Ta Kamugisha
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 3,550
- 2,200
Kuna sehemu kwenye kenji ya nyumba nilikuwa ndo naweka ndom, nyumba haikuwa na ceiling board.
Siku ya siku niko form II dingi akaja chumbani kwangu sikumbuki tulikuwa tunajadili nini, mara paaa! Pakti ikadondoka chini. Ile aibu huwa nikikumbuka nacheka mwenyewe...
Mpaka leo sielewi ilikuwaje zile ndude zikadondoka zenyewe tu, halafu zimechagua siku hiyo mdingi yuko room.
Ilikuwa pasaka,mwaka siukumbuki, ila nakumbuka nilipewa assignment nihakikishe bata wa sikukuu kaaaaivaa vizuri, mama akitoka kanisani afanye finalization.
Kweli, mheshimiwaa bata akaiva vizuri, nikamuipua.
Kosa nililolifanya ni kujaribu kuonja kipande kimoja.
Nikajikuta nimeongeza kipande cha pili.
Kuja kutahamaki, vimebaki vipatio na kile kiwowowo cha bata na mgongo.
Mama katoka kanisani kaja na mchungaji na mwinjilisti.
Pilau ni la kupasha moto tu, kimbembe kwenye mboga.
Siku hiyo nilikuwa fimbo za kutosha, kibaya zaidi hata sikuyasikia maumivu yake.
Pole sana,Asante ila ndio vituko vya utotoni, usiombe ukutane na barafu linaunguza balaa
Kipindi cho ndo na Hamu ya Kujazia kuvutia Mabinti.
Nikanunua Nondo yangu, Baada ya Kumaliza Shule ikawa kama Dozi ya Malaria kutwa mara tatu yaani hata Ukiniambia ninyanyue ndoo ya Maji nilikuwa Siwezi...
Kuna Siku nadhani ni jpil na Ilikuwa sikukuu wazee wakaniacha mwnyw nyumban wakaniachia Bajeti niandae Chakula, Siku hiyo nilikipika mapema tu saa 3 asbh msosi ulikuwa teyari na Mboga...
Aisee sitasahau Nilikuwa nimepika Kilo1 na Robo.. kila nikipasha nasikia Njaa, Nilikigonga chote nikabakiza Kama robo roba yake tena kama vijiko 10 tu...
Walivyorudi nilikanusha kupika chakula kingi lakn Sufuria liliniumbua..
T
Kesho yake naamka asbh nikapashe kama kawaida yangu, Nondo siioni baad ya Kufatilia sana nikaja kugundua Bi mkubwa ndiye aliyekitorosha, Nikaamuulz akakubali, akasema alikitupa Barabarani nilijiulz maswal mengi na uzito ule alikibebaje mpk barabarani..
Baada ya Miaka 3 toka siku ile, tupo kwny hekaheka za Kuweka Pervis chini, nikaja Kugundua Kumbe bi Mkubwa alikizika Chini ya Ardhi... Daaah nilicheka sana...
Bahati mbaya baada ya wiki alihazima jamaa yangu mmj akapashie Maghetoni kwake, Ana ndg yake anaokotota makopo na ni mvutaji mzuri wa bhangi... Akaamka asbh na Arosto cjui ndo zimemkolea akachukua nyundo kubwa Akavunja zege akachukua chuma akaenda kuuza kama chuma chakavu..
Mpka leo, nikiwaona wavutaji nawasalimia "SHKMOONI" Maana wanawez wakuvunja viungo wakauze Nguo....
Sent using Jamii Forums mobile app
Sitasaau siku niliagizwa sukari nikaenda mda wa kurudi nikapoteza mia mbili kwenye chenchi niliyokua nimerudishiwa
Ilikua ni kama 2007 ivi kama sijasaau
Baada ya kupoteza nikaenda nyumbani nikaulizwa mbona chenchi ni pungufu nikajichanganya nikasema sijarudishiwa nikaambiwa rudi kachukie
Nikaamua kurudi kwenda kuisaka nilipopotezea...niliangaika sana pale kuitafuta lakini sikuipata
Kosa nililokua nimelifanya baada ya kusema sijarudishiwa chenchi nikaingia chumba cha maza fasta nikachomoka na mia mbili
Baada ya kwenda kuitafuta na kuikosa nikafanya kureplace na ile niliyochomoa kwa maza nikarudi zangu nikakabidhi chenchi kamili
Kisanga kilikuja baada ya kuambiwa kachukue mia mbili pale chumbani ukalete kiberiti
Nikaenda uku najua fika mia mbili nilishaichukua nakuanza kuangaika humo ndani nikarudi nakusema sijaiona
Maza anajua kabisa mia mbili aliweka apo mda sio mrefu na akajua kuna mda niliingia chumbani kwake nilipoagizwa dukani
Asee wala akunisemesha...usiku ukapita ikawa mchana nikala ugali wangu vizuri nikamaliza kisha nikaitwa na mzee
Asee kumbe mzee alishapewa issue nzima na alishaandaa bakora kazaa
Nilichezea kichapo ambacho sitakaa nikisaau na cha kushangaza siri ya jeshi aikutolewa kitu ambacho nashangaa mpaka leo ningesema tu nimepoteza wala isingekua kesi maana maza alikuwa mwelewa tu
Sent using Jamii Forums mobile app
HahahahaSitasaau siku niliagizwa sukari nikaenda mda wa kurudi nikapoteza mia mbili kwenye chenchi niliyokua nimerudishiwa