Kivipi 16% ya Tanzania ni sawa na 84% ya Barrick?

Kivipi 16% ya Tanzania ni sawa na 84% ya Barrick?

Biashara iendelee na jamaa watoe financial statements zao zikikubali mizania na sie tunaweka mtonyo kununua hisa mpaka 50% ili nipate haki sawa na faida. Inamaana kama wanaoa 16% naongeza 34% kukata mzizi. Kama umemuelewa Allen inawezekana vipi mwenye 16% apate sawa na mwenye 84%???

Na kwakuwa hisa wanaendelea kuuza na biashara inalipa mbeleni tutakuwa na uwezo wa kumiliki hisa nyingi na kuwa na maamuzi. Mabepari hawanaga free ride.
Wamesema hawatoi financial statement? Kwani mwanzo walikuwa hawatoe financial statements?
Okay let say wametoa financial statement, tukanunua hizo hisa, biashara ikileta hasara, hautolalamika tumepoteza mabilioni?

Usilete ushabiki tu hapa, cha msingi nikupambana tupate hiyo hela na mapasu tuliyokubaliana.

Na uwakika 100%, tume ingesema tumepata 16% then tutanunua hisa 34% kwa mabilioni ya shilingi, bado ungepiga kelele, unabisha?

This is a good offer, tunatakiwa tubane utekelezaji wake, hilo ndo la msingi. Tukabe tuhakikishe tunapata chetu.
 
Ningependa kweli tugawane hiyo faida baada ya stahiki zote za serikali 50/50 kama alivyosema waziri, lakini nikiwasoma barrick sioni kama lugha yao ni sawa na ile ya waziri, wao wanaongea economic benefits 50/50. Time will tell kwani hapa huenda tukapata principles mpya za kufaidika na mali asili hata kama zina defy logic tulio zoea. Niliwasikia wachumi wawili wakisema 50/50 peke yake sio issue, issue ni kudhibiti gharama za kuzalisha kwani hawa wenzetu wana kitu inaitwa transfer pricing-yaani wanakuwa na kampuni nyingi tu chini ya kampuni moja kubwa, halafu hizi kampunu zinauziana huduma na vifaa vya kazi kwa "bei waijuayo wao" matokeo yake faida inakuwa ndoogo. Ngoja tusubiri.
 
Wamesema hawatoi financial statement? Kwani mwanzo walikuwa hawatoe financial statements?
Okay let say wametoa financial statement, tukanunua hizo hisa, biashara ikileta hasara, hautolalamika tumepoteza mabilioni?

Usilete ushabiki tu hapa, cha msingi nikupambana tupate hiyo hela na mapasu tuliyokubaliana.

Na uwakika 100%, tume ingesema tumepata 16% then tutanunua hisa 34% kwa mabilioni ya shilingi, bado ungepiga kelele, unabisha?

This is a good offer, tunatakiwa tubane utekelezaji wake, hilo ndo la msingi. Tukabe tuhakikishe tunapata chetu.

Huwezi kupambana ukapata pesa ya bure labda kama USAID, hii ya biashara inahitaji tahadhari kubwa ndio tunachosema si nasie tununue hisa ili tuwe na haki sawa na wao katika biashara shareholders hawadanganywi kama inavyodanganywa serikali, ndio maana watu wa fedha wanaomba FS ili wajue uwezo wa biashara, faida na hasara. Hamuwezi pata chenu wakati hamjatoa kitu.
 
Upo sawa kabisa, tatizo hizo hela zipo? Na kamati ingekubali hivyo msingepiga kelele?
Najua maamuzi hayo yangefanyika, bado tungekuwa kwenye mijadala humu jf.
Let take the win and move on.
 
Suala hili ni pana ila nijaribu kwa kifupi tu kutoa picha ya lengo la serikali kwa jicho langu. Tanzania tuna madini ya dhahabu katika ardhi yetu. Madini yana thamani kubwa kwenye soko la dunia ila sisi hatujawa na utaalamu wala nyenzo za kuyachimba wenyewe na kuyauza kwa faida wenyewe pamoja na kuwepo kwenye ardhi yetu miaka nenda rudi.

Mtazamo wa Rais muasisi wa taifa hili kihistoria na kwa kuzingatia hila za kibiashara na ujanja wa makampuni ya kigeni yenye uwezo wa kuyachimba haya madini ilikuwa ni kuwa; Kwa kuwa hatujawa na utalaamu/wataalamu wenye uwezo na nyenzo za kuyachimba madini yetu, ni bora yakae ardhini hadi hapo watoto wetu watakapopata akili ya kuyachimba na kutunufaisha sisi kwa kiwango kikubwa.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa hadi kufikia mwisho wa awamu ya pili ya Rais Alhaji Mwinyi, Baada ya hapo kuanzia awamu ya tatu Rais Ben Mkapa: mambo ya ubinafsishaji mali ulipoanza kushika kasi ndio tukaona ujio wa wawekezaji mbali mbali wakiwemo Barrick. Hapa tuelewe kuwa kuna mabadiliko/maamuzi ya kisera yaliyopelekea kuruhusu uchimbaji au kwa ubia na shirika letu la madini STAMICO au kwa makampuni ya uwekezaji kutoka nje kwa utaratibu wa kulipa kodi na mrahaba.

Asilimia 16% iko kwenye umiliki wa kampuni ya ubia itakapoundwa ambayo itashughurika na uchimbaji wa dhahabu na umiliki unategemea ni mtaji gani unaingiza kwenye ubia,Yawezekana hivyo ndivyo walivyokubaliana kwa maana ya kwamba 84% ya umiliki wa mbia wetu inahusisha: utaalamu,teknologia itakayotumika, uongozi wa kampuni pamoja na mitambo na vifaa vitakavyofanikisha uchimbaji. Kwa upande wetu mchango wetu kama mtaji kwa kampuni ni pamoja na ardhi yetu ambayo ina dhahabu tayari na ulinzi miundombinu ya barabara na nishati kwenye eneo la mgodi. Hapa ifahamike kuwa tunashiriki kwenye uwekezaji tukimiliki 16% mtaji wa kampuni na kama itabidi kuwekeza zaidi tutachangia kwa uwiano huo,hatukupewa bure kama baadhi ya wengine wanavyoandika-Ardhi ni mtaji tosha.

Hii asilimia 50%/50% iko kwenye kugawana faida au hasara itokanayo na shughuri nzima ya uzalishaji kwa mwaka, hapa tusichanganye na ile 16% ya umiliki kwa kuwa ni vitu viwili tofauti. Kawaida faida hugawanywa kwa wabia baada ya kutoa gharama zote na kulipa kodi zote stahiki. Inawezekana masharti yakaonekana kuwa magumu kwa wawekezaji na hivyo kutishia kujitoa, lakini labda lengo la serikali ni kuelekea kuchimba wenyewe kwa kutumia makampuni ya kitanzania na wataalamu wa kitanzania. Hii kwa tafsiri yangu ni "kubaliana na matakwa yangu tufanye biashara au niache nihangaike mwenyewe na mali zangu".
 
Hivi acacia akisema apewe chake asepe itabidi nasie tuchangie kwa 16%? Kuwinda chonja kunahitaji umakini
 
Hivi acacia akisema apewe chake asepe itabidi nasie tuchangie kwa 16%? Kuwinda chonja kunahitaji umakini
 
Yaani wazungu 25 wenye akili wakae mezani watoke kapa? Namashaka sana
 
Kuna uzi mmoja uko humu Jf yote hayo yameelezwa kwa ushahidi wa pande mbili Kuhusu iyo 50/50 tafuta huo utaelewa zaid
 
Back
Top Bottom