Kitu gani haramu unaweza kuhalalisha nchini?

Mimi nafikiria wakiruhusu malaya na kuwatoza kodi umalaya yaani ukahaba yaani watapunguza kujiuza madada poa kama itakuwa ruksa na kutakiwa kulipa kodi - uchangudoa utapungua Kwa kiwango kikubwa

Bangi pia ikipitishwa na ziuzwe kwa kulipishwa kodi na mvutaji alipe kodi pia itapunguza vichaa wengi mtaani

Uchawi utambulike kiserikali na ikitokea mtu kamloga mtu ashitakiwe Kwa sheria na katiba ya nchi- tutapinguza kasi nyingi ya misukule na kutiana ulemavu na ukichaa

Na mengine kibao
 
1. Uraia Pacha
2. Uzalishaji wa Pombe za kienyeji (pombe za kienyeji kama gongo kwa sasa ni haramu)
 
Katika uhalalishaji haramu na kuharamisha halali ningependa #bangi ihalalishwe na #uvunaji wa mazao ya misitu iwe haramu.
 
Back
Top Bottom