Kitimtim bungeni

Kitimtim bungeni

ndugai.jpg
Mambo haya ni magumu sana. Kazi ya Jaji Mkuu ni kulinda mhimili wa mahakama tena kwa wivu kabisa na kazi ya Spika ni kulinda Bunge tena kwa wivu mkubwa,” alipoyasema hayo alishangili.” Ndugai
Na Boniface Meena, Mwananchi

Posted Novemba22 2014 saa 11:36 AM
Kwa ufupi

  • Kauli hiyo ya Zungu aliitoa jana bungeni baada ya wabunge kuanza kuhoji kuwapo kwa taarifa za barua ya mahakama kutaka kuzuia mjadala wa ripoti hiyo.


SHARE THIS STORY

0
inShare​




Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge, Muss Azzan Zungu amesema kuwa ripoti ya uchunguzi wa sakata la Tegeta Escrow itawasilishwa bungeni kama ilivyopangwa na kwamba hakuna zuio lolote la mahakama linalotaka suala hilo lisijadiliwe bungeni.


Kauli hiyo ya Zungu aliitoa jana bungeni baada ya wabunge kuanza kuhoji kuwapo kwa taarifa za barua ya mahakama kutaka kuzuia mjadala wa ripoti hiyo.

Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala (CCM) alisema, “Nitoe taarifa tu ya kiti kwamba hakuna barua yoyote ya mahakama iliyozuia kujadili Escrow. Uhusiano wa Bunge na mahakama ni mzuri mno,” alisema Zungu na kuongeza:

“Hakuna katazo lolote, hakuna zuio lolote.”

Alisema ripoti hiyo itawasilishwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini(Chadema), Zitto Kabwe kama ilivyopangwa.

Juzi na jana madai ya kuwapo kwa barua hiyo yalizua mtafaruku bungeni na wabunge wa pande zote mbili waliwasha moto wakitaka kujua kama kuna ukweli wowote kuhusu barua hiyo.

Wabunge David Kafulila (Kigoma Kusini), Esther Bulaya (Viti Maalumu), Lekule Laizer (Longido), Peter Msigwa (Iringa Mjini), James Lembeli (Kahama) na Tundu Lissu (Iramba Mashariki) walitaka kujua ukweli kuhusu barua hiyo na kama kweli ipo basi jaji aliyeiandika awekwe mezani ili ajadiliwe.

Hali hiyo ilimfanya Naibu Spika, Job Ndugai juzi kusema, “Mambo haya ni magumu sana. Kazi ya Jaji Mkuu ni kulinda mhimili wa mahakama tena kwa wivu kabisa na kazi ya Spika ni kulinda Bunge tena kwa wivu mkubwa.” Alipoyasema hayo alishangiliwa na wabunge.

Alisema wakati Sitta alipokuwa Spika aliwahi kuwaambia kuwa, “tukiwa viongozi hatuwezi kutengeneza umoja katika maovu.”

Ndugai alisema kutokana na kauli hiyo, Bunge haliwezi kuficha uovu katika jambo hilo na kwamba litashughulikiwa vizuri na haki itatendeka.
 
Hizi mada ni ngumu sana kwa LB7. Sijui kama wataingia humu! Tusubiri tuone maana nchi hii vibweka vimekuwa ni hali ya kawaida ya kila uchwao. Maana mijamaa kwa kujitoa akili!
 
Katika awamu ya Uongozi ulotia fora kwa ufisadi na majanga mengi Tanzania, hii awamu ya Kikwete imekua TOO MUCH ,Sijuwi nikua yeye mwenyewe kwakua ana maskandar kibao ndio ikabidi na yeye mafisadi wahemukwe kufanya watakavyo bila ya uongozi imara?.

Tanzania inaliwa na wenye meno, imekua kila kiongozi anaiba na kulilimbikizia mamali kicha anakaa upande anambisha mwengine, imekua kama mbio za vijiti kupokezana?.

Hali hii nikweli Watanzania wataweza kuchupa mtego wa Umaskini na kuwa na maisha bora kwa wote?.
Mimi naona hao nchi za donators zenye kusaidia Budget ya Tanzania kila Mwaka watashindwa kwa vile pesa yote inaingia kwenye a/c za vigogo na kujinufaisha wao na familia zao.

ulaji wa viongozi wa Tanzania niwakutisha ,wanakula kwa matonge ,hivi juzi nilishtuka kusikia kila kiongozi wa Tanzania kwenye a/c yake kuna billion 160 zimekaa tu mbali aseti za majumba na mashamba ,washini anambiwa huyo hana kitu basi ana billion 40 huyo ndio hahe hahe.

Sasa kweli tanzania na Watanzania watapata maisha bora kweli haliyakua kila kiongozi wa ccm ni mwizi wa mabilionea? na hali yakua bado Watanzania tunambiwa ni watu wa pole na Tanzania inapigiwa mfano wa aman? hii Amani ya kukaa kimya Watanzania ndio nyimbo ya kuchombezwa na viongozi ili waibe pasipo hofu.

Tukiendelea kuwa kimya Wananchi basi , hali zetu za maisha zitazidi kua duni na wachache ndio watakao miliki rasilimali za nchi hii yote, hivi sasa ukiangalia Mahospitali ,Maskuli, masupwermarket yote ni miliki za vigogo kwa pesa zatu za wizi , lakini tunakangwa kwa mafuta yetu wenyewe.

Wanaua hospitali za Serekali wanajenga zao ili kuzidi kutubana wananchi, kama umma haujaja juu basi itakua mchezo ni huu huu kiongozi anaiba anakaa pembeni anambicha mwenzake na yeye anaiba anakaa pembeni anampisha mwengine mpaka nchi inafilisika kabisa .

Na ndio ukaona viongozi ukija na swala la kuwahukumu mafisadi hukingiana vifua kwa kua wote si wasafi ni wezii tu wa mali za umma ukiwa Umma wenyewe unachombezwa kwa nyimbo za Amani na Utulivu .
 
Back
Top Bottom