Kitumbua

Wa kijiji naingia
Na jibu nawapatia
Funza alichosifia
Hakika nakikandia
Kitumbua si Sambusa!

Utamu wa kitumbua
Ni hamira kutumua
Na sukari mwaijua
Na joto la kuumua
Kitumbua si sambusa!

Kwanza hakina nyama
Kitumbua lele mama
Hadi kiive ni noma
Wangoja washika tama
Kitumbua si sambusa!

Kwanza uoshe mchele
Ungoje kama milele
Usubiri kwa machale
Usage mwembaba vile
Kitumbua si sambusa!

Utafute cha kupikia
Chenye mashimo mamia
Kimoja hutotumia
Hakika nawaambia
Kitumbua si sambusa!

Sambusa utamu wake
Vilivyomo ndani yake
Ladha ni ya peke yake
Ukila uweweseke
Kitumbua si sambusa!

Kwanza kina pembetatu
Ni mtego mara tatu
Hata wenye roho kwatu
Wafakama kama fyatu
Kitumbua si sambusa!

Ikiwekwa pilipili,
Sambusa iko kwa mbali
Na vitunguu kwa dili
Haruku mpaka kwa Juli!
Kitumbua si sambusa!

Hakuna kama sambusa
Ninacheza na Nzawisa
Na ngoma za kinyakyusa
Hata ile Pase posa!
Kitumbua si sambusa!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti Ya Kijiji)
 
Dah kulaleki...Mwanakijiji wewe kiboko...yaani umeshuka hizi beti toka kichwani au uliliona hili shairi tokea mwanzo ukaenda nyumbani kulitungia majibu?

Anyway, I salute mkuu.
 
Dah kulaleki...Mwanakijiji wewe kiboko...yaani umeshuka hizi beti toka kichwani au uliliona hili shairi tokea mwanzo ukaenda nyumbani kulitungia majibu?

Anyway, I salute mkuu.

hapana.. nimeona kule jamaa aliponishtua kuna hili shairi ndio nikaingia kulijibu.. unajua NN kama vile mtu mwingine anavyowaza effortlessly juu ya mambo mbalimbali, ndivyo kwangu (labda na wengine) mistari huwa inashuka.. kwa mfano sasa hivi kichwani kuna shairi linasema "She Kissed Me Anyway".. na linacheza tangu jana.. sasa nikianza kuliandika litatiririka tu..
 
Heheheheheee....na wewe bana....eti "She Kissed Me Anyway".....haya bana. Nalisubiri hilo nalo nione kama litanifaa na mimi...Lol
 
Kuna vitumbua vingine bwana,vyahitaji makini katika ulaji waweza kukuta vimetengenezwa kwa unga wa kupandikiza.
 
sambusa zinakifu, nyingi zina uchafu
zinapikwa kwa rafu, kipato kijidurufu
zimepunjwa minofu, ukiziona dhoofu
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

Bora kusifu andazi, lipikwalo kwa uwazi
Ndani latiwa nazi, ladha kuipalizi
Ulishawekwa uwazi, Kitumbua si andazi
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

Ukisema cha Mchanga, Utakuwa na kilanga
kosa la mkaanga, hata sambusa unangwa
Kitumbua kinakonga, waweza hata kuonga
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

Sambusa kwa pilipili, mtoto katu haili
Na kusema ukweli, kitumbua ndio dili
Ukipata tu viwili, njaa inajighaili
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua

(c) Funzadume (Soli ya Mbingu) mwana wa washawasha 2010
 
Back
Top Bottom