Nimesoma kwenye magazeti na JamiiForums kuhusu kusimamishwa kazi kwa Maafisa wa NEMC kuwa walitumia madaraka yao vibaya kwa kukifungia kiwanda hicho kwa sababu walikuwa na vibali vyote vya kuendesha kiwanda hicho. Napenda kuelemiswa yafuatayo:-
- Hivi kweli Tanzania tumefikia hatua ya kufungua kiwanda cha nyama ya punda?
- Punda kama mnyama ni msaada mkubwa kwa jamii waishio vijijini, Je kuwa na kiwanda cha nyama ya punda haitapunguza idadi ya punda vijijini na kukinzana na dhana ya punda kuwa msaada mkubwa kule vijijini?.