Dr criminal
JF-Expert Member
- May 16, 2022
- 2,284
- 4,330
Mama mitano tena

Out there wakuuuu.
Mwanaume usitelekeze mtoto please!
Usimwache mwanamke aangaike kulea mtoto peke ake tafadhali, usifanye hivyo, hata kama una hali ngumu, hata kama unataka kuiokoa ndoa yako, hata kama ulitaka kumnyoosha huyo mwanamke, usitekeleze mtoto, iwe una miaka 25,30,35,40,45 au hata kama una miaka 50 as long as hujafa safari bado, usitelekeze mtoto.
Kama unatelekeze mtoto ili tu uokeo ndoa yako nakuhakikishia yule mtoto ana thamani zaidi ya ndoa
Kama unataka kuikimbia mimba kisa hali yako ngumu nakuhakikishia hali yako haiwez kuimalika Kwa kuimbia mimba
Kama unampa mwanamke mimba ili tu umnyooshe mwisho wa siku kinachonyooka ni kile kiumbe kilicho tumboni
Kama alishika mimba Kwa bahati mbaya, Kuna bahati mbaya nyingi sana zimekuja na mema, usitelekeze mtoto, please.
Kama alikushikia mimba ili tu akukomea, as long as ni mimba yako kweli, usitelekeze mtoto, msubiri aje umhudumie.
Ntawapa visa viwili
.................….…………………………………………………………………
KISA CHA 1.
Huyu ni mzee mmoja mitaa ya nyumbani nilipokulia, huyu mzee alikuwa ameoa na walibahatika kupata watoto watano na huyo mke wake.
Kazi kubwa pale home( kwenye ile wilaya) ni kilimo , na huyu mzee alikuwa mkulima wa wakaida tu, pato lake halikuwa haba, kupitia pato lake la shambani alijitahidi kusomesha watoto wake kadri alivyoweza Kila mtoto, yani mzee japokuwa pato halikuwa zuri lakini ushindwe wewe, alijitahidi wanawe wasome.
Kwenye hao watoto watano, watatu walibahatika kusoma mpaka elimu ya juu na kubahatika kupata kazi tena serikalini, mmoja mwalimu, mwingine hata sijuagi naskiaga tu ila huyo mwingine anafanya kazi wilayani, mmoja alisoma lakini sio Kwa kiwango cha hao watatu na ni mkulima aliyefanikiwa, yani anafanya ile kilimo biashara pato la kueleweka maisha safi, huyo mmoja ndo kama bahati mbaya hivi, bangi na yeye.
Sasa huyu mzee kwenye pita pita zake mikoa ya mbali alishawahi mpaga ujauzito uko mwanamke mmoja, lakini mwisho wa siku mzee akatembea kurudi home, kiufupi alimtelekeza yule mwanamke na mimba yake, akamuambia kwamba yeye ameoa ana mke wake na hawezi kuwa na wake wawili, mwanamke akamuomba awe hata anahudumia basi na awe anakuja kumtembelea mwanae mara moja moja, mzee akakubali lakini alipoondoka hakuwahi kurudi tena kule aliko mwanamke, yani aliwatelekeza.
Lakini kwa bahati nzuri au mbaya, huyu mzee alimwambia yule mwanamke exactly location yake anayotokea(Yani wilaya ya home) na pia alimtajia majina yake yote matatu ili mtoto akizaliwa apewe hayo majina
So kama unavojua siku hazigandi, ikawa ni saa, masaa, siku, masiku, wiki, mawiki, mwezi, miezi, mwaka na mwisho wa siku miaka ya kutosha, yule mtoto kule akawa amekuwa, kumbe yule mwanamke alipoona mpaka mtoto amefikisha umri wa miaka 5, hakuna mwanaume hajawahi kuja na mawasiliano hakuna, akajua tu hapa nimetelekezwa na mtoto, yule dogo alipoanza kujitambua akamuuliza mama ake kuhusu baba ake mama akamjibu baba ako alifariki na ajali.
Sasa sijui zile zilikuwa ni busara tu akisubiri mtoto akue au baadae aliingiwa tu na upako, huyu mtoto baada ya ku-settle yani ameshasoma amemaliza na kaanza kushika shika visenti vyake, mama akamuita mwana na akampa mkasa mzima mtoto wake, kwamba "Baba ako hakufa, ilikuwa hivi, hivi na hivi, na nilikuficha ili tu usahau kabisa usitegemee kabisa uwepo wake ila leo umekuwa najua haiwezi kukusumbua, ila hilo jina ni kweli la baba ako na yeye anaishi mkoa fulani, wilaya fulani, ila sina uhakika Kama ni mzima au vipi maana tangu aondoke tulipoteza mawasiliano kabisa"
Jamaa kusikia hivo akasema anatami akamuone, mama akampa radhi zote jamaa akajipanga panga alivokaa sawa safari ikaiva, kufika kule baada ya kuhangaika kama siku 2 mbili tu akawa amefika nyumbani Kwa Mzee(Mzee ni maarufu kidogo afu mji ni mdogo tu), kufika pale mzee ana hari mbaya, yani hari mbaya, mzee anaumwa sana.
Kufika pale akajitambulisha japokuwa hawakumuelewa vizuri na mtu mwenyewe wa kuthibitisha hilo ndo huyo mgonjwa ikabidi wamuache kwanza.
Wamempeleka hospital lakini hamna kitu, kwahiyo wanamuangalizia nyumbani, pesa ipo lakini watu ndo hawapo, mke wake peke hawezi ameshazeeka, wale watoto wake wanatoa tu pesa ila nyumbani hawaji kukaa na mzee wao, mzee anachoitaji ni love, anaitaji upendo na watu wakaribu sio pesa haiwezi kufanya kitu.
Sasa huyu mtoto wake wa nje ya ndoa, aliyetokea from nowhere sijui ndo shauku ya baba ake au ndio moyo wake tu uko hivo, yani yupo na baba yake bampa to bampa, anasaidia na huyo mama yake wakambo kumuangalia Mzee, anahakikisha Mzee yupo vizuri, kama kajikojolea ambadilishe nguo, akijinyea ambadilishe nguo, amnyweshe uji, yani ni kama vile mama mzazi anavo-care mtoto wake mchanga, kwahiyo care na madawa madawa ya kienyeji Mzee anaanza ku-recover, dawa tangu zamani zilikuwepi kwasababu pesa ilikuwepo lakini Mzee alikuwa anakosa love and care.
Kwahiyo bado mzee afya yake aijatengamaa lakini angalau tofauti na mwazo, Mzee alivopata nguvu kidogo ikabidi amuulize jamaa na mtoto akampa mzee mkanda mzima, mzee wa watu ni machozi tu, ikabidi amtambulishe kwenye familia yake.
,................................................,...............................
Ndio juzi hapo nimeenda home mama angu ananipa hii story yote,, hope mzee atakuwa vizuri
Sio kwambaa usitelekeze mtoto kisa hiyo story hapana , ila usitelekeze mtoto Kwa sabab:
-Mwanamke uliyemtelekezea atapata tabu sana kumlea peke ake
-Yule mtoto atakulia mazingira magum
-Yule mtoto anakosa malezi ya baba, anakosa viini vya uanaume
-Hatujui kesho yetu, hatujui nani atatatuzika, unaweza kuwa na pesa mpaka uzeeni, lakini itafikia hatua unahitaji zaidi watu tena wenye upendo na sio pesa
-Unatengeza yatima wa uwongo, unamdhulumu yule mtoto
Mi nalog out
Dr criminal.