Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,230
Kampeni za kituo kwa kituo, mtaa kwa mtaa zinazofanywa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Professa Kitila Mkumbo zimeendelea kusonga ambapo Septemba 12, 2025 alikitembelea kijiwe cha kahawa kilichopo Tabata Mwananchi, jijini Dar es Salaam.
Alipotembelea kituo hicho alipata wasaa wa kuwaombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan, yeye mwenyewe na mgombea Udiwani wa Kata ya Makuburi Issa Ahmed Faru.
Pamoja na hayo Kitila alipata kusikiliza changamoto za wananchi eneo hilo na kujibu maswali ya wananchi ambapo mwananchi, Atway Mohammed alieleza changamoto ya ubovu wa barabara pamoja na kuchelewa kutolewa kwa takataka kunavyowaathiri, huku Iddy Mussa(muuza kahawa) akisisitiza umuhimu wa utatuzi wa changamoto ya ubovu wa barabara.
Hata hivyo Atway alisisitiza imani yake kubwa kwa Kitila akimuomba asiwaangushe wamamchi wa eneo hilo kwani taifa lilishamuamini na kumpa jukumu zito na kuandaa Dira ya Taifa 2025-2050. Zoezi ambalo limemjengea heshima kubwa na uaminifu.