Kituko JNIA mgahawani: Immigration hii si sawa!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
17,589
Reaction score
28,567
Nasafiri kwenda Mwanza flight FN 141 kuelekea Mwanza.
Kabla ya kupanda ndege naamua kupata kipasha moto, kahawa na keki, kwa kiswahili safi kabisa.

Namuuliza mhudumu kaunta aliyevaa shati bkuu, tai na kapendeza, muasia.

Cha kushangaza ananiuliza "what sir?"
Nashangaa, narudia tena kwa kiswahili.
Ajabu jamaa anasena"I dont understand sir"
Namuuliza "how did you get here, and where are you from"
Ananijibu "India sir"
Immigration, mtu asiyejua hata lugha ya kiswahili anafanya nini hapo?
Na ana kibali cha kazi au?
 
Kuna kitu kingine mkuu chakula pale wana tu uzia sawa Na wa zungu wakati kwengine raiya wa nyumbani wana punguzo kubwa mno , huwezi nunua chakula sawa Na mgeni hiyo ipo kwetu tu ! Tena kwa usd!!

Wapi kwingine uliona migahawa ya airport wana bei mbili za raia na wageni ? Iwe kwa dola yen pound euro au shillingi?
 
Bi kairuki kimyaaa mikwala alieka week mbili za mwanzo tu
 
Sasa kosa ni lugha, ok.

Ila waakiweka wazawa nao washindwa na kuharibu biashara.

Wewe kwenda kusema sijui achekiwe ni ubaguzi tu. kwani mtu kutokujua lugha ndio hana kibali cha kuwepo nchini? Siku nyingine jibadili uwe detective uulize maswali hapo hapo
 
Wapi kwingine uliona migahawa ya airport wana bei mbili za raia na wageni ? Iwe kwa dola yen pound euro au shillingi?

Naam naomba niongezee wanawezaje kutofautisha raia.wa nchi wa chi moja na nyingine kama kigezo ni utaifa, imagine pale Jomo Kenyata Int. Airport wanawezaje kutoautisha masai wa Namanga upande wa Tz na yule wa Namanga Kny wanaosafiri kwenda Hispania
 
Kuna kitu kingine mkuu chakula pale wana tu uzia sawa Na wa zungu wakati kwengine raiya wa nyumbani wana punguzo kubwa mno , huwezi nunua chakula sawa Na mgeni hiyo ipo kwetu tu ! Tena kwa usd!!

Wapi huko wanauza chakula kwa bei ya kubagua kama wewe ni raia au la?
 
Tutaona na kusikia mengi awamu hii, ngoja tunyooshwe huenda tutajifunza kitu
 
Nasafiri kwenda Mwanza flight FN 141 kuelekea Mwanza.
Kabla ya kupanda ndege naamua kupata kipasha moto, kahawa na keki, kwa kiswahili safi kabisa.

Namuuliza mhudumu kaunta aliyevaa shati bkuu, tai na kapendeza, muasia.

Cha kushangaza ananiuliza "what sir?"
Nashangaa, narudia tena kwa kiswahili.
Ajabu jamaa anasena"I dont understand sir"
Namuuliza "how did you get here, and where are you from"
Ananijibu "India sir"
Immigration, mtu asiyejua hata lugha ya kiswahili anafanya nini hapo?
Na ana kibali cha kazi au?

Acha kelele za kishamba. Kwani wewe hufahamu Kiingereza. Isitoshe inaitwa Julius Nyerere INTERNATIONAL Airport. Ukiagiza chai na andazi kwa Kihindi, Kiswahili au Kiingereza ladha ni ileile.
 
Wapumbavu ndio waliwao!
Nafikiri hata kinachoongelewa hapa mantiki yake imekupitia kwa mbali sana.
 
Nenda India katafute kazi, sina uhakika kama utakaribishwa, sembuse kupata kazi.
Nchi yetu sijui wanatumia sheria za wapi? Wachina kibao kariakoo wanaletana tu.... Kazi ambazo mtanzania alishia std 7 anaweza fanya wao wanaleta wakwao. Sasa faida za uwekezaji nini kama wazawa hawafaidiki? .......nenda kanunue bidhaa kariakoo... Mchina ndo porter, ndo store keeper,ndo muhudumu na cashier... Ukimkuta mmbongo mmoja labda tena kazi yake kufuta vumbi tu.
Acha kelele za kishamba. Kwani wewe hufahamu Kiingereza. Isitoshe inaitwa Julius Nyerere INTERNATIONAL Airport. Ukiagiza chai na andazi kwa Kihindi, Kiswahili au Kiingereza ladha ni ileile.
Sasa na wewe hata tu waiter na waitres au receptionist watokee nje?!?!
 
Nchi yetu sijui wanatumia sheria za wapi? Wachina kibao kariakoo wanaletana tu.... Kazi ambazo mtanzania alishia std 7 anaweza fanya wao wanaleta wakwao. Sasa faida za uwekezaji nini kama wazawa hawafaidiki? .......nenda kanunue bidhaa kariakoo... Mchina ndo porter, ndo store keeper,ndo muhudumu na cashier... Ukimkuta mmbongo mmoja labda tena kazi yake kufuta vumbi tu.

Sasa na wewe hata tu waiter na waitres au receptionist watokee nje?!?!
Ndiyo. Ni International Airport. Wapo Watanzania wengi wanafanya kazi za umachinga Uchina.
 
Back
Top Bottom