BOSS si walikuwepo wale makaburu wauza stationeries toka South Africa ambao waliingizwa na Mkapa kwa mtutu wa bunduki lakini kazi ikawashinda? Hata Wazungu pia hufanya madudu mengi tu.
Mie naamini wako Wabongo ambao wanaweza kabisa kuiendesha TANESCO ila tu wawe huru kuachiwa kuiendesha bila kuingiliwa na Serikali (Wizara ya Nishati) Angalia matatizo mengi sasa hivvi ya TANESO (Dowans, IPTL, mikataba ya Gas n.k.) Chanzo chake kikubwa ni Serikali (Nishati) Kwa mfano baada wataalamu wa TANESCO kuitathmini kampuni ya Richmond kabla haijaingia mkataba na Serikali wataalam wa TANESCO waliishauri Serikali kwamba Richmond haina uwezo wa kufua umeme hivyo isipewe mradi ule, lakini Serikali haikusikia ushauri wa wataalam wa TANESCO na yaliyotokea wote tunayajua.