Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Apr 22, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi'


  tropicanaoriginal.jpg


  BILA shaka unapoingia dukani au supermarket kununua juisi ya box, huwa unaamini kuwa iliyoandikwa ‘100% Puer Juice' huwa ni halisi na ndiyo bora. Kwa kukuongezea imani zaidi, watengenezaji wameweka na neno ‘No Sugar Added' au ‘No preservatives' (haikuongezwa sukari wala dawa)!

  Kuanzia leo elewa kwamba hayo ni maneno ya kibiashara tu, ukweli hauko hivyo! Umewahi kujiuliza kwa nini maboksi yote ya juisi hiyo yawe na ladha moja tu. Sote tunajua kwamba, kama ni juisi ya machungwa kwa mfano, ukila machungwa matano, yote hayawezi kuwa na ladha moja!


  Lakini kwa juisi za maboksi imewezekana kuwa na ladha moja kwa sababu za kikemia zinazofanywa kiwandani wakati wa kuhifadhi juisi hiyo ambayo huweza kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Hivyo siyo kweli kwamba unachokunywa ni asilimia 100 ‘pure'.

  NINI KINACHOTOKEA?
  Ni kweli kwamba ‘100% pure juice' hutokana na matunda halisi kama vile machungwa, mananasi, embe, n.k, lakini mchakato wake wa kukamua, kuhifadhi na hatimaye kumfikishia mlaji ndiyo wenye dosari za kiafya.

  Kinachofanyika baada ya tunda kukamuliwa ni kuhifadhi juisi yake kwenye matanki maalumu makubwa ya viwandani. Ili juisi hiyo iweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika, wanalazimika kuondoa hewa yake asilia ya oksijeni (mchakato unajulikana kitaalamu kama ‘deaeration'), kitendo ambacho huifanya juisi hiyo kupoteza ladha yake ya asili.

  NINI HUFANYIKA KUREJESHA LADHA YA MATUNDA?
  Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Food Renegade' wa nchini Marekani unaojishughulisha na masuala ya lishe na kuhimiza ulaji wa vyakula asilia, makampuni yanayozalisha juisi hukodisha makampuni yenye ujuzi wa kutengeneza ladha mbalimbali za matunda na manukato.

  Makampuni hayo husimamia utengenezaji wa maboksi ya kuhifadhia juisi ambayo huwekwa ladha na harufu ya matunda husika. Inaelezwa zaidi kuwa makampuni hayo ndiyo yanayotengeneza pia manukato (perfumes) maarufu duniani, kama vile Dior na Calvin Klein.

  Lakini cha kushangaza, virutubisho vinavyotumika kutengenezea ladha hiyo bandia haviorodheshwi kwenye boksi na wenyewe wanajitetea kwa kusema kuwa ladha hiyo haiwezi kuorodheshwa kama sehemu ya ‘ingredients' kwa sababu hutengenezwa kutokana na tunda lenyewe, ingawa wataalamu wengine wanadai utengenezaji wake huhusisha kemikali zingine ambazo siyo za asili.

  Mtaalamu mwingine kutoka Taasisi ya Sera ya Kilimo na Biashara nchini Marekani, Bi. Alissa Hamilton J. D (PhD), ameelezea kwa undani jinsi juisi ya machungwa inavyotengenezwa kiwandani. Undani huo umo kwenye kitabu chake cha; ‘Squeezed: What You Don't Know About Orange Juice'. (Kitu usichokijua kuhusu juisi ya machungwa).

  Katika kitabu hicho, mwanadada huyo anasema kuwa ni muhimu kila binadamu kujua kwa undani jinsi chakula chake kinavyoandaliwa, kwa sababu maelezo au lebo inayowekwa kwenye boksi, siyo tu haisemi ukweli, bali pia hailezi ukweli wote.

  Anasema kwamba, kama kweli ‘pure orange juice' tunayokunywa ilipatikana baada ya kukamuliwa chungwa peke yake na kuwekwa kwenye boksi, basi bila shaka ladha ingekuwa tofauti kati ya boksi moja na lingine, kwa sababu chungwa moja linatofautiana ladha na chungwa lingine. – mengine matamu, mengine makali.

  Mbali na hilo, kila kampuni inayotengeneza juisi ya machungwa ina ladha yake. Juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Tropicana ina ladha tofauti na juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Ceres, sababu ya tofauti hiyo inaacha maswali mengi zaidi kuliko majibu.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Aidha, Hamilton anaendelea kueleza mchezo mchafu unaochezwa na watengeneza juisi viwandani kwamba ladha ya juisi hiyo ya machungwa hutofautiana pia kati ya nchi na nchi, kwani viwanda huweka aina ya ladha kwenye chungwa kulingana na vile ambavyo wanapenda watu wa eneo inakokwenda.

  Juisi inayotengenezwa kwa ajili ya nchi za Amerika Kaskazini huwa na kiwango kikibuwa cha kirutubisho aina ya ‘ethyl butyrate', ambacho ni moja ya kemikali inayotumika sana kwenye utengenezaji wa manukato na ladha. Mbali ya kirutubisho hicho kuwa na uwezo wa kutengeneza aina mbalimbali za ladha za matunda, lakini pia hakina gharama (cheap).

  HATUA GANI ZA KUCHUKUA SASA?
  Kama makala haya yatakuwa yamekushitua na kukushangaza, jua hauko peke yako. Hata hivyo, lengo kubwa la makala haya ni kukufumbua macho ujue juisi unayokunywa siyo salama kiasi gani na uwe na uamuzi wa kuicha au kuendelea kuitumia kwa hiyari yako mwenyewe, lakini siyo kwa kudanganywa na maelezo ya uongo ya kibiashara yanayowekwa juu yake.

  Kama ambavyo mwandishi wa kitabu hicho Bi. Hamilton anavyosema: "Lengo la kitabu changu siyo kukataza watu kunywa juisi, isipokuwa kuwafanya wakijue vizuri wanachokinywa. Watu wana haki ya kujua ni kwa kiasi gani utengenezaji wa juisi hivi sasa umekuwa wa kibiashara zaidi, hii itawafanya wawe na maamuzi sahihi kuhusu afya zao."

  Ingawa ni vigumu sana kuepuka ‘kuingizwa mkenge', lakini unaweza kujiepusha na madhara ya kiafya yatokanayo na unywaji wa juisi hizi ‘feki' kwa kupendelea kunywa juisi uliyoitayarisha mwenywe nyumbani na kuacha kununua vyakula au vinywaji ‘ready made', hasa kwa vile ambavyo vinapatikana kwa wingi sokoni.

  TAHADHARI
  Kwa ujumla matunda na juisi zake zina virutubisho vingi muhimu kwa ustawi wa afya ya binadamu, lakini tahadhari inatolewa kwa wanaopenda kunywa kiasi kingi cha juisi za matunda, hasa juisi ya machungwa ambayo inaelezwa kuwa na sukari nyingi.

  Kiasi cha glasi moja ya juisi ya machungwa ina wastani wa gramu 25 za ‘fructose', (sukari), kiwango ambacho ni cha mwisho kabisa anachotakiwa mtu kutumia kwa siku moja. Hii ina maana kama utakunywa zaidi ya glasi moja pamoja na vinywaji vingine vinavyotumia sukari, kama vile chai, tayari utakuwa umezidisha kiwango kinachopendekezwa kwa siku.

  Iwapo utakuwa na tatizo la unene na unahitaji kupunguza uzito, ni vyema ukapunguza sana au ukajiepusha kabisa na uywaji wa juisi za matunda, kwa sababu kiwango cha sukari kilichomo ni zaidi ya wastani unaotakiwa.

  Ili upate faida za virutubisho vinavyopatikana kwenye matunda, yakiwemo machungwa, unashauriwa kula matunda hayo kama yalivyo kuliko kukamua juisi na kutupa makapi yake. Inaelezwa kwamba sukari iliyomo kwenye chungwa inapoliwa pamoja na nyama zake (fibre), sukari hiyo huwa haina madhara kwani huweza kujichanganya kwenye mfumo wa damu bila kuleta athari zozote kwa mlaji.

  Hivyo ushauri wa ujumla unatolewa kwamba pendelea zaidi kula matunda na mboga za majani kama zilivyo kuliko kunywa juisi zake. Kwa kufanya hivyo utajiepusha na uwezekano wa kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Iwapo utakunywa, basi kunywa nusu glasi au isizidi glasi moja kwa siku. Asanteni.
   
 3. c

  chi-boy Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante kwa hilo..
   
 4. BCR

  BCR Senior Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  point noted & taken
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana dokta mzizimkavu. Kuanzia leo nitaacha hizo juice za box.
   
 6. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  okey. note taken
   
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Matunda tunayo, kwanini tule vya kwenye maboksi?
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  @Kiranja Mkuu hilo nalo neno muhimu sana.
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tusiinge mambo ya kigeni bali tutumie mazao yetu ya asili tutapunguza magonjwa mengi sana kwa kuwa nchi yetu imebarikiwa kila sehemu ina neema yake tuleni sana (Parachichi,Ndizi, machungwa,magimbi,zabibu, matango, tikitimaji,etc) yanapatikana pande zote za nchi
   
 10. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ngoja niwahi shamba nikachume ya mtini.
  OTIS
   
 11. Zuia Sayayi

  Zuia Sayayi JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 834
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  God bless u man!
   
 12. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Thanks alot pal! Unajua kwa muda mrefu nilikuwa napendelea kunywa juice ya mapera ya Azam. Ilinishangaza sana kuona ladha yake haibadiliki. Kipindi hiki mapera yanapatikana, hivyo juice ya mapera kwa sasa ni home made. Imenishangaza mno kwa kuwa ladha yake ni tofauti mno na ile ya boksi! Kwa sasa ni zaidi ya mwezi natumia juice ya mapera ya hapa home.
   
 13. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Mimi nilacha kunywa juice hizi muda mrefu sana.Ziliniongeza uzito sana mpaka zikanigharimu muda na pesa kuushusha uzito sana
   
 14. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Thanx for reminding us Mzizi,
  Ndiyo maana mimi hutumia juisi ninayotengeneza mwenyewe tuu!
   
 15. M

  Mimi k Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ubarikiwe sana!
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  @SILENT ACtOR inakuwa jambo zuri kutengeneza wewe mwenyewe juisi yako kwa kutumia mashine ya Blender ni vizuri sana.
   
 17. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  mkuu mimi kwa sasa nakunywa maji tu, nina mwaka na miezi mitano tangia niache kutumia juice za makopo na soda, mkuu swali langu liko kwenye juce ya Rozela vipi hii juice ina faida zipi?

   
 18. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Matunda yenyewe pia yanapigwa dawa ile mbaya. so ni dawa juu ya dawa
   
 19. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kama upo karibu na shamba ni vizuri uende ukachume matunda na kama unataka juice tengeneza mwenyewe nyumbani na ule wakati huo huo. Lakini kuna wenzetu wapo mbali na mashambani hivyo jinsi ya kupata matunda na virutubishi vyake ni kuyachakata na kuyahifadhi kwenye maboksi au chupa. Kiukweli haiwezi kuwa 100% purity kama ya shambani lakini angalau ataambulia at least 60% purity kama yatachakatwa na kuhifadhiwa vizuri. Na hizi preservatives na additives zipo nyingi ambazo zimethibitika kutokuwa na madhara kwa mlaji na kuruhusiwa kwa kupewa namba.
  After all, ukichukua chungwa ukakamua juice na kuweka kwenye chupa bila kuweka preservatives ni bure kwani itaharibika muda si mrefu, hivyo kukabili upotevu wa matunda/vyakula wakati mwingine ni bora kuchakata na kuhifadhi ili matunda yaweze kukaa kwa muda mrefu na kuwafikia watu wengi na pia kupunguza uharibifu wa chakula!
  Labda hapa hoja ni udanganyifu wa kusema 100% purity wakati sio kweli...
   
 20. d

  debon Senior Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  asante
   
Loading...