Kiwanda cha kutengeneza Tambi

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Posts
5,407
Reaction score
5,245
Kumekucha tena,

Natamani niwe na kiwanda cha kutengeneza tambi kwa ajili chakula. Nimepata habari kuwa Unguja biashara hii ipo sana. Natamani kujua ukubwa wa mtambo/vifaa muhimu na gharama zake. Kama unajua cho chote basi tupia hapa ichangie utafiti wangu.
 


Kwa hiyo unataka kujenga Kiwanda cha kutengeneza tambi kwa ajili ya soko la Unguja? Utarusdisha mkopo kweli?
 
Kwa hiyo unataka kujenga Kiwanda cha kutengeneza tambi kwa ajili ya soko la Unguja? Utarusdisha mkopo kweli?

Sio soko la Unguja pekee, na maeneo mengine, ila habari zilizopo ni kwamba Unguja biashara ya utengenezaji tambi na kuuza ipo sana. Mkopo wa nini?
 

Wazo zuri!,ngoja waje wadau watumwagie maujanja.
 
Kwa ushauri wangu kama ur serious nenda unguja kaangalie wanafanyaje pitia viwandani..Unguja ni soko lake kubwa au kuna viwanda pia?
 

Tambi za kula ni deal sana.
Hapa Tanzania nimeona tambi za Metl(Mohamed Enterprises) tu ndo zimetengenezwa na kupakiwa vizuri zilozobaki ni za kienyeji ila nyingi zinatoka nchi za nje kama Italy.
Komaa na ndoto yako tambi zinauzika sana waulize hata wenye maduka ya rejareja na jumla watakuambia.
Cha msingi zitengeneze katika ubora wa kisasa zipack vizuri tafuta vibali vya TFDA na TBS utapiga bingo wala usiogope changamoto za hapa na pale angalia jinsi ya kukabiliana nazo tu.
Kila la heri.
 
Kwa ushauri wangu kama ur serious nenda unguja kaangalie wanafanyaje pitia viwandani..Unguja ni soko lake kubwa au kuna viwanda pia?

Nimeshaunga udugu na Mpemba mmoja ili awe mwenyeji wangu kisiwani Unguja. Nataka nikaone.
 

Asante kwa kunitia moyo
 
Malila mkuu vp project yako ya tambi ulifikia wapi
 
hakuna kisichowezeka na kaza buti tu kama una mautundu unaweza DIY au jaribu kutembelea SIDO kipawa utapata idea
na pia mashine hizo siyo complex no simple mashine kama itakua ya manial Jaribu kugoole pia utapata idea tofauti
kwa mfano hiyo inayoonekana hapo juu ina wheel na axle axle ambayo inakua na kitu tama trade za bolt kinachotokea chapati yako uliyooiandaa inapita na kukandamizwa huku ikikatwa kufuata mistari ya trade ,
NB mbona wachina wanaweza why not us Tuumize vichwa .
 

Haya ndio mawazo na mambo ya wanaume, asante sana mkuu.
 
Haya ndio mawazo na mambo ya wanaume, asante sana mkuu.
mkuu vp mashine za kutengeneza tambi sh ngap zipo wapi? me nataka zile tambi za bites pamoja na za kula nahitaji mashine zinazoweza kutengeneza
 
Nilipogundua kuwa kuna viwanda bubu vingi mtaani nikaamua kuachana na wazo lenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…