Kitimoto chamharibu Wema

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
WEMA.jpg
Siku chache baada ya kubainika kuwa, Miss Tanzania 2006-07 ambaye pia anatisha katika tasnia ya filamu nchini, Wema Isaak Sepetu ni mtumiaji mzuri wa nyama ya Nguruwe ‘Kitimoto’, imeonekana kuwa msosi huo umeanza kumharibu kwa kutokwa na minyama uzembe.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, kwasasa mrembo huyo ameongozeka unene na kuwa na ‘shavu dodo’ tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma kidogo, huku utumiaji wa nyama hiyo ukitajwa kama chanzo.

Akiongea na Mwandishi Wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, ulaji wa Kitimoto kwa Wema huenda ukamuathiri kwani kwa muda mfupi ‘figa’ yake imeanza kubadilika.

“Yaani Wema kwa Kitimoto usimpimie kabisa, lakini sasa ulaji wa nyama hiyo umeanza kuuharibu mwili wake kwani katoka minyama uzembe, nimekuwa nikimshauri ale kwa kiasi lakini mwenyewe anaona sio ishu,”alisema shoga huyo wa karibu na Wema.

Katika siku za hivi karibuni, Wema alinaswa akipata nyama ya Kitimoto pamoja na ndizi za kuchoma katika baa moja bubu iliyopo nyuma ya Ukumbi wa Africentre uliopo Ilala jijini Dar es Salaam huku akishushia na kinywaji murua kisicho na kilevi.

Msanii wa filamu ambaye anajulikana zaidi kwa ‘taito’ ya Pacha wa Uwoya, Jacqueline Wolper amepigwa chini kwenye shindano la kusakata muziki, maarufu kama Serebuka.

Za chini chini zinadai kuwa, Pacha wa Uwoya ameburuzwa out ya mashindano hayo yanayosindikizwa hewani na runinga ya TBC1 baada kuwa mtoro kwenye mazoezi.

Aliposakwa kwa simu na kijiwe hiki, Jack hakupatikana hata.

globalpublishers.info - Portail d'informations
 
sasa mnataka mzee wa meza aka mbuzi katoliki aliwe na nani? mwacheni mrembo ajinome bana! Kwani kunenepa ndiyo nini? Si ndiyo uzuri wa mwanamke wa kiafrika? Yaani watu wengine bana wanashangaza sana wanaposhabikia umbao a.k.a njia ya reli au pasi. Huo si wetu, ni wa watu weupe (wazungu).
 
Ila binadamu kweli hatuwezekani ukinenepa kosa ukikonda kosa ..kwani anaenda kushindania umiss tena
Wema kula ile kitu inapenda na hasa ukiwa na appetite ...kuna wengine chakula kinashindikana hata kupita mdomoni
kwa raha zako enjoy.
 
Thats her..ameamu mwenyewe, ni mtu rational, ana akili zake na hisia, anapenda, anapendwa, ana matamanio, ana principles katika maisha yake, yuko huru, ana uchaguzi....KWAHIYO AACHWE AFANYE ANACHOTAKA...HUH!
 
Wema ndugu yangu KULA KABLA HUJALISHWA, kuna watu wako pale Muhimbili sasa hivi wanakitamani chakula mdomoni hakipiti hata kiduchu. Ili mradi usipitilize ikawa mbaya kwa afya yako. Sisi ni waafrika mwanamke kuchanika babu!!!!!! Jamani hata hivyo huyu Wema anakuwa mkubwa sasa mwanadamu ananenepa pia kutokana na umri wake, jinsi umri unavyokuwa mkubwa na uzito pia unaongezeka kiasi fulani.

Halafu watu wengine wananenepa kwa stress, isitoshe labda mchuchu kamwambia anenepe ndiyo atampenda zaidi.
 
Tandika KM mama kwenda mbele lakini piga sana ile ya kukausha, kachumbari safi nyingi...rost ndo unene..punguza bia, piga whisky au Konyagi..hapo makali ya unene yatapungua..Kitimoto kwa Afya zetu bana.
 
She is what they call "Thick Madamme", an African figure, good. Aongeze anapendeza zaidi
 
habari za magazeti ya bongo bwana! hiyo ndo imejaza ukurasa mzima habari ya kuwa wema anakula kiti moto kanenepa!

nawasikitikia wale wanaonunua magazeti hayo ....duh
 
Jamani huyu Wema si alibadili dini akawa muislamu wakati anapigwa na yule msela wake wa migo migo? Au ndio mambo yale yale ya UKIRO? Mdudu mtamu lakini, muacheni tu na si mnajua ile ni dawa.Kula tu mwaya.:target:
 
habari za magazeti ya bongo bwana! hiyo ndo imejaza ukurasa mzima habari ya kuwa wema anakula kiti moto kanenepa!

nawasikitikia wale wanaonunua magazeti hayo ....duh

halafu umeona hapo wamechanganya cjui nani kaenguliwa kwenye kitu gani, yaani ili mradi shaghala baghala......
 
Ila binadamu kweli hatuwezekani ukinenepa kosa ukikonda kosa ..kwani anaenda kushindania umiss tena
Wema kula ile kitu inapenda na hasa ukiwa na appetite ...kuna wengine chakula kinashindikana hata kupita mdomoni
kwa raha zako enjoy.

hahaaaa umenikumbusha ....
'nikikonda ninao, nikinenepa nimeanza dozi'.........

kazi kweli kweli mwacheni ajilie vyake, maisha yenyewe yako wapi

WEMA: angalia tu usije ukapata kifafa
 
Siku chache baada ya kubainika kuwa, Miss Tanzania 2006-07 ambaye pia anatisha katika tasnia ya filamu nchini, Wema Isaak Sepetu ni mtumiaji mzuri wa nyama ya Nguruwe ‘Kitimoto’, imeonekana kuwa msosi huo umeanza kumharibu kwa kutokwa na minyama uzembe.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, kwasasa mrembo huyo ameongozeka unene na kuwa na ‘shavu dodo’ tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma kidogo, huku utumiaji wa nyama hiyo ukitajwa kama chanzo.

Akiongea na Mwandishi Wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, ulaji wa Kitimoto kwa Wema huenda ukamuathiri kwani kwa muda mfupi ‘figa’ yake imeanza kubadilika.

“Yaani Wema kwa Kitimoto usimpimie kabisa, lakini sasa ulaji wa nyama hiyo umeanza kuuharibu mwili wake kwani katoka minyama uzembe, nimekuwa nikimshauri ale kwa kiasi lakini mwenyewe anaona sio ishu,”alisema shoga huyo wa karibu na Wema.

Katika siku za hivi karibuni, Wema alinaswa akipata nyama ya Kitimoto pamoja na ndizi za kuchoma katika baa moja bubu iliyopo nyuma ya Ukumbi wa Africentre uliopo Ilala jijini Dar es Salaam huku akishushia na kinywaji murua kisicho na kilevi.

Msanii wa filamu ambaye anajulikana zaidi kwa ‘taito’ ya Pacha wa Uwoya, Jacqueline Wolper amepigwa chini kwenye shindano la kusakata muziki, maarufu kama Serebuka.

Za chini chini zinadai kuwa, Pacha wa Uwoya ameburuzwa out ya mashindano hayo yanayosindikizwa hewani na runinga ya TBC1 baada kuwa mtoro kwenye mazoezi.

Aliposakwa kwa simu na kijiwe hiki, Jack hakupatikana hata.

globalpublishers.info - Portail d'informations
MKUU,KITIMOTO NI NYETTE
 
Back
Top Bottom