Wakuu kwema, nimepata mtaji kidogo na kwa utafiti wangu nimeamua nifungue kiwanda kidogo cha kukamua mafuta ya alizeti na chakula cha kuku toka kwenye mashudu.
Sasa naombeni wenye uzoefu na hii biashara Naombeni msaada wenu, mashine ya kukamua mafuta ni tani moja kwa siku ni sh ngapi?
Je hii biashara kwa dar itanilipa ukizingatia itakuwa raw oil sababu sina nguvu ya ku refine.
Aliyeshawahi kufanya bussines plan naomba anisaidie.
Alizeti nitakuwa nachukulia singida.
Una uhakika wa kupata raw material ya kutosha ? Kwanini kiwanda usingekiweka hukohuko Singida kisha utengeneza chakula cha kuku ndio ukisafirishe kwenda Dar ambapo inaweza kuleta tija zaidi ?