Mwiyuzi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 853
- 440
Poleni na kazi za wiki nzima Wakuu!
Ni weekend ya kurelaxxx
Nimeona leo tujikumbushe enzi zileeeee
Nikiwa mdogo nilikuwa sipendi kula chakula kingi ila nilikuwa napenda mboga kama nyama au samaki, wasiponiangalia wakati wa kupakua wanaumia! Nilikuwa najijazia mboga kiukwelii...nilikuwa na umri kama wa miaka 6-8
Mama akanidhibiti kwa kunieleza kuwa, kila wakati ninapopakua mboga niwe nawakumbuka wenzangu ambao hawajapakua.
Tokea kipindi hicho mpaka leo huwa kila nikitaka kupakua lazima nikumbuke ambao bado hawajapakua. Hivyo mama alinifundisha nidhamu wakati wa kula tokea enzi zile mpaka leo nakumbuka.
Vipi wewe unakumbuka lipi ambalo mama alikurudisha kwenye reli?