Kituko:Gavana ataka benki zikopeshe wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kituko:Gavana ataka benki zikopeshe wanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Sep 4, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,508
  Likes Received: 19,922
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"] Gavana ataka benki zikopeshe wanafunzi[/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 03 September 2011 20:46[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Fredy Azzah
  GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndulu, amesema Serikali haiwezi kutoa mikopo ya kuwatosheleza wanafunzi wote, badala yake mabenki pamoja na asasi zisizo za kiserikali lazima ziingie katika utoaji wa mikopo hiyo.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana alipofungua Maadhimisho ya Miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), yatakayo adhimishwa na Chuo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii kwa mwezi mmoja, Profesa Ndulu alisema kwa kufanya hivyo wanafunzi wanaohitaji mikopo hiyo wataipata.

  "Serikali hata siku moja haiwezi kutoa mikopo ya kuwatosheleza wanafunzi wote, Serikali ina mambo mengi jamani, lazima taasisi kama za kibenki, mashirika binafsi na asasi nyingine ziingie katika kuwapa wanafunzi mikopo," alisema Profesa Ndulu na kuongeza.

  "Benki kuu inasomesha baadhi ya watu katika shahada za uzamili, kwa sasa tunaanzisha mfuko ambao utakuwa unawasaidia wanafunzi wa kike ambao wanasoma masomo ya sayansi na hisabati kwa shahada za awali."

  Kuhusu maendeleo ya chuo hicho, alisema kuwa lazima elimu ubora wa elimu inayotolewa na chuo hicho udumishwe.
  Alieleza pia kwamba, Serikali na wadau wengine wa elimu wanapaswa kuangalia namna ya kukisaidia chuo hicho kupata fedha kwa ajili ya kukarabati na kujenga majengo mengine.

  Kuhusu kuendelea kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania, Profesa ndulu alisema njia pekee ya kudhibiti hali hiyo ni kuhakikisha nchi inakuwa na fedha za kigeni za kutosha.

  "Tusiseme tu kwamba shilingi inashuka, tukumbuke pia wakati mwingine inapanda, lakini njia ya kufanya shilingi yetu iwe imara zaidi ni kuhakikisha tunakuwa na hifadhi ya kutosha ya fedha za kigeni," alisema Profesa Ndulu.

  Naye Makamu Mkuu wa UDSM Profesa Rwekaza Mukandala, alisema chuo hicho kilianzishwa Oktoba 25 mwaka 1961 miezi miwili kabla ya Tanzania kupata uhuru wake[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  my take:
  Ushauri wa benki kukopesha wanafunzi katika mazingira yaliyopo sasa HAUFAI hata kidogo na Gavana alitakiwa kutumia BUSARA na WELEDI kutoa ushauri huo. Mfano leo hii mwanafunzi akikopa sh million 10 ili kugharamia shahada yake ya Kwanza itakayomchukua miaka minne na apewe grace period ya miaka miwili baada ya kumaliza chuo ili aanze kulipa mkopo wake mtu huyu atatakiwa kulipa wastani wa sh 600,000 kila mwezi kwa miaka 10.

  Hii ni km mkopo huo umepatikana kwa riba ya sasa 20% na mkopaji anapewa mia kumi ya kulipa baada ya kumaliza shule na kuanza kulipa. Nilitegemea kuona Weledi wa kiasi fulani kutoka kwa Gavana wakati anatoa mapendekezo yenye athari kubwa za kijamii. Hivi graduate atakiwe kulipa laki 6 kila mwezi ataishije, kwanza wengine hawapati mishahara hiyo. Niseme tu Ushauri wa Gavana ni wa wa kis**
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,508
  Likes Received: 19,922
  Trophy Points: 280
  hivi kweli huyu si anataka mshahara wako wote uishie kwenye kuilipa benki? masaburi haya jamani.....
  si kasoma bure huyu?
   
 3. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Si ndo hapo sasa, utawezana wapi na interest za ma Bank kama sio kuwataka watu mishahara yote ije iishie Bank???
  Watu waliosoma bure zamani wana matatizo sana, wanapenda kuona vijana wanateseka na maisha huku wao wakiishi kama wafalme.
   
 4. D

  Derimto JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani watu wamekurupuka ila kwa uzoefu wangu huyu jamaa anachokisema kinawezekana kama hakutakuwa na ubabaishaji katika mfumo wake wa ukopaji na urejeshaji na itaondoa matumizi yasiyo rasmi kwa wanavyuo maana watajua ni mikopo ya kulipa na siyo msaada kama wanavyochukulia sasa ambapo pia kuna ubabaishaji mwingi ili iweze kutoka.
   
 5. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  hata kwa shida zako ukikubaliana na io interest, benki wataanzia wap?risk sn, ukidisco,io ajira utata mtupu,may b kama watakuajir

  never.benki zinakimbilia bonds za serkali coz les risk
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu gavana kila siku nikimuona naona kama vile ni mgomjwa na ndio maana hata ushauri wake mara nyingi una utata!! Benki ni taasisi inayofanya biashara ya kukopesha fedha ili ipate faida; sasa hao wanafunzi ambao serikali yao imeshindwa kuwakopesha benki itawakopesha kwa kutumia collateral gani? Hizo benki anazosema ziwakopeshe wanafunzi ni benki zipi hizo?

  Problem ya mikopo ya wanafunzi iko kwenye utendaji/usimamiaji na sio upatikanaji wa fedha za kuwakopesha kwani kama utaratibu wa marejesho ungekuwa makini wanafunzi wengi wangefaidika. Tumezoea kuwa kila fedha itolewawayo inakuwa kama mabilioni ya Kikwete; we are politicising everything ndio maana hata gavana wa benki anakuwa mwanasiasa pia!!
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Naona wachangiaji wengi wanapenda vya bure. Mawazo ya gavana ni sahihi- mabenki na taasis nyingine za fedha zikiamua kukopesha zitaweka special scheme inayoendana na maisha ya mwanafunzi. Jiulize wale waliokopa wanalipa kiasi gani kwa mwezi?

  Je, kunaaliyelalamika kuwa anakatwa kiasi kikubwa kwa mwezi?. Mimi namuunga mkono gavana kwani kuna taasisi nyingi za fedha ambazo zimekalia mamiliono ya alipokodi, mf:NHIF, NCCF,PSPF, LAPF etcetera.
   
 8. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nani kakwambia ni msaada? Wewe ulipewa mkopo na haujerejesha? Sisi wengine tunarejesha na tulikopeshwa wakati mfumo huu unaanza tu.
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mkuu welcome to the USA policies.
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,088
  Trophy Points: 280
  Ama kweli aliyeshiba hamjuhi mwenye njaa...hawa wauni wao walisoma bure leo hawataki hata sie tusome kwa pesa ya mkopo wa serikali..wanataka wafanyabiashara ndo wawe watoaji wa mikopo ili na yeye aanzishe benki yake ili wachukue pesa yetu kwa riba kubwa wazidi kutunyonya maskini

  Yes,nachoamini ni kwamba hili likija matajiri wote wataanzisha mabenki na wote watatoa mikopo kwa riba watakayokubaliana wao kwa masrahi yao,mwezi huu mie nimekatwa 8% nahisi kuwa masikini je inakuwaje kama wanaweka na riba?
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,508
  Likes Received: 19,922
  Trophy Points: 280
  inawezekana huyu jamaa ana benki yake tayari anataka kuipa shavu la kukopesha wanafunzi ..ndio yale yale ya Nimrod Mkono...hawa jamaa hawafai kabisa ..wanaweza kunywa uji wa mgonjwa ..cio watu wazuri kabisa hawa..benki gani amabayo inaweza au itamkopesha mwanafunzi kwa vigezo vinavyoeleweka? hio itakuwa benk au bodi
   
Loading...