Kituo kikuu cha Mabasi Masasi ni kero Tupu

Program Manager

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
2,517
3,441
Mji wa Masasi ni miongoni mwa miji ya kibiashara na inawezekana ukawa kitovu cha biashara kwa miji ya kusini kama Nachingwea, Newala,Nanyumbu na Tunduru.
Licha ya kuwa ndiyo mji unaokua kwa kasi sana katika mkoa wa Mtwara ukiacha Mtwara yenyewe, mji wa Masasi una kero sugu mbili ambazo ni kukosa Kituo Cha Mabasi cha kisasa na kutokuwa na mtandao wa barabara za mitaa (za lami).

Kero ya stendi

Mwaka 2019 Mh Rais JPM (r.i.p) alipofanya ziara ya kushtukiza mjini masasi alihoji miradi mingi ikiwemo mradi wa stand mpya na kaimu mkurugenzi kipindi hicho alijibia kuwa eneo limetengwa, pesa ipo na haraka mchakato wa ujenzi wa stendi mpya utaanza.

Cha kushangaza huu ni mwaka wa tatu sasa hakuna hata dalili za ujenzi wa stendi mpya na hii ya zamani imekuwa kero sasa hasa kipindi hiki cha mvua kunajaa tope na maji mpaka magari yanakwama.

Cc Mbunge wa jimbo la masasi mjini Mh Geofrey mwambe
 
Hali jinsi ilivyo
_20220124_190006.JPG
_20220124_185929.JPG
_20220124_185843.JPG
 
Mji wa Masasi ni miongoni mwa miji ya kibiashara na inawezekana ukawa kitovu cha biashara kwa miji kama Nachingwea, Newala,Nanyumbu na Tunduru.
Licha ya kuwa ndiyo mji unaokua kwa kasi sana katika mkoa wa Mtwara ukiacha Mtwara yenyewe, mji wa Masasi una kero sugu mbili ambazo ni kukosa Kituo Cha Mabasi cha kisasa na kutokuwa na barabara za mitaa (za lami).

Kero ya stendi

Mwaka 2019 Rais JPM (r.i.p) alipofanya ziara ya kushtukiza mjini masasi alihoji miradi mingi ikiwemo mradi wa stand mpya na kaimu mkurugenzi kipindi hicho alijibia kuwa eneo limetengwa, pesa ipo na haraka mchakato wa ujenzi wa stendi mpya utaanza.

Cha kushangaza huu ni mwaka wa tatu sasa hakuna hata dalili za ujenzi wa stendi mpya na hii ya zamani imekuwa kero sasa hasa kipindi hiki cha mvua kunajaa tope na maji mpaka magari yanakwama.

Cc Mbunge wa jimbo la masasi mjini Mh Geofrey mwambe View attachment 2094247
Aibu hiyo ipo hadi pale Mtwara mjini ambayo ni Icon ya Mkoa! Inashangaza kidogo! Nanyumbu wamejitahidi sana! Miji muhimu kama Mtwara na Masasi kukosa Stendi ni aibu kubwa. Kwa sasa, miji mingi ya hadhi kama Mtwara na hata Masasi yote ina stendi nzuri na za kisasa! Hii kila jambo kuwa wa mwisho Mtwara inakera sana. Nenda Iringa, Mbeya,Tabora, Mpanda, Sumbawanga, Kibaha, Morogoro, Singida, Babati, Tanga, Dodoma kutaja baadhi miji yote hiyo ina stendi mpya za basi, kwa nini Mtwara hakuna? Shida ni nini!?
 
Kwakweli inashangaza sana, unaweza kujiuliza kuwa wanaangalia vipaumbele gani katika kutoa fedha za miradi ya stendi za kisasa? Maana kuna baadhi ya miji unakuta mkoa mzima hakuna mji wenye stendi ya maana mfano mkoa wa Mtwara
 
Kwa kigezo cha stendi tu mkuu au kuna kingine?
Ndiyo mkuu, huko hawatajenga hiyo stand kamwe. Japo ushauri huu wa kuhama siko serious lakini jua hapo pesa ishapigwa na stand haitajengwa kwani hakuna maslahi huko wala mfatiliaji wa hilo kutoka serikalini.
 
Kuna fursa zipi mkoa wa Njombe?
 
Back
Top Bottom