KERO Kituo cha afya Bunju kinatoza gharama kubwa kwa wamama wajawazito kwenye kliniki zao za kwanza hadi za mwisho. Huu ni wizi!

KERO Kituo cha afya Bunju kinatoza gharama kubwa kwa wamama wajawazito kwenye kliniki zao za kwanza hadi za mwisho. Huu ni wizi!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Kituo cha Afya cha Bunju kimekuwa kikitoa huduma zisizoridhisha kwa wananchi, hasa katika upande wa kliniki za wajawazito. Mbali na utaratibu kuwa mbovu, pia kuna kutoza gharama kubwa zisizoeleweka.

Kwa mfano, mama mjamzito anapoenda kliniki ya kwanza, anatozwa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na vituo vingine vya afya au zahanati. Mimi binafsi nilimpeleka mke wangu kwa vipimo pamoja na ultrasound, ambapo tulitozwa zaidi ya shilingi 150,000/=. Hii ni tofauti kubwa ukilinganisha na vituo vingine ambavyo gharama yake huwa haizidi shilingi 50,000/=.

Aidha, kila tarehe ya kliniki anapokwenda, analazimika kwenda na zaidi ya shilingi 40,000/=. Swali linakuja: fedha hizi ni za nini hasa? Je, hizi si dalili za ufisadi wa wazi?

Soma Pia: Wajawazito wanalipishwa, risiti hawapewi katika Idara ya Afya Mpanda Manispaa Mkoani Katavi

Kuhusu sindano ya pepopunda, katika vituo vingi vya afya na zahanati hutolewa bure. Hata hivyo, katika Kituo cha Afya Bunju, wanatoza shilingi 12,000/= kwa sindano moja, wakati mama mjamzito anatakiwa kuchomwa sindano mbili, sawa na shilingi 24,000/=.

Mbaya zaidi hata malipo hayafanyiki kwa Control Number unawapa cash, halafu wanakupa risiti ya mchongo tu!

Hadi sasa, katika kliniki nne tu, tayari nimetumia zaidi ya shilingi 300000/=. Hii ni gharama kubwa sana kwa mwananchi wa kawaida.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba ukihoji au kuuliza maelezo kuhusu gharama hizi, wahudumu wanakuwa wakali na wakati mwingine hutishia kutokutoa huduma.

Ni rai yangu kwa mamlaka husika kuacha kukaa ofisini na kufuatilia kwa karibu hali halisi iliyopo katika Kituo cha Afya Bunju, ili kuondoa huu upigaji unaowaumiza wananchi.
 
Hii Nchi Uholela Umezidi Sana
UUmepewa. Risiti Ama
 
Back
Top Bottom