Kiu yangu si chama cha siasa

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,066
Watanzania tunataka kupotoshwa sana, kiu yetu si jina la chama cha siasa, hili linaushahidi wa kutosha, wananchi iwe tz au kwingineko duniani hawahitaji chama cha siasa isipokuwa wale tu ambao baba na bau zao walifanya chama ni chanzo cha mapato na ndo muhimili wa msingi mkuu ktk maisha yao.

Tuangalie ukweli pale ambapo CCM/TANU ilipigania maatakwa ya wananchi iliungwa mkono tena kwa hali na mali, NCCR waliwakilisha matakwa ya wananchi, watu waliwaunga mkono, pale ambapo TLP ilifanya hiyo, iliungwa mkono, pale ambapo CUF ilidai na kusimamia maslahi ya wananchi iliungwa mkono; sasa chadema vivyo hivyo inaungwa mkono sio kwa jina lake zuri, sio kwa sura za mwenyekiti na katibu wake kuwa nzuri, sio kwa urembo na utanashati wa wabunge wake, la hasha ni kwa hoja ile ile kusimamia matakwa ya wananchi.
-Kupinga wizi wa mali ya umma/Ufisadi
-Kutaka katiba mpya
-Kupinga unyonyaji kwenye migodi ya madini
-Mfumko wa bei, bei za bati simenti, soda, sukari, ada za shule, chakula nk mifani michache
-uongozi wa bora liende huku watu wanaumia
-tunataka maendeleo sio maendejana
-uhuru wa habari na haki ya kuwakosoa viongozi wakichemka
-haki ya kuandamana na kufanya mikutano
-haki ya unafuu kwenye maisha, ellimu, kupinguza kwa maksudi matabaka ya walionacho na wasionacho
Na mengine mengi

Haya mambo chadema wakiyapigania, wataendelea kuvaa beji ya chama cha umma chenye nguvu ya wananchi na umma kwa ujumla, wakiacha wanapotea kama NCCR, CUF, TLP UDP etc.

Mbaya zaidi CCM wakifanya matakwa ya wananchi, upinzani utakosa mashiko. kwa mwenye akili ndani ya CCM kama yupo (Nape-umepigana na magamba umekwisha wewe mwenye, kimya kama mavi chooni, Mwigulu-mchumi daraja la I tumia akili sio tumbo, Kinana-Si ulipewa ukatibu mkuu ufufue chama au uongoze umafia ndani ya chama-Uliwahi kuwa usalama wa taifa wewe, Mwanachama wa CCM (Wasaidieni viongoozi wenu kurejesha kazi ya wananchi ndani ya chama sio kuwaibia wananchi na wengine) suala sio CDM au chama chochote cha upinzani, suala ni kuwatimizia wananchi, pale wanapohitaji uwakilishi kweli wawakilishwe na waone kuna watu au chama kinawasimamia, sio kinaungana na matapeli kuwaibia wananchi, au Nyingi wenyewe kuwaibia wananchi harafu mnajifanya wajinga, EPA, RADA, RICHMOND etc. WATAKIKATAA CHAMA CHENU HATA WAKIWA KABURINI.

Kiu yetu sio chama ni maendeleo na maisha bora hata kikwete anajua, sasa vita na chama inatoka wapi? Je mtaishinda vita hiyo kama walionyuma ya chama ni wananchi wenyewe??? fikirieni sana kabla mandela hajafa maana is the icon of wisdom, mass power and rule of law.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom