G-Mdadisi
Senior Member
- Feb 15, 2018
- 157
- 99
JESHI la Polisi Mkoa wa KaskaziniPemba linamshikiiwa kijana mwenye umri wa miaka 15 kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 3.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamisha Msaidizi Juma Sadi Khamis amethibitisha tukio hilo na kusema limetokea shehia ya Kiuyu mingwini wilaya ya Wete.
Akizungumza Ofisini kwake kamanda sadi amesema mtuhumiwa huyo anaendelea kumhoji na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Aidha kamanda Sadi amewataka viongozi wa Dini kuendelea kutoa elimu ya kupinga matendo hayo sehemu za ibada ili kufanikisha lengo la serikali la kuyatokomeza matendo hayo.
Kufuatia mtuhumiwa huyo kuwa chini ya umri wa miaka 18, sheria namba 6/2021 , kifungu cha 45, (1) sheria ya mtoto ya zanzibar mahakama itamwachia mtoto huyo katika matunzo ya wazazi kwa sharti ya kwamba kila anapohitajika afikishwe mahakamani
#UGATvFurafaYako