Bonge La Afya
Member
- Dec 19, 2016
- 35
- 83
Hakuna kitu kikubwa na muhimu humu duniani kama kuishi ukiwafanya watu wanaokuzunguka pasipo ubaguzi wowote ( Walemavu na wale walio na mahitaji kama yatima na wazee) kuwa na furaha na amani wakati wote na hasa pale utakapokua karibu yao,
Binadamu sote tungeishi kwa kufuata yale maneno tunayoambiwa au kuyasikia kila siku kutoka kwa aidha wachungaji wetu, wazee wetu au wenzetu waliotutangulia ambayo maneno haya wengi wetu tumeyageuza maana na hayatusaidii chochote kwani tumeyafanya yawe maneno ya kuweka mitandaoni kutufanya tuonekane tuna hekima.
Nikuambie tu ewe ndugu yangu leo, Kutumia maneno ya hekima pasipo kuitumikia hekima yenyewe unafanya kazi bure, Haikusaidii wala haikubadilishi chochote kwani sisi kama watu tunaokuzunguka tunakufahamu vizuri na tutabaki kuwa mashahidi wako popote uendapo.
Nakukumbusha tu hii dunia tunapita hivyo Kila mtu ana mtu wake, kila muonekano una mvuto wake, kila umbile lina tunu yake na kila hulka ina mwenziwe. Hakuna aliye mbaya kwa wote, mzuri kwa wote au mwenye kumfaa yoyote. Kila mtu na maradhi yake.