Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 116,124
- 214,217
Nitasema kweli daima , fitna kwangu mwiko .
Wanaccm wote wa Tanganyika na Zanzibar mara zote wamejiapiza kuhakikisha Maalim Seif Sharrif Hamad hapati uongozi wa Juu wa Zanzibar , iwe kwa halali au kwa haramu, chaguzi zote hilo limeshuhudiwa kwa macho yetu likifanyika ikiwemo kuumiza na kuua wale wote waliomuunga mkono Maalim katika harakati zake, Ushahidi wa wazi uko dhahili
Maalim Seif ndio Mwanasiasa wa Zanzibar aliyetukanwa Matusi yote unayoyafahamu hapa duniani kuliko mwanasiasa yeyote wa Zanzibar , Watukanaji wakubwa wakiwa viongozi wa CCM, leo hawa ndio wanajifanya wako mstari wa mbele kumuenzi Maalim Seif , Huu ni unafiki na haukubaliki duniani na ahera .
Maalim Seif amewahi kuwekwa gerezani na serikali ya CCM kwa kesi ya Uongo ya Uhaini pamoja na Duni Haji na Wengine , kabla ya kumsifia kizandiki mtueleze ni lini ccm ilimuomba radhi Maalim Seif kwa kumsingizia Uhaini wa Uongo?
Labda kwa kumbukumbu tu ni kwamba , Wakati wabunge wote wa upinzani wakisusia uzinduzi wa bunge baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 , uliopangwa kuhutubiwa na John Magufuli aliyetangazwa mshindi wa Urais wa Tanzania , ili kupinga Maalim Seif kunyang'anywa ushindi kwenye uchaguzi ule wa Zanzibar , MBUNGE PEKEE WA UPINZANI ALIYESALIA NDANI YA BUNGE LILE ALIKUWA MBUNGE WA KIGOMA ZITTO KABWE , Ushahidi wa maandishi na video upo .
Nasisitiza kwamba ni laana kubwa sana kumsifu mtu kinafiki , wale waliompinga kwa uchawi na hata kwa bunduki leo ndio wanajifanya kumsifia , Hii ni ghiliba ya kiwango cha chini sana na haikubaliki .