Kitochi cha Tigo ni Utapeli Uliopitiliza

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Mimi ni mmoja ya wateja waliohamasika kununua simu ya kitochi inayotangazwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo lakini baada ya kufika katika ofisi zao zilizopo blue house jijini Arusha ,liliambiwa lilipe advance ya sh, 20,000 ili nipatiwe order ya simu hiyo na baada ya simu kuja nimalizie malipo ya sh,29000 kwani simu hiyo zitatoka kwa order kwa mauzo ya sh,49000. Badala ya 47500 wanayotangaza.

Lakini Tangu nimetoa hiyo sh,20,000 wiki tatu zimepita zijawahi kupigiwa simu kuarifiwa kama simu yangu imekuja huu ni utapeli wa hali ya juu sana hawa Tigo wamekuwa kampuni ya kitapeli

Nimewaambia warudishe pesa yangu lakini hawataki wananiambia nisubiri simu inakuja huu si wizi jamani,wadau hebu nisaidieni nifanyaje.
 
Okay hapo sasa kitochi sio utapeli ila wewe ndio umetapeliwa.
Kweli mkuu hata mimi nilidhani ametumia hiyo simu na kuiona feki kumbe yeye kaingizwa kichwa... Haiwezekani simu ya bei ndogo hivyo ilipwe kwa awamu mbili
 
Simu Zimejaa Tele, Wewe Unatoa Pesa Mbele Kama Tai Ya Msabato, Nenda Kachukue Chako
Zikija Unakwenda Kuwalipa. Vinginevyo Unaibiwa Unajiona
 
Badili heading isomeke kuwa umetapeliwa!
Halafu kwani ulishikiwa bunduki utoe hiyo hela?
si ulitoa kwa maprnz yako!
 
Mi niliwaambia nitasubiri zije,kwanzia lini simu ya kitochi ikawa deal,zimekuja zantel na nikapata
 
Kweli maisha magumu.. Elf 20 unaanzishia uzi kabisa?
Ishu sio 20k, ishu ni kudanganywa, kudanganywa na taasisi kama hiyo ambayo mtu aliiamini kutokana na jina kubwa, inatia hasira na kushangaza.
Mwenyewe ningetapeliwa hata 10k na tigo ama voda ningeanzisha uzi,
 

Usisahau kuja na 20,000 cash bro!
 
wanasubiri idadi iwe kubwa ndipo waagize, vumilia, vinginevyo ungechukua ya Voda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…