Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Majaliwa amesema hayo leo Februari 7,2017 alipokutana na viongozi wa Wilaya hizo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta njia za kuondoa msongamano huo, na moja ya hatua alizowashauri kuchukua ni pamoja na kuhamisha kituo cha Mabasi ya Mikoani ya Kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutoka Temeke hadi Mkuranga
Amesema kwa sasa hakuna namna ambayo wataweza kuondoa msongamano huo zaidi ya kuhamishia kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini wilayani Mkuranga, amesema eneo la Mbagala kwa sasa lina msongamano mkubwa ambao ni lazima Serikali ichukue hatua za haraka za kuondoa
"Ikiwezekana mabasi ya mikoa ya Kusini yaishie Mkuranga, hivyo shirikianeni kutafuta eneo la kujenga kituo kikubwa cha kisasa cha mabasi, "alisema
Majaliwa amesema kituo hicho watakachokijenga kiwe na uwezo wa kuhudumia mabasi yote yatokayo mikoa ya kusini na kituo cha Mbagala kiwe cha daladala za kawaida
Pia amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kutawezesha kuongeza mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga
Majaliwa amewataka viongozi hao kwenda kujadiliana katika vikao vya mabaraza ya Madiwani juu ya mkakati huo na kisha kumpekea taarifa ifikapo Februari 15 mwaka huu
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema wazo hilo ni zuri na Wilaya yake ina maeneo ya kutosha kujenga miundombinu hiyo
"Ni kweli wilaya ya Temeke imeelemewa kwa maana ya maneno kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maendeleo na haina pa kupumulia zaidi ya Mkuranga, hivyo tupo tayari kushirikiana nao, "alisema
Aidha, Sanga ameiomba Serikali itakapoanza awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi ufike hadi Mkuranga mjini badala ya kuishia Vikindu
Amesema kwa sasa wilaya yake ina viwanda 67 ambavyo kati yake vipo vinavyofanya kazi na vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, hivyo mabasi hayo yatarahisisha usafiri kwa wafanyakazi.