Kiutawala: Namfananisha Maalim Seif na Queen Elizabeth I

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
125
Nikitatafakari sana suala la Hamad Seif ( Makamu wa kwanza wa Rais) baada ya kusoma mabadiko yaliyofanywa kwenye katiba, naona kama vile utawala wake utashabihiana sana na utawala wa Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Yaani atakuwa yuko pale kwenye cheo chake cha sasa ili kuwaunganisha pamoja na kuwatuliza wapemba wasifanye wamalize tofauti zao. Hata nadiriki kusema kufikiri mbele zaidi na kuona hata malkia wa uingereza ana nguvu/sauti ya kimaamuzi kwenye serikali ya UK kuliko Seif aliyeolewa na CCM A ya Kikwete kuunda CCM B inayopambana na CHADEMA.
 

Awo

JF-Expert Member
Apr 12, 2010
793
476
Hapana - huwezi kumlinganisha Seif na Queen Elizabeth. Huyo mfananishe na Rais Canan (not sure of the spelling) Banana wa Zimbabwe enzi zile Mugabe ni Waziri Mkuu.
 

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
125
Mkata utepe na muitisha mikutano ya amani

Wanachama wa CUF sijui wanasubiri nini wasijiunge na CHADEMA, Mwenzao keshapata alichokuwa anakitaka na sasa ni kazi moja tu kutekeleza ilani ya CCM ambayo practically haijawahi kutekelezeka tangu uhuru.
Wapemba subirini kwa matumaini huku mkiuza urojo, kumbe mtu mwenyewe mnaemuamini ni mlevi wa madaraka, atakuja kukumbuka baada ya miaka mitano ya mwanzo ulevi umeisha na anahitaji kura nyingine alewe tena.
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,933
1,509
Kiongozi wa Matamasha na kukata utepe duuuuu! JOKA LA KIBISA HALINA SUMU!
 

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,234
28,204
CCM walimsoma Seif Sharif Hamad kwa muda mrefu, wakagundua kuwa kilichokuwa kikimsumbua ni ukubwa, wakatafakari baadaye wakamwita na kumwambia kuwa, 'kuanzia leo utakuwa mkubwa - Makamu wa kwanza wa Rais, hutakuwa na kazi maalum, Rais asipokuwepo, Makamu wa piliwa Rais atashikilia serikali na wewe utakuwa makamu wake', yeye akaitikia kwa furaha kubwa kuwa, 'hayo ya nani atashikilia serikali kama Rais hayupo au kutokuwa na majukumu maalum ya kiutendaji katika serikali siyo muhimu, cha muhimu mnihakikishie kuwa wakati wote mtanitaja kuwa Makamu wa kwanza wa Rais, na maslahi yangu yawe kama ya 'Makamu wa Rais halisi'. CCM wakamkubalia kwa kumweleza kuwa jukumu lake kubwa litakuwa kupooza hasira za wanachama wa CUF.

Kiutendaji, Seif Sharif Hamad ni makamu wa kwanza wa Rais kama Rais yupo; lakini pia ni makamu wa kwanza wa Makamu wa Pili wa Rais.
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,944
8,834
payuka... nilipoona title nikajua unamfananisha na queen suzy wa twanga au queen latifa

dah
 

Mwapachu

Member
Nov 1, 2010
14
0
Kwa kweli mkuu Seif Hamad ni mroho wa madaraka na atajuta. Ninge mueshimu kama asinge kubali kuwa makamu wa kwanza wa rais wakati rais yupo tu hata mjinga gani anaweza kuiona lakini Seif hakuona hilo, sasa sijui nimwite nani. La busari angemchagua mtu toka CUF kuchukua hiyo nafasi yeye abakie kwenye chama halafu angeweza kuona ukweli. CUF wangejiunga na Chadema lingekua jambo la busara mkuu
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom