunga mtambo mmoja tuu KILN 3 lakini uzalishaji kwa kutumia mitambo mingine unaendelea,pia mauzo kama kawaida yanaendelea.Hilo ni changa la machoo tuu wakuu
 

Swali la msingi ni kama viwanda vingine navyo vinatimiza masharti ya kimazingira kama wote tunavyojua.

Ndugu,

Siku ukikamatwa na PCCB kwa kupokea rushwa tena ya Tzs 100,000 tu kamwe utetezi wako usiwe mbona kuna ESCROW na sandalusi za mabilioni huko na wahusika hamuwashiki? Utaishia jela.

NEMC ni watchdog wa usalama wa mazingira kwa ujumla wake. Bado kiwanda kingeweza kufungiwa kwa kutishia uhai wa viumbe hai wengine, kuchafua vyanzo vya maji, kuharibu misitu na hata miundombinu. Kwa hiyo hata kama Kiwanda still kingekuwa mazingira yaleyale ya 1960`s lakini kinaelekeza uchafu katika mazingira bado sheria za NEMC zingekibana.

Kwangu mimi mjadala wa muhimu ni athari za kiuchumi kwa kukifunga hicho kiwanda lakini si kwa kiwanda kukiuka sheria za mazingira.
 
Inawezekana kudhibiti vumbi hilo kwa kuwekeza katika vifaa vya kufanya hivyo. Hivyo kampuni inatakiwa kuwekeza kwenye hilo.
 
wasiishie hapo wazo waende na vikindu mkuranga kuna Rhino cement. hiki ni kipya na kiko mtaani kabisa. hatariii
 
Mbona kile cha Morogoro kilichotajwa kuwatia kansa ya polepole wakazi wa Dar na Pwani wanakiogopa kulikoni?!!
 
A good move but too late.

Hiki kiwanda cha Wameliki wa Norway ni jangala mazingira. They have been polluting they envionment for
a long time something which they cant do in Norway.

Children in the neighbourhood have been suffering from acute respiratory diseases while homes have been rendered inhabitable. They are also releasing storm water every year causing flooding in Boko area .Shame on you Dirty investors. This is not possible anywhere in Europe.


Wameleta adha kubwa kwa afya za watu na mazingira. Watu wamejenga nyumba za maana lakini hazikaliki. Pia humwaga maji ya mvua na kusababsha mafuriko eneo la Boko kila mwaka.

Kuna waziri mmoja aanayehusika na kutunza mazingira Kampuni yake imepewa tenda kubwa ya mambo ya mazingira ili kumziba mdomo.



Candid Scope
 
Hivi afya zunazofaa kulindwa ni za wananchi tu au hata vijana wetu ambao ni watumishi wa humo viwandani?
 
Hivi viwanda vingetoka katkati ya mji vijengwe nje kabisa huko. Hata kiwanda cha bia TBL sio haja ya kuendelea kung'ang'ania pale Mariakoo.
 
Kwa kumwaga mvua ndio kabisa hao inaeza ikanyesha mvua kidogo sana halafu wao wanaachia mashimo yao maji mpaka mafuriko mafuriko ya boko yanasababishwa ba kiwanda kwa asilimia 80
 
Your take: Unahisi vumbi linalotoka pale linaishia maeneo jirani na kiwanda peke yake? Unadhani kiwanda kinashindwa kudhibiti hilo vumbi lisitoke?

Jamaa wana kiburi sana, wafungiwe tu.

kweli wewe ni cloroquine....!
 
Your take: Unahisi vumbi linalotoka pale linaishia maeneo jirani na kiwanda peke yake? Unadhani kiwanda kinashindwa kudhibiti hilo vumbi lisitoke?

Jamaa wana kiburi sana, wafungiwe tu.

Wafungiwe tu!! Ukijifanya mkaida, utafungiwa, namimi nasema wafungieni, eeh, maana hakuna namna nyingine, ukuambiwa usichafue mazingira na ukakaidi, utafungiwa.
 
Back
Top Bottom