Kitoto kichanga kilichotupwa jalalani


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,351
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,351 280
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/kitoto-kichanga-kilichotupwa-jalalaniNa,Jumbe Ismailly,Singida

POLISI Mkoani Singida wanamtafuta mwanamke mmoja aliyezaa na kisha kukitupa kwenye pagara la nyumba iliyopo Mtaa wa Majengo,katika Manispaa ya Singida kitoto kichanga chenye umri wa takribani miezi saba akiwa tayari ameshakufa.

Akithibitisha tukio hilo kamanada wa jeshi la polisi Mkoani Singida,Bi Celina Kaluba alisema licha ya mwanamke huyo kutofahamika,lakini jeshi hilo linaendelea kufanya jitihada za kumtafuta ili liweze kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Hata hivyo Uwazi ilipofika kwenye eneo la tukio majira ya saa kumi jioni ilishuhudia mwili wa kichanga hicho ukiwa umetupwa na huku ukiwa umezingirwa na mainzi mengi na pia umekaribia kuoza kabisa

Kutokana na kitendo hicho cha kinyama wananchi wa eneo hilo la tukio walionekana kutoridhishwa na kitendo kilichonywa na mwanamke huyo ambaye hadi sasa bado hajafahamika.
Akizungumza na Uwazi kwenye eneo la tukio mmoja wa wakazi wa maeneo hayo,Bi Hadija Ramadjhani licha ya kulaani tu kitendo hicho kilichofanywa na mwanamke mwenzake,lakini akaongeza pia kwamba mbali ya kuwa ni dhambi kwa mwenyezinmungu,vile vile ni kitendo cha kinyama na kisichostahili kuvumiliwa.
"Mwanamke huyo,kweli ni mwanamke mwenzangu hana budi kulaaniwa kwa maana hinaonekana kuwa hakuwa na haja ya mtoto sasa alibeba mimba ya nini hata kama iliingia kwa bahati mbaya lakini hakuwa na sababu ya kufanya kitendo cha kinyama kama hiki"alisisitiza Hadija huku akionekana kuchirizika machozi.

Kwa upande wake mmoja wa wanaume waliokuwepo kwenye eneo hilo la tukio,Bwana Juma Hamisi pamoja na kukiri kwamba kitendo hicho ni cha kinyama,lakini hata hivyo hakusita kuweka wazi kwamba wananchi wa Mtaa wa Majengo watafanya msako mkali na wa siri hadi kumbaini mwanamke huyo aliyetupa kichanga hicho na hatimaye kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

"Kwa kweli siyo siri mimi binafsi kitendo hiki kinaniuma sana kwani tangu nimeoa takribani miaka 11 hivi sasa sijafanikiwa kupata mtoto na ninapoona mtu anatupa mtoto,roho yangu inaniuma sana wakati mimi namtafuta kwa miaka 11 sasa bila mafanikio na sijui majaliwa ya Mwenyezimungu kama nitafanikiwa"alisisitiza Bwana Juma huku akionyesha kukerwa na kitendo hicho.

Katika hali ya kushangaza licha ya gazeti hili kuomba ushirikiano kwa Afisa tarafa wa Mungumaji,Bwana Ally Mwendwa,lakini hakuwa tayari kutoa ushirikiano huo zaidi ya kukataa katakata kutoa maelezo yeyote yale kwa madai kwamba yeye siyo msemaji wa eneo hilo na kuwataka wanahabari waliokuwa kwenye eneo hilo wamtafute Afisa mtendaji wa kata ya Manjengo,ambaye kikazi yuko chini yake.

"Mimi siyo msemaji,kwa kweli tukio nimeliona lakini siwezi kusema chochote kile kwani siyo msemaji mtafuteni mtendaji wa kata yeye ndiye anaweza kusema siyo mimi"alisema huku akiwasha pikipiki yake na kuondoka kwenye eneo la tukio huku wananchi wakimkodolea macho na kumshangaa.

Chanzo: Global Publishers

Hawa wanawake wengine kama hawawataki Watoto si watupe sisi tunaowataka jamani? Mbona huu ni Ukatili mkubwa sana!!!!!!!!!!
 
D

dr chris

Member
Joined
Sep 23, 2011
Messages
77
Likes
0
Points
0
Age
45
D

dr chris

Member
Joined Sep 23, 2011
77 0 0
hakika kitendo hiki kinapaswa kulaaniwa na kila mtu mwanamke huyu amemkosea mungu na wanadamu pia,alishndwaje hata kumpeleka kwenye vituo vya kulelea watoto yatma! kwa yeyote anaemfahamu mama huyo asaidie jesh la polis ili huyu mama aieleze jamii yaliyomsibu mpaka kufanya unyama huo.ilibidi picha yake ikipatkana itundkwe kwenye mtandao wa jf kwan mndao huu upo tz kila kona
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,351
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,351 280
hakika kitendo hiki kinapaswa kulaaniwa na kila mtu mwanamke huyu amemkosea mungu na wanadamu pia,alishndwaje hata kumpeleka kwenye vituo vya kulelea watoto yatma! kwa yeyote anaemfahamu mama huyo asaidie jesh la polis ili huyu mama aieleze jamii yaliyomsibu mpaka kufanya unyama huo.ilibidi picha yake ikipatkana itundkwe kwenye mtandao wa jf kwan mndao huu upo tz kila kona
Ana njaa ya Maisha mimi ninahisi atakuwa ni mwanafunzi wa shule eidha shule ya Msingi au shule ya secondary......... Huo ni unyama wa hali ya juu ehhhhh
 
Anko Sam

Anko Sam

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2010
Messages
3,212
Likes
24
Points
135
Anko Sam

Anko Sam

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2010
3,212 24 135
Huyo aliyekitupa kichanga hicho akikamatwa, azibwe na superglue ili iwe fundisho kwa wengine!
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,351
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,351 280
Huyo aliyekitupa kichanga hicho akikamatwa, azibwe na superglue ili iwe fundisho kwa wengine!
Sasa akizibwa na superglue si atashindwa hata kwenda haja ndogo? Ni hatari hiyooooooo
 
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Messages
14,344
Likes
5,360
Points
280
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2011
14,344 5,360 280
:A S-heart-2::rip::rip::rip::A S-rose::A S-rose:
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,351
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,351 280
attachment.php?attachmentid=38128&d=1317436839


Binadamu ni watu wanyama zaid kuliko hata huyo mnyama ahhhh kwanini amezaa kisha kukitupa hichi kitoto? Mbuzi Mzee
 
Last edited by a moderator:
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,379
Likes
2,858
Points
280
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,379 2,858 280
Miezi saba?...ni mimba imetolewa au ni mtoto alizaliwa premature?
 

Forum statistics

Threads 1,238,115
Members 475,830
Posts 29,311,160