KITILA: Bajeti ya Maji Inatosha

Na hapo fedha inayoweza kutoka ni 20% tu. Sasa sijui kuna haja gani ya kuwa na bajeti kubwa ambayo haitekelezeki. Nafikiri wabunge wanatakiwa pia wasimamie ili hizo fedha za bajeti ziwe zinatoka.
Usiishi kwa mazoea, huu ni utawala mwingine.
 
ni changamoto labda anapata taarifa kutoka kwa watendaji, maana ukiangalia changamoto nyingi za wizara ni Budget kutokutosha kama wadau walivyosema hapo juu hata hii wizara. Kwa maelezo yake Vitu vyote vikibaki Constant na Budget ikawepo inawezekana. Lakini changamoto ya Maji nadhani kiuhalisia ni kubwa sana kuliko hata budget tunazowekewa na haichukui mwaka mmoja kutatuliwa. Ndio maana katibu kama mtaalamu anatakiwa kutoa analysis zake kisomi tuache pia kupeana matumaini kisiasa, maana hayo atasema Waziri ambae ni mwanasiasa zaidi...
 
Hiyo ndiyo siasa.

Hapo ndipo utaelewa vizuri, sababu ya taaluma ya siasa ikaitwa "Political Science' na siyo Political Arts"
 
Asante sana..
 
Ulitegemea aseme nini kama hana utaalam katika aspect hiyo? Aseme ameambiwa kuwa bajet inatosha!!!
 
NIMAPEMA KUMUITA MNAFIKI, NACHELEA HUSIJE UKAWA WEWENDIYE MNAFIKI.
YEYE NDIYE KATIBU WA WIZARA, ANAPOSEMA ZINATOSHA AMESHAFANYA MCHANGANUA WA MAHITAJI YA WIZARA YAKE.
CHA MSINGI SERIKALI ITOE HIZO PESA ZOTE THEN WIZARA WAKISHINDWA KUTATUA TATIZO LA MAJI NDIPO TUTAMUULIZA KITILA WHY ALISEMA ZINATOSHA!
 
Huyu naye anajipendekeza. Alipokuwa nje ya system alikuwa anapost post kwenye mitandao. Leo vipi tena?
Sio Kila kitu ni kujipendekeza Mkuu! Shida ya nchi hii sio hizo figure za kibajeti bali ni kuipata hio figure ili utekeleze mipango ya maendeleo. Kuna idara zilipata less dhan 20% ya zilichoomba katika bajeti inayoisha.
Hapo Kitila anasema kuwa kama hela hio ikipatikana yote, inatosha_sasa subiri utekelezaji. Shida bajeti ya nchi kwa sasa haieleweki maana ni ONE MAN SHOW! Mtapanga lakini yeye akiona haimpendezi anapiga chini
 
Itatosha kama kweli serekali itajitahidi kutoa hiyo fedha yote kwa muda muafaka.mara nyingi huwa wanatoa asilimia ndogo sana ya kiwango halisi kilichopitishwa kwenye bajeti,hivyo miradi mingi inakwama au inaishia njiani
 
Anapingana na kiongozi wake Zitto maana alisema bunge itake serikali kupanga upya bajeti maana haikidhi mahitaji
Kitila kaishapata ugali wake na kasema hajiusishi na siasa tena. Hivyo mkuu kifupi Kitila sifikiri kama ni ACT active member hivyo hana haja ya kumsikiliza Zitto.
 
Sasa yeye kama mtendaji mkuu kashasema inatosha lakini wanatokea watu wanampinga.
 
Na hapo fedha inayoweza kutoka ni 20% tu. Sasa sijui kuna haja gani ya kuwa na bajeti kubwa ambayo haitekelezeki. Nafikiri wabunge wanatakiwa pia wasimamie ili hizo fedha za bajeti ziwe zinatoka.

Na hicho cha 20% badala ya 100% ndio kikwazo kikuu! Ukiangalia Prof kasema kama ikitolewa yote!
So far naona watanzania wanatamani kuona Figure kubwa ambayo hata hivyo haitakuwepo badala ya figure ya kawaida realistic ambayo labda taifa litamudu.
 
Mwaka huu wa fedha.wamepelekewa around 34% ya mahitaji
Mwaka huu tena vilevile (in Bwege'voice aka mbunge wa kilwa)
 
pesa kwa miradi iliyopo na mipango inayoendelea,pesa km ikitoka yote inatosha ttz ni pale serikali inapitisha bajeti alafu inatoa asilimia 20 tu.
 
Yeye kwa sasa ndo Katibu Mkuu wa Wizara husika. Kwa hiyo anajua undani wa anachokisema. Ukiwa nje wakati mwingine unasema kwa sababu unakuwa hujui undani wa jambo.
Unahitaji kuwa ndani ya Wizara kujua kwamba bajeti hiyo kwa matatizo ya maji ya nchi hii, haitoshi haka kutatua robo ya tatizo lilopo? au ndiyo mambo ya maisha bila unafiki hayaendi?
 
Serikali inachotakiwa ni kuongeza vyanzo vya mapato ili iwe na fedha za kutosha iweze kuboresha huduma za muhimu kama maji,umeme,afya na elimu kinyume cha hapo kila mwaka itakuwa ni kupiga kelele kuwa bajeti haitoshi.
Mojawapo wa vyanzo vya mapato tulivyoongeza ni rambirambi na faini za trafiki! Likitokea janga tu mkichanga rambirambi sisi tunajengea miundombinu ya serikali na trafiki tumewapangia walete laki tano kwa siku kama faini ya usalama barabarani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…