CCM walimsoma Seif Sharif Hamad kwa muda mrefu, wakagundua kuwa kilichokuwa kikimsumbua ni ukubwa, wakatafakari baadaye wakamwita na kumwambia kuwa, 'kuanzia leo utakuwa mkubwa - Makamu wa kwanza wa Rais, hutakuwa na kazi maalum, Rais asipokuwepo, Makamu wa piliwa Rais atashikilia serikali na wewe utakuwa makamu wake', yeye akaitikia kwa furaha kubwa kuwa, 'hayo ya nani atashikilia serikali kama Rais hayupo au kutokuwa na majukumu maalum ya kiutendaji katika serikali siyo muhimu, cha muhimu mnihakikishie kuwa wakati wote mtanitaja kuwa Makamu wa kwanza wa Rais, na maslahi yangu yawe kama ya 'Makamu wa Rais halisi'. CCM wakamkubalia kwa kumweleza kuwa jukumu lake kubwa litakuwa kupooza hasira za wanachama wa CUF.
Kiutendaji, Seif Sharif Hamad ni makamu wa kwanza wa Rais kama Rais yupo; lakini pia ni makamu wa kwanza wa Makamu wa Pili wa Rais.