Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
- Wanajua kuwa wao ni wanachama wa chama tawala-CCM.
- Wanajua kuwa CCM ndiyo inayounda Serikali baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015.
- Wanajua kuwa, kama chama tawala, wanapaswa kutekeleza Ilani ya CCM waliyoinadi wakati wa uchaguzi.
- Wanajua kuwa Serikali ya CCM inatokana na wanachama wa CCM.
- Wanajua kuwa wapo vijana na watu wazima 'walioonekana' kwa Rais na kuteuliwa hapa au pale. Mfano, wale Vijana waliokuwa wakiitwa JUKWAA LA WAZALENDO.
- Wanajua kuwa utetezi wa chama chao CCM mitandaoni, redioni na runingani si utetezi wa hivihivi na wa kizalendo. Ni utetezi wa kimaslahi katika kuvizia teuzi mbalimbali.
- Wanajua na kuamini kuwa CCM ina hazina ya wanachama wanaoweza kushika nafasi yoyote ya kiuongozi Serikalini. Kwanini atoke ACT-Wazalendo?
- Wanajua kuwa Rais anawapenda wanachama wa chama chake na anawatumikia watanzania kwa uwezo wake wote ili kuendelea kuking'arisha chama chake. Kwa RC Mghwira vipi tena?
- Wanajua kuwa CCM imeuda na kutawala Serikali na Bunge na bado teuzi huongeza morali ya 'kujituma' ndani ya CCM. Hapo kwa RC Mghwira vipi?
- Wanajua na kuamini kuwa wapinzani hawana watu kama wao wenye uwezo na uzoefu wa uongozi wa kitaifa.