yani kwa akili ya kawaida anazani mwanamke kashobokea gari.....nadhani afwatilie ajue rafiki yake kama yuko salama mana matukio mengi siku hizi......wanawake wanahusishwa......
Kama hadithi yako ni kweli basi huyo mwenzako pamoja na kuishi huko alikoishi na kutembea kote huko, bado ni 'limbukeni' wa wanawake. Miaka hii huwezi tu kupakiza mtu ovyo kwenye gari yako. Hasa wanawake usiowajua. Wao ndo hutumiwa Sana kwenye maswala ya ujambazi.
Pia wadada bhana. Why are MOST women so cheap nowadays? Umeona gari tayari unalowana?..aaaah!!
Unamwacha rafiki yako anaingia kwenye mtego wa jambazi kirahisi hivo!
Matukio yote huwa yapangwa kwanza,hivyo ni ngumu kuona mtu na kujaribu kufanya tukio la uhalifu,ninachojua mwanamke kashobokea lifti.
Stori ni ya kweli kwa asilimia zote na imetokea leo,jamaa yangu ni mtu wa watu na mtu wa kujichanganya sana,kwa hiyo huwa hasiti kusaidia mtu lifti sio tu mwanamke,pia muda ulikwa unaruhusu kufanya hivyo na ukizingatia na lifti ya umbali mdogo sio long way drive.Zaidi ya yote matukio yote ya uhalifu kutekwa,kupewa sumu nk huwachukua muda mwingi wahalifu kuandaa na kufanikisha huwa hayatokei tu mara baada ya kuona mtu wasiyemjua.
sio wote tunaoshobokea vimagari wala hatunaga hiyo tabia ni baadhi tu wanakuwa na ulimbukeni wa vifaa hivyo
kwani kama uantaka gari si utafute kwa jasho lako sio kuparamia watu usiowajua besti
basi tu ni ulimbukeni unawasumbua baadhi ya wanawake wenzetu wakitulia na kutafuta watakuwa nayo kwani gari nini basi mpaka ushindwe kulinunua hata vitz lako?
hiyo ni lout na ulimbukeni tu
Mkuu unachokisema ni sahihi, hata kama siyo jambazi, wengi ni matapeli. Hapa juzi kati kama week mbili zimepita nilikuwa natoka zangu home naelekea kibaruani. Siku hiyo binti yangu alikataa kubanda school buss ikabidi nimpeleke mwenyewe shule. Njiani nikaombwa lift na mdada flani akakaa seat ya nyuma ambapo kulikuwa na laptop yangu. Nikamfikisha binti yangu shule mitaa ya Sanawari na kwa vile office zipo njiro, nilimshusha yale dada Sanawari, kosa kubwa nililolifanya ni kutomuangalia yule dada wakati anashuka. Kufika officine, lahauraaaaa, nimebakiwa na kibegi na charger tu, laptop hakuna. Siku hizi, sitoi lift kwa mtu nisomfaham.
Haya tumekusikia, au ulikua waona wivu kwa rafiki yako
sasa unadhani hawajapanga......muda wote wew unaongea na rafiki yako.....na wao walikuwa wanapanga mipango yao......yani kirahisi rahisi amwoche bwanaake kweupe pee......
Kimsingi rafiki yangu atakuwa ameamua kumsaidia kama lift,sina hakika kama yeye anawaza kitu kingine.Wanaume tumeumbiwa mioyo ya ukarimu.Ingekuwa wewe ungekataa kumpa lifti?
tofautisha huruma na udhaifu.
Mtu amekuja kula starehe na jamaa yake halafu anamwacha jamaa yake anakukimbilia unasema et huruma?!
Tena mbaya zaidi humfaham kabisa. Inamaana hyo sehem mwenye gari alikuwa peke yake?
Mazingira ya kumhurumia mtu yapo hatukatai kama vile
yuko barabaran amekosa usafir, anaumwa, yupo eneo hatarishi, nk.
Ukijifanya baba huruma hapo lazma ikuponze.
Babu yangu alikuwa ananiambia
"IPYANA IGOGI"
Naamini weekend inaenda poa.
Leo nikiwa katika hoteli fulani nikikutana na rafiki yangu katika mambo ya kazi,mimi nilitangulia kufika hotelini hapo kisha akafuata rafiki yangu aliyekuja na gari yake,tukazungumza mambo yetu wakati anataka kuondoka akatokea mwanamke mmoja akiyemuuliza rafiki yangu anaenda wapi? jamaa yangu akamjibu kuwa analelekea Ngaramtoni,yule mwanamke akakurupuka mbio na kushuka toka kwenye balcony ya hoteli hiyo na kumuacha mpenzi wake waliye kuwa wameketi wote wakipunga upepo.
Rafiki yangu alimsubiri ashuke na kuondoka naye,sasa najiuliza yule mwanamke kashobokea gari au ni kitu gani?
Nina uhakika wa asilimia zote kuwa hawajuani na rafiki yangu,maana naye alishangaa kuona mtu akiomba lifti kwa nguvu.
Hivi inakuwa wanawake wengi kuwa udhaifu kwenye magari??
Mchana mwema.!