Mkuu
Mzizi mkavu sijawahi kwenda hospitali na kupata vipimo vya aina yeyote kwa sababu kuna kipindi nilimcontact daktari mmoja na kama unavyojua madaktari wetu akaniambia nenda kesho ukiendelea hivihivi urui, kesho yake nilikua poa hivyo sikwenda tena. Sasa kwa kuwa hili tatizo huwa linanikumba kwa muda mchache ndani ya siku na hutokea baada ya muda mrefu sikuwahi kulipa umuhimu sana. Kuhusu makazi mie naishi Tanzania, na baridi ninayoiongelea hapa ni kale kabaridi ka jioni hasa pale ninapokuwa nje ya Dar-es-Salaam ( sio siku zote panapokuwa na baridi bali hutokea mara mojamoja).
Na tumaini nimekujibu maswali yako mkuu.