Kivipi 16% ya Tanzania ni sawa na 84% ya Barrick?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,924
Reaction score
50,992
Mimi siyo msomi wala mtaalamu wa Hisabati, lakini nimeulizia kwa watu wenye uwezo wa fani hiyo nipate ufafanuzi kuhusu sintofahamu inayoendelea kwenye Jamii yetu juu ya "Gawiwo" la 50/50 Tanzania na Barricks tutakalogawana baada ya Kampuni "Mpya" Kuundwa.

Nimeambiwa kwamba gawiwo kwenye biashara hutokana na idadi ya asilimia za hisa zinazomilikiwa na wenye hisa. Nimeambiwa kwamba mwenye hisa nyingi ndiye anayepata gawiwo kubwa na mwenye hisa chache anapata gawiwo dogo. Hata hasara ikitokea ni hivyo hivyo.

Sasa kama hiyo nadharia kuhusu Gawio ni ya kweli, inakuwaje tunatangaziwa kwamba Profesa kabudi na wenzake wameongoza majadiliano yatakayowezesha Tanzania kugawana faida ya 50/50 na Barricks kampuni mpya itakapoundwa?

Hisa zetu za kupewa za 16% zinawezeshaje sisi kupata gawiwo sawa na Barricks wenye hisa 84%? Umiliki wa hisa kwenye makubaliano hayo siyo ndiyo utakaotumika kufanya ukokotozi wa jinsi ya kugawana faida? Au kuna kanuni tofauti itakayotumika mbali na kuangalia umiliki wa idadi ya Hisa?
 
Sababu tanzania ni mmliki na barric ni muekezaji
 
Bro' hapo tujiandae kama taifa kulipa 50/50 kwa kila hasara inayotekea katika shughuri za uzalishaji.Hii 50/50 tutaikataa wenyewe muda si mrefu.Haiwezekani upate 50/50 kwenye faida tuu halafu ikitokea hasara unakaa pembeni.Tatalipa saaana kuliko kulipwa.
 
Yes hisa huwa ina amua mgawano, ila kazi ya hisa siyo hiyo tu. Kiasi cha hisa kina amau pia una sauti kiasi kani kwenye kampuni katika maamuzi. Ukiwa na hisa kubwa unakuwa na sauti kubwa.

Kwa hiyo basi, kwa mtazamo wangu, Barrick wametaka kutupa mgawano mkubwa 50/50 lakini hawapo tayari kutupa hisa ya 50% maana tutakuwa na sauti kubwa sana kwenye kampuni.

Pia hisa inaendana na pia capital utakayoweka au unayoweka, sisi 16% tumepewa bure, tukipewa kubwa sana bila kuwekeza hela yoyote kampuni ingefilisika. Kugawana 50/50 ni profit wakati gharama zote zimesha katwa.
 
Kugawana 50/50 ni profit wakati gharama zote zimesha katwa.
Ndiyo nataka kujua inawezekanaje? Maana kwa maelezo yako ni kwamba wenye sauti ni Barricks, sasa ni kwa kanuni ipi itakayotumika sisi kugawana 50/50 na wale wenye hisa 84% wakati sisi tuna 16%?
 
Mleta mada hili mbona limeshajadiliwa na kutolewa ufafanuzi, hizo ni economic benefit, kama hujui labda kuanzishe uzi mwingine,

na hayo sio mageni jamefanyika peru argentina saudia elitrea, tena kule elitrea wanaofanyakazi mgodini ni jkt ya huko na badala ya kulipwa mshahara pesa inaenda serikalini ndio maana wanajeuri hata ya kupigana na ethiopia.

Nasisi tusiishie japo tu, walinzi wa mgodini badala ya kuwa makaburu wa gfs wawe sumajkt, watingaji badala ya kuwa bynacat na kakola mining wawe sumajkt, malori ya kusomba mining logistics badala ya kupewa huyu dogo wa mombasa iwe kazi ya sumajkt, ili dola yote inayopatikana iende hazina.
 
Tatizo lako bado unalinganisha 16% na 50/50. Kama maelezo yangu hapo juu 16% ni hisa ya umiliki wa kampuni. 50/50 ni makubaliano mengine ambayo hayaja angalia hisa.
Unajua inasemekana bongo bado madini yapo mengi sana. Tungeweza pewa hisa 50% lakini tatizo linakuja kuwa hisa ina mambo mengi ndani yake.

Kama biashara nzuri, 50/50 siyo ishu. Acha kuchulia mfano wa faida wa laki moja ambao mtagawana elfu 50 50. Chukulia faida ya mamilioni, hata mkigawana 50/50 bado hela ndefu, zaidi ya hapo, ita wa guarantee kufanya biashara bongo muda mrefu.

Na pia kama wamekubali 50/50 inamaana faida ni kubwa mno.
 
Kinachojadiliwa ni mali yetu watz. Ni kwamba wachache wetu wanasahau kuwa haya madini ni yetu watz. Tunaweza kuamua kuyachimba wenyewe au kuwa na mwekezaji. Badala ya viongozi wetu kuhakikisha kilicho chetu waTz wao wamewapa wageni. Hilo ndio tatizo kubwa na sasa limekaa kisheria na tumesainisha kuwa wazungu watatuibia hadi watakapochoka wenyewe.

Hiyo hisa ya asilimia 16% ni kama mfano kampuni itakufa leo nani apate nini. Kwa kuwa wanachimba madini yetu lazima tuwe na sehemu ya hisa. Hii haimaanishi kuwa madini yote ni ya kwao. Wao wana hisa kubwa katika umiliki wa kampuni tu si umiliki wa madini au faida kwa asilimia kubwa. Na hii ndio kitu ambacho viongozi wetu waliopita walikosea kwa tamaa ya pesa za kupewa na wafadhili.

Tunamshukuru Rais wetu kwa kuliona hilo. Kwa macho ya upinzani hutaliona hilo. Kama wewe ni Chadema vaa macho ya raia mwema utaona tofauti. Mpinzani hapendi nchi ifanikiwe, yeye mpinzani hupinga kila kitu kinachofanyika. Sisi kama raia wa Tz hatuna pengine pa kwenda na hapa ndio petu lazima tuipiganie nchi yetu na mali zake.
 
Mimi siyo msomi wala mtaalamu wa Hisabati, lakini nimeulizia kwa watu wenye uwezo wa fani hiyo nipate ufafanuzi kuhusu sintofahamu inayoendelea kwenye Jamii yetu juu ya "Gawiwo" la 50/50 Tanzania na Barricks tutakalogawana baada ya Kampuni "Mpya" Kuundwa.

Nimeambiwa kwamba gawiwo kwenye biashara hutokana na idadi ya asilimia za hisa zinazomilikiwa na wenye hisa. Nimeambiwa kwamba mwenye hisa nyingi ndiye anayepata gawiwo kubwa na mwenye hisa chache anapata gawiwo dogo. Hata hasara ikitokea ni hivyo hivyo.

Sasa kama hiyo nadharia kuhusu Gawio ni ya kweli, inakuwaje tunatangaziwa kwamba Profesa kabudi na wenzake wameongoza majadiliano yatakayowezesha Tanzania kugawana faida ya 50/50 na Barricks kampuni mpya itakapoundwa?

Hisa zetu za kupewa za 16% zinawezeshaje sisi kupata gawiwo sawa na Barricks wenye hisa 84%? Umiliki wa hisa kwenye makubaliano hayo siyo ndiyo utakaotumika kufanya ukokotozi wa jinsi ya kugawana faida? Au kuna kanuni tofauti itakayotumika mbali na kuangalia umiliki wa idadi ya Hisa?

Haya zaidi ni mambo ya Ngoswe, na ya Ngoswe aachiwe ngoswe. Afadhali wewe umeandika wengi wameshikwa na butwaa/kihoro na daflau hata hawajui wafanye nini. Mzungu ukarimu wa namna hii kautoa wapi na kaanza lini, mahesabu ya hawa jamaaa yanasoma loss kwa muda sasa unaingizwa mkenge kukubali 50/50 katika faida less than 0 hapa Mkubwa amepelekwa choo cha kike.

Na kwakua ni mbishi na asiyetaka kusikia tofauti na anachojua muacheni muda utamnyoosha tu wenyewe wanaita economic benefit mbali ya hiyo Halmashauri nazo zitaendelea kubonya mrabaha na SR inaendelea kama kawa. To be curious hii kitu sio visible kuna something fish going on to the expense of political gain sio biashara.
 
Dear wana JF.
Ni vigumu sana Ku deal na mabepari,especially kwenye sector ya madini.
Kuna vitu viwili katika mgawanyo wa madini.
1. Royalty
2. Joint venture
Mimi sijaona hayo makubaliano lakini kama serikali imechukuwa namba mbili kama chaguo imeula wa chuya.
Joint venture mnagawana faida baada ya matumizi na ninavyowafahamu hawa ndugu kila siku itakuwa hasara kwa sababu ya overheads.
Ni bora serikali ikachukua hata 10% percent ya royalty kuliko kusubiri 50% ambayo ni ndoto.
Lastly, serikali iwalazimishe kurudisha faida yao katika miradi endelevu kama viwanda na kilimo.
 
Mleta mada hili mbona limeshajadiliwa na kutolewa ufafanuzi, hizo ni economic benefit, kama hujui labda kuanzishe uzi mwingine,

na hayo sio mageni jamefanyika peru argentina saudia elitrea, tena kule elitrea wanaofanyakazi mgodini ni jkt ya huko na badala ya kulipwa mshahara pesa inaenda serikalini ndio maana wanajeuri hata ya kupigana na ethiopia.

Nasisi tusiishie japo tu, walinzi wa mgodini badala ya kuwa makaburu wa gfs wawe sumajkt, watingaji badala ya kuwa bynacat na kakola mining wawe sumajkt, malori ya kusomba mining logistics badala ya kupewa huyu dogo wa mombasa iwe kazi ya sumajkt, ili dola yote inayopatikana iende hazina.

Mkuu Eritrea unazungumzia Bisha mining, si kweli kwamba pale bisha mining wanaofanya kazi ni hao uliowasema, expert wapo wakutosha tu pale na mpaka watanzania wapo pale kama experts hasa upande wa mining operations, Aggreko ndio wanauza umeme mgodini na wafanyakazi wao 80% ni wageni.. Ulinzi ndio unafanywa na hao unaowaita JKT ya huko.

Bynacat ni contractor ambaye anauzoefu na shughuli hiyo, hivyo kwa urahisi, speed, na maximum production lazima utumie mtu wa namna hiyo, hizi kazi haziendi tu kwa matakwa ya kisiasa lahasha hizi ni kazi za kitaalamu hivyo zinahitaji wataalamu wenye skills,knowledge,exposure ili mwisho wa siku uzarishaji uwe mkubwa na watu wawe salama pia..

Suala la logistic unaweza ukawa sahihi lakini pia unaweza usiwe sahihi, Tatizo kubwa la kufanya kazi na serikali ni urasimu ambao mwisho wa siku utachelewesha uzarishaji, mfano ni pale STAMIGOLD TUWALAKA ambao uko chini ya serikali lakini mwisho wa siku mpaka leo faida haijawahi kuonekana zaidi ya hasara na madeni, DAR ES SALAAM PORT ambapo tunaendesha wenyewe lakini kila siku tunashindwa kupata super profit zaidi ya makelele tu na hasara kila siku..

ILI TUWEZE KUENDESHA MIGODI WENYEWE, SIASA IWEKWE PEMBENI, UKABILA,UDINI,UNDUGU UWEKWE PEMBENI, utaalamu na uwezo kiutendaji ndio silaha pekee ikiambatana na benefits nzuri na sio hii mishahara mbuzi ya TGS sijui, mining ni eneo la risk na hatari nyingi, ili watu wawe salama unahitajika uwekezaji wenye tija na sio SIASA.
 
Tatizo lako bado unalinganisha 16% na 50/50. Kama maelezo yangu hapo juu 16% ni hisa ya umiliki wa kampuni. 50/50 ni makubaliano mengine ambayo hayaja angalia hisa.
Unajua inasemekana bongo bado madini yapo mengi sana. Tungeweza pewa hisa 50% lakini tatizo linakuja kuwa hisa ina mambo mengi ndani yake.

Kama biashara nzuri, 50/50 siyo ishu. Acha kuchulia mfano wa faida wa laki moja ambao mtagawana elfu 50 50. Chukulia faida ya mamilioni, hata mkigawana 50/50 bado hela ndefu, zaidi ya hapo, ita wa guarantee kufanya biashara bongo muda mrefu.

Na pia kama wamekubali 50/50 inamaana faida ni kubwa mno.
Takwimu zinaeleza so far madini yote yaliyowahi kuchimbwa hapa nchi hadi sasa ni 9.9% or lets say 10%...kwa hiyo bado mzigo upo!
 
Haya zaidi ni mambo ya Ngoswe, na ya Ngoswe aachiwe ngoswe. Afadhali wewe umeandika wengi wameshikwa na butwaa/kihoro na daflau hata hawajui wafanye nini. Mzungu ukarimu wa namna hii kautoa wapi na kaanza lini, mahesabu ya hawa jamaaa yanasoma loss kwa muda sasa unaingizwa mkenge kukubali 50/50 katika faida less than 0 hapa Mkubwa amepelekwa choo cha kike.

Na kwakua ni mbishi na asiyetaka kusikia tofauti na anachojua muacheni muda utamnyoosha tu wenyewe wanaita economic benefit mbali ya hiyo Halmashauri nazo zitaendelea kubonya mrabaha na SR inaendelea kama kawa. To be curious hii kitu sio visible kuna something fish going on to the expense of political gain sio biashara.
Haya ni matunda ya zile discussions za Tume...sio matakwa ya Rais..
 
Embu niambie, wewe ulitaka makubaliano ya namna gani? Labda tuanzie hapo.
Kikwete alisema "Usipokubali kuliwa kidogo huli"
 
Tume imedeliver expectations za MKUU, wala msiwabebeshe mzigo wajumbe wa tume. Raisi alisema hiki kabla hata ya kuchukua form ya kugombea sie watu wazima bhana tuheshimiane.
 
Embu niambie, wewe ulitaka makubaliano ya namna gani? Labda tuanzie hapo.
Kikwete alisema "Usipokubali kuliwa kidogo huli"

Biashara iendelee na jamaa watoe financial statements zao zikikubali mizania na sie tunaweka mtonyo kununua hisa mpaka 50% ili nipate haki sawa na faida. Inamaana kama wanaoa 16% naongeza 34% kukata mzizi. Kama umemuelewa Allen inawezekana vipi mwenye 16% apate sawa na mwenye 84%???

Na kwakuwa hisa wanaendelea kuuza na biashara inalipa mbeleni tutakuwa na uwezo wa kumiliki hisa nyingi na kuwa na maamuzi. Mabepari hawanaga free ride.
 
Back
Top Bottom