Kituko cha utotoni ambacho uwezi sahau mpaka leo

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,536
2,187
Enzi za shule ya Msingi, nilikuwa napenda sana michezo mimi na mdogo wangu, ingawa mzee alikuwa hapendi tuwe tunachelewa kutoka kucheza mpira maana alikuwa Mjeda JWTZ

Ila tulikuwa na tabia ya kuiba Ice cream, kwa jina maarufu ziliitwa "ashikilimu" nadhani wote mnazifaham. Tulikuwa tunaziiba tulipokuwa tunataka kwenda kuoga maana friji ilikuwa inakaa kwa mfanyakazi "House Girl"

Tulipigwa marufuku kula Ashikilimu kwa sababu ya kifua, si unajua utoto ukikatazwa kitu ndio kwanza unatengeneza njia ya kukifanya ulichokatazwa

Sasa basi, siku za mwizi ni 40, maana ilikuwa ni desturi yetu kuiba ashikilimu kila siku na kwenda kuzilia bafuni, hapa naongelea miaka 90's. Maana tulipendelea kuogea bafu la nje ili tujinafasi na ashikilimu zetu, ukiiba nyingi unakula nyingi.

Siku hiyo tumezama chumba cha house girl kumbe Mjeshi yupo dirishani anatuchora maana dirisha lilikuwa halijafungwa na sisi tulimuacha nje ya geti anaosha gari lake, tukachukua zile ashikilimu tukazibana na taulo kwenye tumbo au kiunoni kila mmoja tukaiba tatu tatu, ukishaziiba unazifunga vzr kiunoni na kutoka speed mpaka bafuni.

Ukishaziweka kiunoni unatakiwa utoke nduki ya hatari mpaka bafuni maana zinachoma kwa ubaridi si unajua barafu inavyochoma!!!

Kumbe mjeshi anatuchora tu dirisha maana pazia hatukuzifunga, ile tunatoka nje kwa speed ya umeme ili tuwai bafuni, mara mjeshi akatusimamisha.....kah....

Dah ilikuwa hatari, akaaza kutuuliza maswali madogo madogo....kwanini mmechelewa kuoga?....kwanini mmechelewa toka uwanjani? .....shuleni mmesoma nini? Yaani alituhoji maswali kama dakika 10......

Aisee uku sisi tunacheza mguu pande...mguu sawa maana barafu zilikuwa zinaunguza balaaa, uzalendo ukatushinda aisee tukazitupa chini.....

Mjeshi sasa....akasema hii ndio nilitaka kuona maana nilijua zitawaunguza tu.....zilituchoma mpaka tukauza Ramani ya vita kwa Mjeshi....

Babaaaake tulikula mboko za hatari, maana nyuma kulikuwa na mnazi, alitufunga kwenye mnazi na tukala mboko za maana, maana hata sijui tulikula mboko ngapi, na tukapewa adhabu ya kulala bila kula...ila tulichezea kichapo cha mbwa koko

Ila house girl alicheza kama pele, aliposikia tunapewa adhabu ya kulala bila kula, alipakua ubwabwa fasta , sahani mbili za ubwabwa akaenda kuziweka chini ya kitanda....tukafunguliwa kwenye mnazi maana alitaka tulale pale pale kwenye mnazi, Bi mkubwa akatutetea sana, tukaenda kulala zetu ndani, mara House girl akatugongea kwenye dirisha....Ta kamugisha ebu angalieni uvunguni mwa Kitanda..

Mara paaa wali ndondo, tuliula na kucheka sana .....na kumshukuru house Girl wetu, kuànzia siku hiyo atukuiba tena Ashikilimu, maana mboko za mjeshi zilikuwa matata sana aisee....si mnazijua mboka za maafande!!!

Hiki kisa mpaka leo siwezi kukisahau maana Ashikilimu zilituchoma mpaka tukauza Ramani ya vita kwa Mjeshi wa JWTZ
 
Ilikuwa pasaka,mwaka siukumbuki, ila nakumbuka nilipewa assignment nihakikishe bata wa sikukuu kaaaaivaa vizuri, mama akitoka kanisani afanye finalization.
Kweli, mheshimiwaa bata akaiva vizuri, nikamuipua.
Kosa nililolifanya ni kujaribu kuonja kipande kimoja.
Nikajikuta nimeongeza kipande cha pili.
Kuja kutahamaki, vimebaki vipatio na kile kiwowowo cha bata na mgongo.
Mama katoka kanisani kaja na mchungaji na mwinjilisti.
Pilau ni la kupasha moto tu, kimbembe kwenye mboga.
Siku hiyo nilikuwa fimbo za kutosha, kibaya zaidi hata sikuyasikia maumivu yake.
 
Kuna sehemu kwenye kenji ya nyumba nilikuwa ndo naweka ndom, nyumba haikuwa na ceiling board.

Siku ya siku niko form II dingi akaja chumbani kwangu sikumbuki tulikuwa tunajadili nini, mara paaa! Pakti ikadondoka chini. Ile aibu huwa nikikumbuka nacheka mwenyewe...

Mpaka leo sielewi ilikuwaje zile ndude zikadondoka zenyewe tu, halafu zimechagua siku hiyo mdingi yuko room.

Ha ha ha ha umenivunja mbavu kah ilikuwa balaa
 
Ilikuwa pasaka,mwaka siukumbuki, ila nakumbuka nilipewa assignment nihakikishe bata wa sikukuu kaaaaivaa vizuri, mama akitoka kanisani afanye finalization.
Kweli, mheshimiwaa bata akaiva vizuri, nikamuipua.
Kosa nililolifanya ni kujaribu kuonja kipande kimoja.
Nikajikuta nimeongeza kipande cha pili.
Kuja kutahamaki, vimebaki vipatio na kile kiwowowo cha bata na mgongo.
Mama katoka kanisani kaja na mchungaji na mwinjilisti.
Pilau ni la kupasha moto tu, kimbembe kwenye mboga.
Siku hiyo nilikuwa fimbo za kutosha, kibaya zaidi hata sikuyasikia maumivu yake.

Ha ha ha chovya chovya umaliza buyu la asali
 
Nakumbuka nilikua chekechea tu maeneo ya ubungo pale kuna kidemu kizuri nilikua nakipenda sanaa nkaona isiwe taabu acha nkirud home niandike barua kisha tukitoka class nimpe kesho yake!

Nkakaa zangu jiran na mlango nkaanza kuandika barua,mara paap mama mdogo akapita akauliza unaandika nini kule kupaniki kuwa picha limeungua nkajkuta nachana ile karatasi!

Mama mdogo akamwita mama chaap nkalibugia mdomoni mama akanishika mikono na mama mdogo akawa ananitekenya huku kanishika taya lahaulaaa!!! Wakaipara barua ile!!

Kipigo nilichopata hiyo siku sitokuja sahau!!!
 
Kipindi cho ndo na Hamu ya Kujazia kuvutia Mabinti.
Nikanunua Nondo yangu, Baada ya Kumaliza Shule ikawa kama Dozi ya Malaria kutwa mara tatu yaani hata Ukiniambia ninyanyue ndoo ya Maji nilikuwa Siwezi...
Kuna Siku nadhani ni jpil na Ilikuwa sikukuu wazee wakaniacha mwnyw nyumban wakaniachia Bajeti niandae Chakula, Siku hiyo nilikipika mapema tu saa 3 asbh msosi ulikuwa teyari na Mboga...
Aisee sitasahau Nilikuwa nimepika Kilo1 na Robo.. kila nikipasha nasikia Njaa, Nilikigonga chote nikabakiza Kama robo roba yake tena kama vijiko 10 tu...
Walivyorudi nilikanusha kupika chakula kingi lakn Sufuria liliniumbua..
T
Kesho yake naamka asbh nikapashe kama kawaida yangu, Nondo siioni baad ya Kufatilia sana nikaja kugundua Bi mkubwa ndiye aliyekitorosha, Nikaamuulz akakubali, akasema alikitupa Barabarani nilijiulz maswal mengi na uzito ule alikibebaje mpk barabarani..
Baada ya Miaka 3 toka siku ile, tupo kwny hekaheka za Kuweka Pervis chini, nikaja Kugundua Kumbe bi Mkubwa alikizika Chini ya Ardhi... Daaah nilicheka sana...
Bahati mbaya baada ya wiki alihazima jamaa yangu mmj akapashie Maghetoni kwake, Ana ndg yake anaokotota makopo na ni mvutaji mzuri wa bhangi... Akaamka asbh na Arosto cjui ndo zimemkolea akachukua nyundo kubwa Akavunja zege akachukua chuma akaenda kuuza kama chuma chakavu..
Mpka leo, nikiwaona wavutaji nawasalimia "SHKMOONI" Maana wanawez wakuvunja viungo wakauze Nguo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahahahaha hii kali
Amevunja zege ili ibaki nondo peke yake akauze chuma chakavu!!!!

Usipoyapangia maisha nini cha kufanya yenyewe yatakupangia wewe nini cha kufanya.
 
Sitasaau siku niliagizwa sukari nikaenda mda wa kurudi nikapoteza mia mbili kwenye chenchi niliyokua nimerudishiwa

Ilikua ni kama 2007 ivi kama sijasaau

Baada ya kupoteza nikaenda nyumbani nikaulizwa mbona chenchi ni pungufu nikajichanganya nikasema sijarudishiwa nikaambiwa rudi kachukie

Nikaamua kurudi kwenda kuisaka nilipopotezea...niliangaika sana pale kuitafuta lakini sikuipata

Kosa nililokua nimelifanya baada ya kusema sijarudishiwa chenchi nikaingia chumba cha maza fasta nikachomoka na mia mbili

Baada ya kwenda kuitafuta na kuikosa nikafanya kureplace na ile niliyochomoa kwa maza nikarudi zangu nikakabidhi chenchi kamili

Kisanga kilikuja baada ya kuambiwa kachukue mia mbili pale chumbani ukalete kiberiti

Nikaenda uku najua fika mia mbili nilishaichukua nakuanza kuangaika humo ndani nikarudi nakusema sijaiona

Maza anajua kabisa mia mbili aliweka apo mda sio mrefu na akajua kuna mda niliingia chumbani kwake nilipoagizwa dukani

Asee wala akunisemesha...usiku ukapita ikawa mchana nikala ugali wangu vizuri nikamaliza kisha nikaitwa na mzee

Asee kumbe mzee alishapewa issue nzima na alishaandaa bakora kazaa

Nilichezea kichapo ambacho sitakaa nikisaau na cha kushangaza siri ya jeshi aikutolewa kitu ambacho nashangaa mpaka leo ningesema tu nimepoteza wala isingekua kesi maana maza alikuwa mwelewa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi cho ndo na Hamu ya Kujazia kuvutia Mabinti.
Nikanunua Nondo yangu, Baada ya Kumaliza Shule ikawa kama Dozi ya Malaria kutwa mara tatu yaani hata Ukiniambia ninyanyue ndoo ya Maji nilikuwa Siwezi...
Kuna Siku nadhani ni jpil na Ilikuwa sikukuu wazee wakaniacha mwnyw nyumban wakaniachia Bajeti niandae Chakula, Siku hiyo nilikipika mapema tu saa 3 asbh msosi ulikuwa teyari na Mboga...
Aisee sitasahau Nilikuwa nimepika Kilo1 na Robo.. kila nikipasha nasikia Njaa, Nilikigonga chote nikabakiza Kama robo roba yake tena kama vijiko 10 tu...
Walivyorudi nilikanusha kupika chakula kingi lakn Sufuria liliniumbua..
T
Kesho yake naamka asbh nikapashe kama kawaida yangu, Nondo siioni baad ya Kufatilia sana nikaja kugundua Bi mkubwa ndiye aliyekitorosha, Nikaamuulz akakubali, akasema alikitupa Barabarani nilijiulz maswal mengi na uzito ule alikibebaje mpk barabarani..
Baada ya Miaka 3 toka siku ile, tupo kwny hekaheka za Kuweka Pervis chini, nikaja Kugundua Kumbe bi Mkubwa alikizika Chini ya Ardhi... Daaah nilicheka sana...
Bahati mbaya baada ya wiki alihazima jamaa yangu mmj akapashie Maghetoni kwake, Ana ndg yake anaokotota makopo na ni mvutaji mzuri wa bhangi... Akaamka asbh na Arosto cjui ndo zimemkolea akachukua nyundo kubwa Akavunja zege akachukua chuma akaenda kuuza kama chuma chakavu..
Mpka leo, nikiwaona wavutaji nawasalimia "SHKMOONI" Maana wanawez wakuvunja viungo wakauze Nguo....

Sent using Jamii Forums mobile app

Ha ha ha hii kali ya mvuta bangi kauza nondo!!!
 
Sitasaau siku niliagizwa sukari nikaenda mda wa kurudi nikapoteza mia mbili kwenye chenchi niliyokua nimerudishiwa

Ilikua ni kama 2007 ivi kama sijasaau

Baada ya kupoteza nikaenda nyumbani nikaulizwa mbona chenchi ni pungufu nikajichanganya nikasema sijarudishiwa nikaambiwa rudi kachukie

Nikaamua kurudi kwenda kuisaka nilipopotezea...niliangaika sana pale kuitafuta lakini sikuipata

Kosa nililokua nimelifanya baada ya kusema sijarudishiwa chenchi nikaingia chumba cha maza fasta nikachomoka na mia mbili

Baada ya kwenda kuitafuta na kuikosa nikafanya kureplace na ile niliyochomoa kwa maza nikarudi zangu nikakabidhi chenchi kamili

Kisanga kilikuja baada ya kuambiwa kachukue mia mbili pale chumbani ukalete kiberiti

Nikaenda uku najua fika mia mbili nilishaichukua nakuanza kuangaika humo ndani nikarudi nakusema sijaiona

Maza anajua kabisa mia mbili aliweka apo mda sio mrefu na akajua kuna mda niliingia chumbani kwake nilipoagizwa dukani

Asee wala akunisemesha...usiku ukapita ikawa mchana nikala ugali wangu vizuri nikamaliza kisha nikaitwa na mzee

Asee kumbe mzee alishapewa issue nzima na alishaandaa bakora kazaa

Nilichezea kichapo ambacho sitakaa nikisaau na cha kushangaza siri ya jeshi aikutolewa kitu ambacho nashangaa mpaka leo ningesema tu nimepoteza wala isingekua kesi maana maza alikuwa mwelewa tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Ha ha ha ha hii balaa
 
Hahahaha
 
Dah!
Mmenikumbusha mkasa wa kutafuna mihogo mikavu (udaga) ya Msengi,
Yule jamaa sitakaa nisahu siku hiyo.
Maana tulikua karibia nusu ya watoto wote wa kijiji, tunacheza mpira mara mvua ikaanza kunyesha ikabidi tukajibanze kwenye kibaraza ambacho msengi aliacha mihogo yake alokua anauza na kwenda kula nyumbani, aisee tulikua tuishambulia mbuzi wakasome na vile ilikua mitamu.

Mara, "Hivyo hivyo mlivyo" kugeuka, Msengi huyo anapaki baiskeli yake na alikua anajulikana kwa ukorofi wake na kulikua na tetesi kuwa ni muumini wa kijamaika. Kwanza ni kusafisha mdomo hatujakaa sawa jamaa akaagiza fimbo, wana wakaanza kujikata kwa mbio, aisee jamaa aliunga na baadhi ya wana mpaka kijiji cha pili.
Hili ni moja ya matukio yanayodumu, hii ni late ya 90's

Similar Discussions

Back
Top Bottom