Kitovu kikubwa cha mtotoo

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,628
10,242
-Naomba kufahamu,mtoto ana miezi saba,ila kitovu chake ni kikubwa ,Je hili ni tatizo ?!
 
Kwa mm navyojua sio tatizo kwani wapo watoto wenye hali kama hiyo na ni wazima!

Kwa ushauri muone dakitari
 
Iliwahi kutokea kwa kijana wangu niliambiwa niweke sh 200 na kumfunga na plasta kwa muda kama wa mwezi mmoja. It worked kitovu kilirudi ndani
 
Hapana kitarudi ,ila kwa ushauri kuna Dr moja wa watoto pale ilala bungoni Jahaa dispensary .Alitusaidia kwa kijana wangu
 
Nenda Kwa Dokta Haraka Sana! isijekuwa ana "Umbilical Hernia" ikaja ikawa balaa la bure Baadae!
 
Usijali ni tatizo la kawaida mtoto akifikisha miezi 18 kitaisha chenyewe. Kama hapati shida kuumwa tumbo huna haja hata ya kumwona daktari.
 
Iliwahi kutokea kwa kijana wangu niliambiwa niweke sh 200 na kumfunga na plasta kwa muda kama wa mwezi mmoja. It worked kitovu kilirudi ndani

Ni kweli kabisa mkuu mi kijana wangu wakati anazaliwa alikuwa na kitovu kidogo, baada ya wiki mbili akaanza kulia mfululizo basi kitovu kikawa kikubwa balaa.
nilipata ushauri kama wako nikawa namfunga shilingi kumi kwa plasta kwenye kitovu chake, ndani ya mwezi mmoja kitovu chote kushney.
 
Back
Top Bottom